Nimenasa kwenye ulimbo wa ndoa natamani kutoka nashindwa

Nimenasa kwenye ulimbo wa ndoa natamani kutoka nashindwa

Wadada wengi sikuhizi wanaolewa kwasababu ya kukata tamaa ya wanaowapenda, kuto kua tayari kuwaoa eiza kwa sababu za kiuchumi au zinginezo.
Wanaamua kuolewa na wasio wapenda ili kutimiza ndoto zao za kuolewa, au shinikizo la wazazi.

Pole sana mkuu,kama unauhakika upande wako hakuna tatizo basi Bwana wake Wa zamani ameshapata Pesa.
Usipo muacha tarajia lolote

Sent from my TECNO-W5 using JamiiForums mobile app
 
Pole son.

Ongea na mshenga japo najuwa mliishaongea pia ikashindikana.

Wazazi wako pengine wameshauri imeshindikana.

Usimwachie nyumba aweza pata majanga wakasema wewe ndo umemuua ukaishia jela.

Mchukueni umrudishe kwa wazazi wake. Kawakabizi mikononi, pengine atajutia aombe msamaha. Utulie kidogo kabla hujaingia mahusiano mengine.

Mtoto mpe mama yako amlee usimwachie mtoto.
 
Mimi ni kijana ambaye tayari nina miaka 30,nilifunga ndoa yangu mwaka 2019.Ndoa yangu imekuwa ya furaha kwa miezi 6 pekee baaada ya hapo mambo yaliharibika na sijui ni kwanini

Nakumbuka siku moja natoka zangu kazini namkuta wife kajamu,nilipouliza kulikoni sikupata jibu, kuanzia hapo hatuna mawasiliano zaidi ya kuwasiliana kama kuna kitu kimepungua nyumbani nitapewa taaarifa.

Uchumi wangu umeyumba sababu ya hizi vurungu, nimefunga nakuomba hakuna ndoa haitulii kuna wakati nikiona mtu na mke wake wakitembea njiani huku wakipiga stori na kucheka naona nijambo la ajabu nijiuliza inawezekanaje hii?.

Nimejaribu kushirikisha ndugu zake bado hatoi majibu nini ambacho nilimkosea.

Kiukweli nimestuka baada ya watu wawili kuniuliza kwanini nakonda, kwanini sina amani kama zamani?

Mimi ndugu zangu ni bingwa wa kuvumilia matatizo lakini kwa hili nimenyoosha mikono nimeamua niondoke nikaaanze maisha mapya ili nipate amani ya moyo wangu, Mungu ataibarika kazi ya mikono yangu nitainuka tena.
Ukitaka ufaidi maisha ya ndoa wewe jali hii principles" mlioao mjihesabu kama hamjaoa"

Ukifunga Kwa maombi usiombe vibaya wewe muombe Ombi moja Tu Mungu akujalie akili njema baaas

Hesabu ni wako wa karibu unapokuwa naye tu

Utakufa mweenzio ataewa na maisha mapya yataanza
 
Kumbuka kabla ya kumuoa hukuwa peke yako mpiga sound, na hukuwashinnda wapiga sound wengine lkn wewe ulimvuta hisia zake, sasa hisia zake zikibadirika anawakumbuka wale wengine wapiga sound wenzio huenda akaanza kuchakatwa, na wengine

Isipokuwa omba tu apate achakata mwenye huruma na ndoa yako ndiyo ataanza kubadirika na utaiona ndoa yako kana kuwa ndo imeeanza upya , lkn atakuwa na makasiriko makali ya kipindi tu hasa anapotaka kwendea mchakato akirudi fresh Ila kuumwa ,na kuchoka ndo itakuwa siraha yake
 
Mkuu pole Sana,binafsi napenda Sana amani ya moyo kuliko kitu chochote,hivyo kivyovyote fanya ufanyalo kuitafuta amani ya moyo,sasa juu ya swala lako japo sijajua ni ndoa ya Imani gani ,Ila Kama ndo hizi za Hadi kifo kiwatenganishe Basi umekwisha ikiwa utataka kufuata kauli za Hadi kifo kiwatenganishe.

Binafsi nimefunga hizo ndoa Ila kamwe siwezi kuvumilia upuuzi wa namna hiyo,maumivu ya moyo Ni hatari Sana ,Yanaua,amini utakufa ikiwa utaendekeza hiyo Hali,pambana kuitafuta amani ya moyo ,maisha ya duniani ni mafupi Sana yakupasa uyaishi kwa amani na furaha.

Nahili hata mke wangu analijua,nashukuru hatujawahi nuniana zaidi ya Lisaa limoja,na ikiwa yeye ndo atanununa kauli yangu huwa ni moja tu,nenda kwenu kapumzike ,ukipata amani ya moyo ndo urudi.

Ndoa za kununiana ni uchuro mtupu,matokeo yake kuombeana vifo ili mwenza mmoja apate amani,mkuu itafute amani ya moyo kwa gharama yoyote,usiache mtu awaye aondoe furaha ya moyo wako
 
Pole Sana mkuu ila Mimi naona endelea kumuombea maana hajioni yawezekana ni pepo limemvamia
 
Mkuu BAK piga kile kibao cha Lucky dube..Its not easy.
Nitapenda mtoa mada asikilize kwa umakini.
 
We jamaa mwaka jana ulikua hujaoa. Sasa unasema ulioa 2019.

Tunalaumu wanawake bure kumbe we umeleta chai.

  • Kicheko
Reactions: Cyb
Kabla hatujaenedelea hv migegedo inaendelea???[emoji41][emoji41][emoji41]
Hao wanatakaga yale mapenzi ya kwenye movie akikusumbua sana jifanye sharukh khan....jaribu ata kumuimbia,migegedo ya nguvu,mpe muda wako wote unaobaki baada ya kazini[emoji847]
Akiendelea nenda kwa sangoma
[emoji23][emoji23]aende wapi???

