Nimenuniwa kisa nimejiita Bachela mbele yake!!!!

Nimenuniwa kisa nimejiita Bachela mbele yake!!!!

Shark

JF-Expert Member
Joined
Jan 25, 2010
Posts
29,775
Reaction score
29,746
Wadau, ukiacha maswala ya kuajiriwa mimi pia ni mwanafunzi wa chuo hivyo hua nabebaga madaftari, vitabu, past papers, notisi na makaratasi mengine kibao tu siti ya nyuma kwenye gari. Last time nikiwa na galfriend wangu ambae hatuishi pamoja ilitokea tukampa mdada mmoja hivi ambae nafahamiana nae lift ambae alishangaa kukuta gari limejaa mavitabu ndani. Nlichomjibu ni kua ubachela ndio unaonisumbua ndio maana gari halijapangwa. Eti mwenzenu nimenuniwa toka hiyo jumatatu mpaka leo. Nachoomba mnisaidie neno bachela linagumika pia kwa mtu mwenye mchumba??? Maana hui mnuno as safari hii too much!!!
 
ulitaka aimbe 'haleluya'?
Unamdharau ndo maana ulijiita bachala mbele yake.

Au kuna kitu huyo rafiki yako uliyempa lift unataka kumwambia.
 
Ni uelewa wake tu huyo gf wako. Wewe bado ni bachelor, kwani hujaoa bado. Uchumba/gf haimaanishi kwamba sasa ameshakuwa mke/mume. Ni mpaka pale mtakapoamua kuoana rasmi. Uchumba/gf huweza kuvunjika muda wowote. Mimi naamini ulikuwa sahihi na yeye gf/mchumba anapaswa kuelewa hivyo. Kama anaona si vema wewe kujiita bachelor kisa una gf/mchumba, then afanye utaratibu ili muoane. Jaribu kumwelewesha ili aelewe.
 
ulitaka aimbe 'haleluya'?
Unamdharau ndo maana ulijiita bachala mbele yake.

Au kuna kitu huyo rafiki yako uliyempa lift unataka kumwambia.
Sijamuoa bado, na wala sikai nae. Ili kuepuka usumbufu wa kutafuta daftari asubuhi nimeamua kuyachukua yote nikayabwaga siti ya nyuma. Ye mwenyewe kajistukia tu
 
Ulikua unatangaza biashara?
Maana kauli yako naweza nikaitafsiri hivi "sina mtu ndio maana, unataka kunisaidia??!"

Ulishindwa nini kusema shughuli nyingi? Maana hata nikifikiria sioni mahusiano ya ubachela na vitabu vingi kwenye gari. Unless unategemea siku ukiwa na mke awe anakupelekesha kama mtoto kwamba uvitoe au awe anatoa yeye.
 
Mimi naamini ulikuwa sahihi na yeye gf/mchumba anapaswa kuelewa hivyo. Kama anaona si vema wewe kujiita bachelor kisa una gf/mchumba, then afanye utaratibu ili muoane. Jaribu kumwelewesha ili aelewe.

Mkuu, mtu mwenyewe haelewesheki, yaani hakuna kabisa mawasiliano kwa sasa. Nikimpigia hapokei, wala hajibu sms. Jana nimekwenda kwake kuanzia saa mbili usiku namsubiri nje kwake mpaka saa tano naomdoka hakutoka.
 
We nawe umekosea, hata mm ningenuna, ulivosema ivo as if ua single and ua lukin 4 sm one to tk cre, haikuwa poua
 
Mkuu, hajakununia kwa Kujiita Bachelor, kakununia kwa Kumuonesha mbele ya huyo Bint Mwingine kuwa hawezi ku take care thats why Gari lako liko shaghalabaghalah, Ki msingi umemuabisha sana na Mbaya zaid,mbele ya Mwanamke mwenzake ambaye wewe na sio yeye unafahamiana nae, Jiulize ulishawahi kununiwa nae Before, if yes, what was the reason, if No Mtoe out one day, Mtafute huyo uliyrmpa lift, kaeni mahali, katika Mazungumzo yenu jikite zaid kumsifia Demu wako bila yeye kujua kuwa una Neutrilize mambo, usiku nenda nae kalale nae home (Kama sio mtoto wa Mama/ Geti) Mpe Mikasi ya Haja, i assure you kesho mambo swafi....
 
Ulikua unatangaza biashara?
Maana kauli yako naweza nikaitafsiri hivi "sina mtu ndio maana, unataka kunisaidia??!"
Ulishindwa nini kusema shughuli nyingi? Maana hata nikifikiria sioni mahusiano ya ubachela na vitabu vingi kwenye gari. Unless unategemea siku ukiwa na mke awe anakupelekesha kama mtoto kwamba uvitoe au awe anatoa yeye.
Lizzy, kuna tofauti kubwa sana kuishi na mke ndani na kuishi bila yeye. Angalau mke angeweza kuvipanga vizuri, au hata ashauri nivitafutie begi kubwa. Lakini pia labda swala ni kwamba mimi ni Bachela tu, so sikua na kosa kusema vile
 
Hakuna haja ya kusugar coat maneno: wewe ni bachelor, period.

