Nimenunua Umeme muda huu, gharama zimepanda kimya kimya kutoka Tsh 125/unit hadi Tsh 312/ unit kwa mita za kawaida (majumbani)

Nimenunua Umeme muda huu, gharama zimepanda kimya kimya kutoka Tsh 125/unit hadi Tsh 312/ unit kwa mita za kawaida (majumbani)

Mita uliyofungiwa wewe ni 3 phase( ya biashara) kwa watu wa majumbani ni Singe phase ambapo unit 1 tunauziwa 125.
Majority mtaani tunatumia huu wa 3 phase.

Single phase huwa mko wachache.

Kama ni hivyo, basi nawe utakuwa umeungwa kwenye 3 phase.
 
Mita uliyofungiwa wewe ni 3 phase( ya biashara) kwa watu wa majumbani ni Singe phase ambapo unit 1 tunauziwa 125.
HApana, hakuna cha 3 phase, tunatumia single phase Ila 10k ni unit 28 (kama kukiwa hakuna makato ya jengo)

Kwa huku dar es salaam watu wschache ndo wanapata unit nyingi kwa bei hiyo

Ukifika tanescomajibu ni kwamba hufuma hiyo imeondolewa maeneo ya miji,


Uhakika wa dhati wanaujua tanesco, maana kuna wengine bado wanatumia, wengine tunakataliwa huduma na unapewa jibu imekatazwa mwaka fulani, lakini kabla ya huo mwaka waosema ndo huduma imekatazwa tulikataliwa huduma vilevile
 
Mbona hawajafyeka kodi ya jengo?😁 Hudaiwi au mifumo haisomani na TRA!!
Siioni Debit collected??
 
Wameisha wajua mtapiga domo kidogo alafu mtaacha na hali itaendelea kama watakavyo wao.
 
Safi sana, mama anaupiga mwingi.
Octoba tunatiki.

Kwanini wasipandishe iwe 2000 per unit, mimi naona 392 ni ndogo sana, maana hii nchi uzezeta umezidi
 
Mkuu wewe utakuwa ulikuwa TARIFF ZERO kutokana na matumizi yako madogo hili swali watu tunaofuatilia tulishauliza Kitambo sana....; By the way wenzako wa mijini ni kitambo sana walikuwa wanalipia hio Gharama waliobakia na gharama ndogo ni vijijini; Tunaambiwa umeme umeongezea yet wanapandisha gharama...

 
Next time jitahidi hata kuficha namba muhimu za taarifa ya huo muamala ili kujilinda, ili next time ukijichanganya usiishie kudakwa kama panzi

Kwani hujui kwa huu muamala tu unaweza kudakwa na ikajulikana unaishi wapi?? Siri sio namba yako ya simu tu, kupitia huu muamala naweza kupata vyote mpaka namba ya nyumba iliyowekwa. Take your time!!
 
Hii taarifa umeleta ni nzuri ila umefanya kosa moja la kimkakati , hujaficha taarifa zako binafsi.

Hao vibaka wa TANESCO wanashirikiana na watekaji kwa nyakati kadhaa kupitia tracing ya nambari za meter na simu husika iliyonunua huo umeme na hata juzi Hilda Newton katoa tahadhari na mifano kadhaa kuhusu hayo mambo, mnaishi katika serikali isiyotaka kukosolewa hivyo inatumia kila mbinu kuziba mdomo ukiwakosoa.

Mwaka 2019 yule mkosoaji wa serikali kule Twitter aliyekuwa anaitwa Mcomoro alipotezwa hivi hivi baada ya kutoa details zake alipopata changamoto ya umeme ndio Cyprian Musiba na genge lake wakafanya tracking kisha wakampoteza.

Be informed


View: https://x.com/HildaNewton21/status/1966466299455852845?t=eEPq-iiSo2vx1Jhcb-_FMw&s=19
 
Umeme umepanda ghafla na bila taarifa kwa zaidi ya asilimia 150%, na hii imefanywa kimya kimya! Kama kipindi kile walivyoongeza 500 kwenye tozo ya jengo bila taarifa, baada ya kelele wakaiondoa,

Umeme wa 1000 wa matumizi ya kawaida nilikuwa nikipata unit 8.1 sawa na sh 125 kwa unit, leo umeme wa 1500 unapewa unit 4.8?! SAWA NA 312 KWA UNIT...!

wanajua hakuna mahala pengine pa kuwakamua wananchi zaidi ya kupitia ununuzi wa umeme...ndio njia rahisi ya wao kujipatia fedha kwa mwananchi bila usumbufu!

TUENDAKO HALI NI MBAYA ZAIDI! Tusipochukua hatua SASA!

TANESCO tunahitaji ufafanuzi!

View attachment 3480704
Hapo ni September na November mambo ni mapya kazi kwel kweli
 
Tuache kelele Oct tukatiki ***** zao wale watu wa kijani
inasikitisha...
Na hao watu wa kijani wakiwa pamoja wanatucheka wana sema k**** zao hizi nyumbu za tz ni kuzikamua tu.
 
Back
Top Bottom