Nimenusurika kutapeliwa siku ya leo

Nimenusurika kutapeliwa siku ya leo

Naendelea....

Wakati yule dada anaongea na yule jamaa mimi nilikumbuka kitambaa changu nilichotumia kufunga ule mzigo na kuanza kukifungua, Kitendo nimemaliza kufungua kile kitambaa na yule dada akawa amamemaliza kuongea na jamaa na akanipa simu yangu nami nikaiweka sikioni kumaikiliza jamaa hatma yake ni nini.

Jamaa: Sasa dada kasema mzigo upo sawa, sasa naomba acha huo mzigo hapo kisha njoo hapa hospital utanikuta nije nikupe hela yako.

Mimi: Sawa mkuu (Nikamuaga yule dada, Nikauacha ule mzigo ukiwa haujafungwa upande mmoja na kuanza Safari ya haraka kuelekea pale hospital aliponielekeza jamaa)

Kufika pale hospital jamaa akaniambia niingie nimsubiri pale reception anakuja.

Kweli nimesubiri kama dk tano ila machale yakanicheza na nikajiuliza ni kwanini hii order ya jamaa imekuwa na changamoto sana, Na imekuwaje mzigo nimeacha kwa madada ambae simjui na hadi muda huu sijalipwa hata advance? Ndipo akili ikaniambia "Wewe ebu toka hapo reception kimbia upesi rudi kwa yule dada kaweke uhakika wa mzigo usiondoke bila wewe kutoa permit" Sikujiuliza mara mbili ghafla mapigo ya moyo yakaanza kwenda mbio nami nikaamka chap na kuanza kukimbia kuelekea kwenye ile frame niliyoacha mzigo (huku naona simu ya jamaa inaita ila sikutaka kuipokea na nisijue ni kwanini niliipuuza). Ndipo natokea barabarani hivi kwa mbali naona kuna bodaboda anafika na abiria alafu abiria yule akashuka haihai kuingia pale na mimi huku speed nikiongeza na sasa nikaanza kukaribia ile frame ndipo nikashuudia yule abiria amerudi kwenye bodaboda alaiyokuja nayo kwa upesi sana na boda akawasha chuma wakaondoka. Ila kwa mimi ile action ilinipa wasiwasi kwamba hawa vipi mbona wako fasta sana na kama ni kuchukua mzigo wangu mbona wameondoka mikono mitupu? Sikujiuliza sana nikajikongoja na kuingia kwenye ile frame niliyoacha mzigo wangu, Nikamkuta yule dada yupo normal tu... Kuchungulia nilipoacha mzigo nikauona ndipo nikapumua kidogo kwa afadhali na nikamuuliza yule dada.

Mimi: Nimerudi maana nimehisi kama kuna kamchezo hapa (kabla sijaendelea yule dada akanikatisha)

Dada: Ehee, umeona hao uliopishana nao na bodaboda?

Mimi: Ndiyo, niliwaona ila nilikuwa kwa mbali kidogo ila niliona kama wapo fasta sana ila sikuwajali maana na mimi nilikuwa na mawazo pengine kwa muda niliopoteza reception pale labda huku nazungukwa.

Dada; Yaani ni kweli kaka yangu, hawa wtu ndo walikuwa wamejia huu mzigo, Mara ya kwanza alikuja mmoja ambae ndo yule tuliekuwa tumewasiliana nae akaniambia ameshamalizana na wewe na akautoa mzigo nje akitaka kuondoka nao ila kutokana na itilafu ya ile kamba akashindwa kuubeba ndipo akaaga kwenda kuita bodaboda, Wakati amendoka mimi pia machale yakanicheza nikaurudisha huu mzigo ndani maana alikuwa kauweka pale nje barazani na ndipo baada ya muda ndo wakaja wawili kama ulivyowaona, Ila awamu hii ikabidi nimchallenge kwamba ngoja nikupigie wewe ulieniachia kwanza kama wameshakupa hela sasa wakati ndo tunabishana ndo yule mwenzake amabae ni bodaboda akawa anamuita kama anamshtua kwamba waondoke ndo wakatoka kwa haraka hata nisielewe shida ni nini.

