Nimeolewa ama nimeoa? Naombeni ushauri

Halafu unamnyima mtu hata chakula anaweza vipi kuwa na itimamu wa kufanya kazi,wewe ukiondoka mwachie hata 5000 ya nauli atajiongeza, psychological hawezi kuwa sawa ni vizuri uzungumze nae maneno mazuri ya kumfariji.

Hataki anasema namchukuliaje kumwambia afanye biashara hizo,nyie nimejaribu kila mbinu.
 
Hataki anasema namchukuliaje kumwambia afanye biashara hizo,nyie nimejaribu kila mbinu.
Sikiza na pole .......

Mwambie nimepata mkopo sehemu nataka tufungue eka wingi ili asione unataka kumpanda kichwani hapo wanaume ndo udhaifu ulipo

Labda duka ama hiki....... Then ukipata muda draft tuu hata cost allocation zote, jifanya mwambie tafuta wewe fremu ili aone umempa heshima......

Then uone majibu yake....... Fanya kila kitu kama acting ili aonyeshe response yoyote

Kumnyima msosi hapana hapo nimeumia aseeh 😢😂.......

Usimnyime msosi mpe tuu, lakini jaribu kumpozisheni aelekee kwenye lengo lako.....

Ukiondkka unaweza jitegemea Kodi kila kitu ama hapo napo mmepanga ?

Vipi watoto nao ?

Jaribu kumshawishi Ila kama unatumia force ni ngumu kukubali

Good luck 👍
 
Vijana na hivi ndivyo wanawake wote walivyo wewe unaweza ukamuoa hana kazi ukamlisha miaka yote hadi uzee wake lakini yeye miaka8 tiyari kashamkimbia mwanaume.Na hapo kaongea uongo 89% miaka8 hakuna mwanaume wakulala na kwenda kijiweni.

Hapohapo kasema ana mwaka kashajitenga nae hampi chakula hafui nk lakina jamaa bado anadunda tu wala hawazi jiulize swali huyu jamaa anakula wapi? sabauni na nguo nani ana mnunulia ? jibu unapata kuwa jamaa anajiweza wala hamtegemei kabisa huyu mwanamke 100%

Manyanza
 
Maskini Mshkaji alidhani kaoa Mke mwema kumbe Kurumbembe ona Ona sasa linavommyoosha.
Wewe ni Yale Mademu yasiyojielewa
 
Mwanamke ni wa kulelewa na hakuna cha hamsini kwa hamsini.
 
Before talaka nimechukua uamuzi ufuatao,ni mwaka sasa nimemhama chumba,nimeacha mfulia wala kujihusisha na chochote kimhusucho nimemwondoa house girl simwachii chakula cha asubuh wala mchana,anavizia cha usiku na weekends ndo anakula.😒
Ahaaa jamani jamani wanaume wengine wanasulubika duniani huku
 
Sheria ya NDOA ya Tanzania (Law of Marriage Act [Family Law] CAP. 29 R.E 2019) inamtaka Mwanaume ndiye mwenye jukumu la kutunza familia.

Ingawa mwanamke anaweza kuwa na kipato wakashirikiana lakini iwapo mwanaume anakiuka ama kukwepa jukumu la msingi la Family Maintenance anakuwa anatenda kosa.

Unachoweza kufanya, anza ngazi ya familia, kaa na wazazi ama walezi wake mzungumze pamoja na endapo hakutakuwa na matunda basi viongozi wa dini wahusike. Kisha SHERIA ihusike
 
Toka hukoo,ulivyoamua kuwa nae hugo gu mzigo gwako ulimwita nani akushauri?Fun enough wakati anafanya kazi analeta minyama home ulikuwa huropoki haya yote.
 
Haya si ndo mnayosema wanaume wawafanyie? Sasa kibao kimegeuka unaona nongwa? Hebu onja hapo walau kidogo mapito ya wanaume wenu nyie mlioolewa. Mnadai 50/50. Nadhani kwa sasa kutokana na uzoefu ulopata hapo; unaweza kutoa ushauri mzuri zaidi kwa wanawake wenzako wanaoishi maisha ya unyumba. Au sio.
 
Swala la kuachana sio kipendeleo changu sana. Ila pole, jaribu kutumia njia tofauti tofauti kumshawishi arudi katika majukumu yake usichoke, kuhudumia sio mchezo.
 
Sheria iko sawa. Lakini pia tusisahau baba huyo anafanya kazi japo sio zote. Kwa mfano joka likiingia ndani utamsikia mama akiguta kumwita mume wake "Baba naniliu, njoo haraka huku kuna dui...." au kumetokea changamoto fulani utamsikia mama akiuliza "Sasa baba naniliu, hapo unasemaje au unashauri tufanye nini?" Kwa maneno mengine naona huyo mama anataka kile anachotaka yy ndo kifanyike na sio vinginevyo. Anonesha kutaka kumkandamiza i.e. Kuwa kichwa kwa mume wake. Hiyo haikubaliki. Kama mume alishamruhusu akatafute au aende kwa wanaume/mabwana wenye kazi mbona hatekelezi hilo ila anakuja kumyanyapaa (stigmatise) huku Jf eti simfulii, simpi chakula, nimemtenga chumba n.n.k vitu ambavyo ni makosa makubwa kumnyanyasa mume wake kutokana na mapito anayopitia.
Huyo mama ni mjeuri na ni mbabe - hafai. Hiyo miaka 8 waliishi hajaona lolote zuri kwa mme wake ila ameachishwa kazi sasa imekuwa ni balaa hapo nyumbani.
 
Ongeza mke wa pili.
 
Mke mpumbavu hubomoa nyumba yake kwa mikono yake mwenyewe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…