Five star rated this one. Kuna na GF hakukufanyi mwanaume usiwe bachelor, ingekuwa mtoa maada kaoa halafu ajiite bachelor hicho kizaa zaa kingekuwa halali kabisa!
 
Mkuu, hajakununia kwa Kujiita Bachelor, kakununia kwa Kumuonesha mbele ya huyo Bint Mwingine kuwa hawezi ku take care thats why Gari lako liko shaghalabaghalah, Ki msingi umemuabisha sana na Mbaya zaid,mbele ya Mwanamke mwenzake ambaye wewe na sio yeye unafahamiana nae, Jiulize ulishawahi kununiwa nae Before, if yes, what was the reason, if No Mtoe out one day, Mtafute huyo uliyrmpa lift, kaeni mahali, katika Mazungumzo yenu jikite zaid kumsifia Demu wako bila yeye kujua kuwa una Neutrilize mambo, usiku nenda nae kalale nae home (Kama sio mtoto wa Mama/ Geti) Mpe Mikasi ya Haja, i assure you kesho mambo swafi....
Story nzima ilianza hivi,
Baada ya kutoka Job nlimpitia Galfr ili anisindikize chuo nichukue some materials nimpeleke yeye kwanza ndio nirudi kwangu.
Baada ya kumchukua yeye Posta, nkamuona mdada mmoja ambae tunakaa nae mtaa mmoja akisubiri daladala kituoni hivyo nikaona si vyema nikimuacha so nikamchukua. Wakati anaingia siti ya nyuma ndio msala ulipoanza.
Yule mgeni alipouliza mbona wifi yake asipange mimi nlijitahidi sana kumtetea kua sikai nae hivyo hana kosa kabisa,
Cha ajabu Galfr akadai nimshushe Namanga kuna kitu anachukua na hangependa kunikwaza kwa kunichelewesha kumsubiri,
Ndio mpaka leo nnimenuniwa.
Jana nafika kwao namuona kabisa ndani akipita pita but hakutoka kamwe!!!
 
anakuwa mjinga ashukuru Mungu amekuta huo ndio ukweli kutoka moyoni mwako na hata kale kandafu ulikalazimsha tu kukila
kuandika jina la Mume na mke duniani .m ningemshukuru Mungu na kujipanga kimya kimya siku natangaza na mi bachela loh
 
Five star rated this one. Kuna na GF hakukufanyi mwanaume usiwe bachelor, ingekuwa mtoa maada kaoa halafu ajiite bachelor hicho kizaa zaa kingekuwa halali kabisa!

Exactly, umeona eee mkuu? Girlfriend sio mke. Marital status ya mshkaji kwenye form shuleni na kazini itasomeka kama yupo single. Sidhani kama atajaza married ili tu kumfurahisha girlfriend wake.
 
Omba radhi yaishe mkuu.
Na siku nyingine shirikisha ubongo kabla hujasema chochote.
OTIS
 
Halafu msichana unayemtangazia kuwa bado uko bachela mnaishi naye mtaa mmoja?? Halafu anakuja kuhoji usafi wa gari lako?? Huyo msichana hana adabu na ana kimbele mbele!!

Umemdhalilisha sana GF wako na itakuwa bahati sana kama atakusamehe...

Kama vipi omba msaada kabla hujafutwa kwenye kitabu chake cha kumbu kumbu!!
 
Omba radhi yaishe mkuu.
Na siku nyingine shirikisha ubongo kabla hujasema chochote.
OTIS

Unastahili kabisa kununiwa

Halafu msichana unayemtangazia kuwa bado uko bachela mnaishi naye mtaa mmoja?? Halafu anakuja kuhoji usafi wa gari lako?? Huyo msichana hana adabu na ana kimbele mbele!!

Umemdhalilisha sana GF wako na itakuwa bahati sana kama atakusamehe...

Kama vipi omba msaada kabla hujafutwa kwenye kitabu chake cha kumbu kumbu!!
Asanteni kwa busara zenu. . . embu muelewesheni huyo kijana akili imchemke.
 
To us men it might seem a normal statement but not for women..they are distinctive creatures who take even small matters seriously....just go n apologize to her
 
Anastahili kununa, kwanza umeonyesha kwamba hawajibiki, pili kujiita bahelor unamaanisha unapatikana yaani huna m2.

Ukiwa na hawa wenzetu unatakiwa kuwa makini katika maongezi mara nyingi wanatumia hisia. Mwombe radhi yaishe.
 
Back
Top Bottom