(kwanza nikapumua kama sekunde 50 nisimjibu kitu yule dada ndipo nikamjibu)
Mimi: Dada hao wamekimbia kwa kuwa yule wa nje aliniona ninavyokuja kwa kasi pengine alihisi nimewashtukia ila sio kesi dada asante sana kwa kuwawekea kikwazo kidogo na pia kingine ile kamba kukatika imekuwa msaada mwingine.

Yule dada alinipa pole sana ila kwa muda huo mimi nilikuwa tu nikiumia ni kwanini wanadanu tumekuwa na roho za kikatili kiasi hiki, Imagine watu wazima kabisa wanaunda timu kuja kutaka kuniumiza mimi mtoto wa kimaskini ninaejitafuta kweli? sh.500,000 mimi si ningekonda kwa mawazo nifie gheto wakuu? Ni hela ambayo nikiwatumia wazazi wangu wananibariki hadi nshangaa asee ila watu hata hawajali.

Basi niliishia tu kumshukuru Mungu wangu ambae nimekuwa nikimuomba kila wakati na haniachi, Na pia baada ya lile tukio wala sijahangaika kumcheki tena yule jamaa kwa kumuonesha nimechukia au nimemdharau bali sinimeamua tu kuupack ule mzigo na kuurudisha store.

Jamaa amenipa loss ya 15k kwaajili ya usafiri pamoja na muda wangu na pia nimenyeshewa sana na mvua ila ni heri kuliko ningepata loss ya vyote.

Mwisho: Wewe ukijaribu kunitapeli kama upo humu au kama utauona huu uzi ama hakika Mimi nimekusame ila nimekuachia Mungu adeal na wewe.

Ambao mnakubali nini nafanya naombeni muendelee ku-support biashara yangu.
Ahsanteni sana kwa kuusoma uzi wangu hadi mwisho kama kuna some corrections za spelling and stuff like mnivumilie tu 🤝
usifanye biashara kizamani
 
Mimi humu kuja jamaa alitaka kunitapeli iphone ya mchongo akaniita bar nikawakuta yeye na wenzie wanakunywa wanakanikaribisha wakanipa simu niangalie, nilivyoona ya mchongo nikamute kwanza nikawaambia tupige vyombo kidogo halafu twende atm tukatoe hela, piga maja piga maji nilivyoona zinatosha me huyo nikawaaga kuwa naenda toielt, jumlaaaa!
 
Huu mchezo nilichezewa hivyo hivyo pale Hospitali ya Bochi teba bidhaa ilikuwa laptop
Ila nilishtuka mapema
 
Naendelea....

Wakati yule dada anaongea na yule jamaa mimi nilikumbuka kitambaa changu nilichotumia kufunga ule mzigo na kuanza kukifungua, Kitendo nimemaliza kufungua kile kitambaa na yule dada akawa amamemaliza kuongea na jamaa na akanipa simu yangu nami nikaiweka sikioni kumaikiliza jamaa hatma yake ni nini.

Jamaa: Sasa dada kasema mzigo upo sawa, sasa naomba acha huo mzigo hapo kisha njoo hapa hospital utanikuta nije nikupe hela yako.

Mimi: Sawa mkuu (Nikamuaga yule dada, Nikauacha ule mzigo ukiwa haujafungwa upande mmoja na kuanza Safari ya haraka kuelekea pale hospital aliponielekeza jamaa)

Kufika pale hospital jamaa akaniambia niingie nimsubiri pale reception anakuja.

Kweli nimesubiri kama dk tano ila machale yakanicheza na nikajiuliza ni kwanini hii order ya jamaa imekuwa na changamoto sana, Na imekuwaje mzigo nimeacha kwa madada ambae simjui na hadi muda huu sijalipwa hata advance? Ndipo akili ikaniambia "Wewe ebu toka hapo reception kimbia upesi rudi kwa yule dada kaweke uhakika wa mzigo usiondoke bila wewe kutoa permit" Sikujiuliza mara mbili ghafla mapigo ya moyo yakaanza kwenda mbio nami nikaamka chap na kuanza kukimbia kuelekea kwenye ile frame niliyoacha mzigo (huku naona simu ya jamaa inaita ila sikutaka kuipokea na nisijue ni kwanini niliipuuza). Ndipo natokea barabarani hivi kwa mbali naona kuna bodaboda anafika na abiria alafu abiria yule akashuka haihai kuingia pale na mimi huku speed nikiongeza na sasa nikaanza kukaribia ile frame ndipo nikashuudia yule abiria amerudi kwenye bodaboda alaiyokuja nayo kwa upesi sana na boda akawasha chuma wakaondoka. Ila kwa mimi ile action ilinipa wasiwasi kwamba hawa vipi mbona wako fasta sana na kama ni kuchukua mzigo wangu mbona wameondoka mikono mitupu? Sikujiuliza sana nikajikongoja na kuingia kwenye ile frame niliyoacha mzigo wangu, Nikamkuta yule dada yupo normal tu... Kuchungulia nilipoacha mzigo nikauona ndipo nikapumua kidogo kwa afadhali na nikamuuliza yule dada.