Sent from my TECNO KC8 using JamiiForums mobile app
 
[emoji13] yani wewe...! Hako ka wimbo umenikumbusha enzi za ujana wangu.

Mshauri mwenzio sasa [emoji18]
Ha ha! Kwani sahivi umezeeka..?

Ushauri ndo huo wimbo..😂
 
Pole sana bro. I'm around your age japo nimekuzidi miaka kadhaa michache. Nina miaka minne tu kwny ndoa.

Binafsi miezi 6 hadi mwaka wa kwanza ndio kidogo shida ilikuwepo. Nadhani ni ile kuanza kuzoeana kuishi pamoja na kuharmonise tofaui zenu kitabia,mitazamo nk. Hii ni hata kama mlikua mkiishi pamoja kabla ya ndoa bado hutokea. Mfano mimi niliishi nae na tulipata mtoto wa kwanza kabla ya ndoa (sasa tunao wawili) na bado miezi 6 ya kwanza hadi mwaka baada ya ndoa hali ilikua si nzuri.

Kwa nini najiexpose na kusema haya yote? Pengine it may help you with perspective. Pambana kunusuru ndoa yako. It will get better na niamini mimi, mkivuka hapa mtafika mbali sana na your next storm ni pale kwny mid life crisis. Mkivuka hii stage yenu ya sasa mapenzi ndio hua moto moto utakuja kupost thread huku kusimulia unavyo enziwa[emoji23]

Kila la heri. My prayers with you.

PS[emoji41] (out of scope) au aliona hii thread ikapalilia moto?

Positive vibes...huu ushauri unamfaa sana .Mungu ampe amani tu muhusika ili aone ushindi ulioko mbele yake

Sent from my TECNO KC8 using JamiiForums mobile app
 
Mimi ni kijana ambaye tayari nina miaka 30, nilifunga ndoa yangu mwaka 2019. Ndoa yangu imekuwa ya furaha kwa miezi 6 pekee baaada ya hapo mambo yaliharibika na sijui ni kwanini.

Nakumbuka siku moja natoka zangu kazini namkuta wife kajamu, nilipouliza kulikoni sikupata jibu, kuanzia hapo hatuna mawasiliano zaidi ya kuwasiliana kama kuna kitu kimepungua nyumbani nitapewa taaarifa.

Uchumi wangu umeyumba sababu ya hizi vurungu, nimefunga nakuomba hakuna ndoa haitulii kuna wakati nikiona mtu na mke wake wakitembea njiani huku wakipiga stori na kucheka naona nijambo la ajabu nijiuliza inawezekanaje hii?

Nimejaribu kushirikisha ndugu zake bado hatoi majibu nini ambacho nilimkosea. Kiukweli nimestuka baada ya watu wawili kuniuliza kwanini nakonda, kwanini sina amani kama zamani?

Mimi ndugu zangu ni bingwa wa kuvumilia matatizo lakini kwa hili nimenyoosha mikono nimeamua niondoke nikaaanze maisha mapya ili nipate amani ya moyo wangu, Mungu ataibarika kazi ya mikono yangu nitainuka tena.
Mke wako ni kabila gani mkuu?
 
Maaah maeeee...

Mkiambiwa MSIOE Huwa HAMSIKIII.

Tomb* halafu pita hivi uone ni nani atakuumiza.

Mungu awe nawe.

#YNWA
Ila Ww Liverpool mimi nakukubali sana mkuu 😂😂😂😂. Ila nkuambie kitu?? Pamoja na ujanja wako woteeee.. utaingia mahali siku moja kimapenzi.. na utashindwa kutoka. Tena unaweza umizwa kweli kweli. Kumbuka Kila shetani na mbuyu wake mazee 😂😂😂
 
Mimi ni kijana ambaye tayari nina miaka 30, nilifunga ndoa yangu mwaka 2019. Ndoa yangu imekuwa ya furaha kwa miezi 6 pekee baaada ya hapo mambo yaliharibika na sijui ni kwanini.

Nakumbuka siku moja natoka zangu kazini namkuta wife kajamu, nilipouliza kulikoni sikupata jibu, kuanzia hapo hatuna mawasiliano zaidi ya kuwasiliana kama kuna kitu kimepungua nyumbani nitapewa taaarifa.

Uchumi wangu umeyumba sababu ya hizi vurungu, nimefunga nakuomba hakuna ndoa haitulii kuna wakati nikiona mtu na mke wake wakitembea njiani huku wakipiga stori na kucheka naona nijambo la ajabu nijiuliza inawezekanaje hii?

Nimejaribu kushirikisha ndugu zake bado hatoi majibu nini ambacho nilimkosea. Kiukweli nimestuka baada ya watu wawili kuniuliza kwanini nakonda, kwanini sina amani kama zamani?

Mimi ndugu zangu ni bingwa wa kuvumilia matatizo lakini kwa hili nimenyoosha mikono nimeamua niondoke nikaaanze maisha mapya ili nipate amani ya moyo wangu, Mungu ataibarika kazi ya mikono yangu nitainuka tena.
Mdogo wangu,kimbia!hatuoi Ili tuwape furaha wenzi wetu,tunaoa Ili mahitaji yetu yatimie,kama mahitaji yetu hayapo,suruhisho ni kuondoka,
Hukuumbwa umpe mtu furaha,furaha yako ni jukumu lako peke yako,ur responsible for ur own happiness,
Huyo si mwanamke pekee,kama kumuacha unaona ugumu,ondoka hata kwa muda,
Kwanza iambie akili yako kwamba sio lazima huyo bibie akupende,akuheshimu,
 
Back
Top Bottom