Nimenasa kwenye ulimbo wa ndoa natamani kutoka nashindwa

Nimenasa kwenye ulimbo wa ndoa natamani kutoka nashindwa

Mimi ni kijana ambaye tayari nina miaka 30, nilifunga ndoa yangu mwaka 2019. Ndoa yangu imekuwa ya furaha kwa miezi 6 pekee baaada ya hapo mambo yaliharibika na sijui ni kwanini.

Nakumbuka siku moja natoka zangu kazini namkuta wife kajamu, nilipouliza kulikoni sikupata jibu, kuanzia hapo hatuna mawasiliano zaidi ya kuwasiliana kama kuna kitu kimepungua nyumbani nitapewa taaarifa.

Uchumi wangu umeyumba sababu ya hizi vurungu, nimefunga nakuomba hakuna ndoa haitulii kuna wakati nikiona mtu na mke wake wakitembea njiani huku wakipiga stori na kucheka naona nijambo la ajabu nijiuliza inawezekanaje hii?

Nimejaribu kushirikisha ndugu zake bado hatoi majibu nini ambacho nilimkosea. Kiukweli nimestuka baada ya watu wawili kuniuliza kwanini nakonda, kwanini sina amani kama zamani?

Mimi ndugu zangu ni bingwa wa kuvumilia matatizo lakini kwa hili nimenyoosha mikono nimeamua niondoke nikaaanze maisha mapya ili nipate amani ya moyo wangu, Mungu ataibarika kazi ya mikono yangu nitainuka tena.
pole sana mkuu, hata mimi napitia hali kama yako na wife alitembea mwenyewe, leo wiki ya pili" japo inauma ila hakuna namna.
 
Mpaka kifo kasema nani wewe, unaachwa tu chap ndoa inavunjwa mahakamani life linaendelea!
Unaoa kanisani alaf kuvunja ndoa unaenda kuvunjia mahakamani kwann huwez kuvunjia kanisani huko huko? Maana binadam wanatabia ya kubadilika mwanamke/ mwanume anaweza akaficha tabia yake ili aingie kwenye ndoa na baada ya hapo akaanza kukuonyeshea makucha pengine umeoa mshirikina alaf ukienda kanisani kutaka kumuacha kanisa linakataa linakwambia alicho kiunganisha Mungu binadam hawez kukitenganisha hii haijakaa sawa
 
Unafunga na kuomba kabisa? Mwanamke ndio anatakiwa kufunga na kuombea ndoa na familia yake, wewe unafungaje sasa....

Hilo la kufungasha na kuyimya ndio mpango mzima, kama mmejenga, mna watoto, we timua kaanze upya muachie nyumba na watoto, siku akisema amepata bwana wa kumuoa unamwambia aondoke wakaanze maisha upya.

Kila la heri mkuu na pole sana!!
 
Sikuamini swala la uajuza wako! Mpaka....

Jamaa akomae tu..[emoji28]
Usijifany tomaso wewe, kwahiyo unataka kapicha?! [emoji1787][emoji1787] , ila uzee jamani usikie kwangu tu mana kila kitu kimefikia ukomo. [emoji17][emoji18]

Ajikaze kiume bwana wee, atalia mpaka lini.
 
Mh! Hufanani na uchoyo mbona!.. halafu unakuwaje na haya mbele ya mjukuu..? Utakosa mume wa uzeeni shauliyo..😁
 
Mungu aliyetuamrisha tuonane, alitwambia ikifikia kuachana tuachane kwa wema, japo talaka ni jambo analolichukia lakini yeye mwenyewe ni kaliruhusu sababu anatujua waja wake, kama hataki mzee usishikile makali utakatika kiganja, mpe talaka yake maisha yaendelee.
 
  • Thanks
Reactions: Cyb
Fanya kweli chacha..[emoji28]
[emoji1787] umetafakari kwa kina lkn?! Mana juzi tu ulianzisha pambio hapa jinsi ulivyozama kwenye bahari ya huba...! Sie wazee tuna mengi usije ukahamisha kambi [emoji855]
 
[emoji1787] umetafakari kwa kina lkn?! Mana juzi tu ulianzisha pambio hapa jinsi ulivyozama kwenye bahari ya huba...! Sie wazee tuna mengi usije ukahamisha kambi [emoji855]
Silagi wazee mimi.. hata hapa anatuona tu!.. kambi haihami.
 
Ww husumbuliwi na ndoa unasumbuliwa na mapenzi.

Huyo hata angekuwa girlfriend angekutesa sababu unafunga na kuomba sababu ya mapenzi badala ya kuchukua hatua.

Kuna mambo ya kutatuliwa kiroho na kuna mambo ya kutatuliwa kimwili kwa kutumia ubongo wako uliopewa.

Mbona ngono hufanyi kiroho? Hufungi na kuomba mkeo ashike mimba?

Mwite mkeo muulize tatizo lipo wapi kama hakuna majibu ya maana mrudishe kwa mama yake.

HALAFU HAKUNA MAAJABU KWENYE KUMUACHA MWANAMKE USIYEMUELEWA. MKEO AJUE HILO PIA.
 
Ushauri safi sana lakin kuna mahala hapako sawa mleta Uzi akubali au akatae kuna mahali hapako poa
 
Inaonekana hujamzalisha, inaonekana hujampa mimba.

Ikiwezekana ongeza mke wa pili ufute machungu.

Umesema pia umefunga na kuomba lakini mambo ni yale yale, mungu hasaidii mkuu, kwenye hali kama hzo mungu hana msaada.
Acha kupotosha.Mungu ana msaada, sema ni kwa wakati wake siyo wakati unaotaka wewe na jinsi unavyotaka wewe.si mkuu endelea kumuomba Mungu yuko karibu kukujibu.Usiharibu uhusiano na Mungu wako just hajakujibu kwa hili kwa wakati uliotegemea.Uvumilivu hupimwa pia.Jaribu halikuwapata bali lile lenye mlango wa kutokea
 
Unaoa kanisani alaf kuvunja ndoa unaenda kuvunjia mahakamani kwann huwez kuvunjia kanisani huko huko? Maana binadam wanatabia ya kubadilika mwanamke/ mwanume anaweza akaficha tabia yake ili aingie kwenye ndoa na baada ya hapo akaanza kukuonyeshea makucha pengine umeoa mshirikina alaf ukienda kanisani kutaka kumuacha kanisa linakataa linakwambia alicho kiunganisha Mungu binadam hawez kukitenganisha hii haijakaa sawa
Dah mie hamna cha alichokiunganisha Mungu yani sitaelewaaa
 
Back
Top Bottom