Nimenyoosha mikono juu

Nimenyoosha mikono juu

Baada ya kupitia misukosuko mingi kwenye ndoa yangu nimeamua kuja kupumzika nyumbani. Moyo unauma sana mpaka sitamani hata kuinuka kitandani natamani kulala tu, nikilala usiku nikisikia adhana ya saa 11 asubuh moyo unauma nataman kuwe usiku tu tulale tusiamke. Sina namna siwezi kumlazimisha anipende, hanipendi, haoni umuhimu wangu wala hisia na mimi hana.

Kinachoniuma zaidi vitu yangu vyote nimeiacha,, nyumba yangu, biashara yangu nimerudi O ninamtoto mdogo
Sijajua kwa ambao wameshapitia hili walifanyaje wakasahau machungu maisha yakaendelea.
Pole Sana, Ukweli unayopitia sasa ndo yanaenda kukukomaza zaidi. Yakishapita haya na ukafanikiwa kuyasahau hakuna kiumbe dunia hii atakayekusumbua.

Tatizo umeacha zaidi hisia zikutawale kuliko akili. Unapofikia situation Kama Hii yakupasa utumie akili zaidi kuliko hisia.

Kaa chini ujiulize, utaaishi hivyo Hadi lini? Yaani ukose Raha na maisha yakuharibikie kisa ushamba wa mpuuzi mmoja tu? Dunia hii yenye watu zaidi ya bilioni moja lakini umekubali maisha yako yaharibiwe n uyo mshamba mmoja? Ambaye umempa muda wako,upendo wako kila kitu chako lakini hakupendi?

Dada yangu Mungu Bado ana makusudi mengi na ww, Na unayopitia sasa ni hatua muhimu zaidi ambayo ni lazima upitie ili uje kuwa Bora zaidi.

Narudia Acha kufanya maamuzi kwa kuongozwa na hisia, Tumia akili. Be Really, hakuna mtu aliyekuchagulia uishi maisha hayo. Ni matokeo ya maamuzi yako. Lazima ukubali ulikosea kuwa na mtu Kama huyo. Kubali kwamba hakupendi. Ruhusu Moyo ukubali ukweli huu. Amani huanza kuja kwa kukubali ukweli. Baada ya Hapo Anza jitihada za kumove on.

Achana na mazoea sijui nilimpenda, sitoweza hapana. Unaweza shida ni kujiendekeza. Vipi uyo mpuuzi Kama angekuwa amefariki? Ina maana ungeshindwa kuendelea na maisha? Mtu mmekutana ukubwani from nowhere ndo Leo akukoseshe Kula kweli? Are you serious? Ana nini cha maana kutuzidi wanaume wengine?

Just Be Really, Take Care huo Muda unaopoteza kumlilia kichaa asiye na shukran kamwe hauwezi kurudi. Suluhisho si ww kukaa ndani. Njia zuri ni ww kuwa busy. Ubusy pekee ndo utakusahaulisha na uyo kiumbe limbukeni.

Pole na hili litapita hatimaye utakaa sawa. Ikiwa Mungu ni wetu site basi hata hili jaribu utalishinda.
 
Pole sana mpenzi, Ila nikwambie dawa ya mwanaume ni mwanaume mwenzie, Kama ilivyo dawa ya mwanamke ni mwanamke mwenzie....upo? Umesema mtoto ana mwaka mmoja, hebu Acha kulea kizamani, oga utakate, jipende, pendeza.....Acha kumuwaza huyo mwanaume halafu utaleta mrejesho hapa.
 
"ugonjwa ukiwa unaanza ni ngumu Sana kuugundua lakini ni rahisi kuutibu,,, ugonjwa ukikomaa ni rahisi Sana kuugundua lakini ni ngumu kuutibu".

Pole Sana, nimesoma nyuzi zako nyingii, nimeona jins gani ugonjwa ulivyokuwa unaanza lkn ulikosa kuutibu mapema Kwa kigezo Cha nitambadilisha kwenye ndoa, au nitambadilisha awe nitakavyo. Huo msemo huwa unawagharimu watu wengi sana,
1) nitambadilisha
2) uvumilivu
Hakunaga kitu kinaitwa nitambadilisha au acha nivumilie kwenye mapenzi. Ugonjwa ulishauona tangu kbl hajakuoa lkn ulishupaza shingo kwasbb ulitamani ndoa , ulitamani kuolewa, upweke ulikuchosha. Lakini ss ugonjwa umekomaa na matibabu yamekuwa ni yenye maumivu mazito ndani ya moyo...

Ni kweli mapenzi ni muhimu ktk maisha yetu, na Kila mwanadamu anahitaji upendo kutoka kwa mwenzi wake. Simama acha kulia, jali mambo yako kuanzia Sasa, Rudi nyumbn kwako, usiache nyumba yako, bihashara zako, Mali zako kwasbb ya mtu 1. Najua ni ngumu lkn jitahidi, pambana Kwa ajili ya wtt wako. Usimuulize chochote ata awe amerudi saa 2 asubuhi, ikiwezekana gawaneni na vyumba kbs, Kila mtu alale kwake, fungua bihashara yako, endelea kupambana. Aache pesa ya kula asiache, usimuulize, na chakula usimuachie. Pika kula na wtt wako. Mandhari hakupigi Wala hakuvunji Taya, pambana Kwa ajili ya wtt wako. Mwanamke pambana, acha kulia Lia. Na ukiona hiyo njia huwezi, nenda kapange, endelea na maisha yako, usimfikirie yeye na hapo ujue tu hakuna mwanaume.

Ila hatushangai siku ukija hapa na kusema umerudiana nae. Maana mwalimu wetu ni kipofu. Na mapenzi hayanaga ushauri, sema tumejipendekeza tu hapa, mn ndiyo hulka ya binadamu ilivyo.
 
Kama umeondoka na mtoto wako inatosha.

Mali utapata.

Angalia usiingie tena kwenye mahusiano, hakuna wa kukupa faraja zaidi yako wewe mwenyewe.

Anzia hapo
 
Mkuu mi nnaomba nikusaidie kupita ktk hali hii, nitakupa faraja sio mapenzi lkn maana sitaki kujiingiza ktk mahusiano na mtu kwa sasa ila i will help you, karibu inbox tuyajenge, unachotakiwa wewe ni counseling tu sio kingine
 
Mkuu mi nnaomba nikusaidie kupita ktk hali hii, nitakupa faraja sio mapenzi lkn maana sitaki kujiingiza ktk mahusiano na mtu kwa sasa ila i will help you, karibu inbox tuyajenge, unachotakiwa wewe ni counseling tu sio kingine
 
Wanawake JF mshikeni mkono mwenzenu huyu anahitaji faraja, uangalizi wa karibu, kuoneshwa upendo wa hali ya juu, kujaliwa.

Nimepitia nyuzi zake hayuko sawa.. Hawa ndio watu hawachelewi kuchukua uamuzi mgumu(Mungu amuepushie mbali ujinga huo)
Nimesoma comments zako nikajiuliza, inawezekana Makaveli kweli alikimbilia Tanzania nini! Refer issue ya Godfather wake marehemu Geronimo Platt ā€œJi-Jaga kujichimbia zake Chuga… umejua kuwafariji hawa wadada to keep their head up…
ā€œIf he can’t learn to love you should leave him, cause sister you don’t need him, I ain’t tryna gas up ….ā€ Pumzika Makaveli.
 
Back
Top Bottom