Poleni na majukumu watu wa humu, niende moja kwa moja kwenye mada,
Tulikuwa watu zaidi ya watatu, tulikuwa kwenye eneo Kama mbuga hivi ambalo ni nyasi kwa wingi, Sasa ilikuwa ni Kama unachagua pa kukanyaga maana Kila baada ya hatua tatu ni nyoka wakubwa kwa wadogo,
Ikatokea nyoka mmoja mkubwa akanirukia na kuning'ata kisogoni, basi nukawa napiga kelele lakini mwenzangu akachuma majani ya mchunga chapu na kuanza kunipaka nilipong'atwa huku akiniambia ni dawa na nitapona tu nisijali,
Sasa wakati nasubiria kupona ndo nikashtuka kutoka usingizini,
Je hii ndoto Ina maana gani wakuu.
Kwanza Kabisa Mkuu Pole Na hongera!
Pole kwa Kuwa Una maadui wengi sana Ambayo wamekuzunguka kila Mahali na Wanakuvizia Ufanye Kosa Dogo ili wakupoteze!..
Hongera kwa Sababu una Backup Ya Marafiki na Ndugu ambao wanakulinda na hao maadui bila wewe Kujua!..
Tafsiri Ya ndoto yako ni kwamba:-
Mbuga Ndotoni humaanisha Mapito yako Ya kimaisha Ukiona Mbuga ni kijani sana Inamaanisha mapito yako ni ya Neema na Amani..
Ukiona Majani yamenyauka na Kipindi ni cha Kiangazi humaanisha Kuna Ups and Down nyingi sana kwenye Mapito yako...
Kisogo humaanisha ni wakati wa Nyuma au Ni kutoka nyuma..So kama Nyuka Amekung'ata Kisogo inamaanisha Uadui wa Huyo ni wa Muda mrefu na sio mpya ni uadui wa Huko Nyuma..
Nyoka wakubwa humaanisha Uadui mkubwa na wadogo humaanisha Uadui Mdogo wa Kusengenya tu na Kukushushia hadhi yako..
Kung'atwa humaanisha kuugua kwa Kimazingara au kupata Uadui huo ambao kwenye Dunia ya Kawaida ni kama Ugonjwa au Mabaya ambayo huyaelewe..Pia inamaanisha Utapoteza Biashara zako au Vitu vyako au baadhi ya mambo au Kupata Hasara kutoka kwa Uadui..
Na nyoka wadogo huweza kumaanisha kwamba unawapenda sana watu na unaishi nao kwa Upe do na Kuwachukulia kama marafiki wakati watu hao ndo ukudharirisha kwa siri na kukusengenya kwa watu na wanapanga njama za kukuangamiza kwa siri
Baada ya kuchambua baadhi ya vitu Sasa ndoto yako inamaanisha nini?
Unapita katika changamoto za Kimaisha na kwa bahati mbaya Unawatu unaowachukulia kuwa ni marafiki Wanajiunga Kwa siri Kukusengenya wewe na kukutengenezea Uadui licha ya wewe kuwachukulia Marafiki wazuri na kuwapenda...
Na hiyo ndo ilitoa chances ya Uadui mkubwa kukupata na ukapata Hasara kubwa kwenye Maisha hako..
Good enough ni kwamba Bado una Ndugu na marafiki wanaokupenda kwahyo watapambana/Wanapambana na wewe ili urudi katika hali yako..
Kwahyo Kutokana na Hao marafiki wanaokupenda Unaweza usione madhara yanayokupata/Au ukaona madhara madogo..
Ila Wao ndo wamepambana sana kuhakikisha Wewe uwe salama na uzuri watakuambia walivyofanya /Watakavyofanya