Mimi: Nimerudi maana nimehisi kama kuna kamchezo hapa (kabla sijaendelea yule dada akanikatisha)

Dada: Ehee, umeona hao uliopishana nao na bodaboda?

Mimi: Ndiyo, niliwaona ila nilikuwa kwa mbali kidogo ila niliona kama wapo fasta sana ila sikuwajali maana na mimi nilikuwa na mawazo pengine kwa muda niliopoteza reception pale labda huku nazungukwa.

Dada; Yaani ni kweli kaka yangu, hawa wtu ndo walikuwa wamejia huu mzigo, Mara ya kwanza alikuja mmoja ambae ndo yule tuliekuwa tumewasiliana nae akaniambia ameshamalizana na wewe na akautoa mzigo nje akitaka kuondoka nao ila kutokana na itilafu ya ile kamba akashindwa kuubeba ndipo akaaga kwenda kuita bodaboda, Wakati amendoka mimi pia machale yakanicheza nikaurudisha huu mzigo ndani maana alikuwa kauweka pale nje barazani na ndipo baada ya muda ndo wakaja wawili kama ulivyowaona, Ila awamu hii ikabidi nimchallenge kwamba ngoja nikupigie wewe ulieniachia kwanza kama wameshakupa hela sasa wakati ndo tunabishana ndo yule mwenzake amabae ni bodaboda akawa anamuita kama anamshtua kwamba waondoke ndo wakatoka kwa haraka hata nisielewe shida ni nini.

(kwanza nikapumua kama sekunde 50 nisimjibu kitu yule dada ndipo nikamjibu)
Mimi: Dada hao wamekimbia kwa kuwa yule wa nje aliniona ninavyokuja kwa kasi pengine alihisi nimewashtukia ila sio kesi dada asante sana kwa kuwawekea kikwazo kidogo na pia kingine ile kamba kukatika imekuwa msaada mwingine.

Yule dada alinipa pole sana ila kwa muda huo mimi nilikuwa tu nikiumia ni kwanini wanadanu tumekuwa na roho za kikatili kiasi hiki, Imagine watu wazima kabisa wanaunda timu kuja kutaka kuniumiza mimi mtoto wa kimaskini ninaejitafuta kweli? sh.500,000 mimi si ningekonda kwa mawazo nifie gheto wakuu? Ni hela ambayo nikiwatumia wazazi wangu wananibariki hadi nshangaa asee ila watu hata hawajali.

Basi niliishia tu kumshukuru Mungu wangu ambae nimekuwa nikimuomba kila wakati na haniachi, Na pia baada ya lile tukio wala sijahangaika kumcheki tena yule jamaa kwa kumuonesha nimechukia au nimemdharau bali sinimeamua tu kuupack ule mzigo na kuurudisha store.

Jamaa amenipa loss ya 15k kwaajili ya usafiri pamoja na muda wangu na pia nimenyeshewa sana na mvua ila ni heri kuliko ningepata loss ya vyote.

Mwisho: Wewe ukijaribu kunitapeli kama upo humu au kama utauona huu uzi ama hakika Mimi nimekusame ila nimekuachia Mungu adeal na wewe.

Ambao mnakubali nini nafanya naombeni muendelee ku-support biashara yangu.
Ahsanteni sana kwa kuusoma uzi wangu hadi mwisho kama kuna some corrections za spelling and stuff like mnivumilie tu 🤝
Mungu ni mwema .....naamini ataendelea kutengeneza njia pasipo njia katika biashara YAKO.
 
Back
Top Bottom