Shark
JF-Expert Member
- Jan 25, 2010
- 29,775
- 29,746
Wadau, ukiacha maswala ya kuajiriwa mimi pia ni mwanafunzi wa chuo hivyo hua nabebaga madaftari, vitabu, past papers, notisi na makaratasi mengine kibao tu siti ya nyuma kwenye gari. Last time nikiwa na galfriend wangu ambae hatuishi pamoja ilitokea tukampa mdada mmoja hivi ambae nafahamiana nae lift ambae alishangaa kukuta gari limejaa mavitabu ndani. Nlichomjibu ni kua ubachela ndio unaonisumbua ndio maana gari halijapangwa. Eti mwenzenu nimenuniwa toka hiyo jumatatu mpaka leo. Nachoomba mnisaidie neno bachela linagumika pia kwa mtu mwenye mchumba??? Maana hui mnuno as safari hii too much!!!