Nimeombwa hela na mwanafunzi

Mtoto wa form 2 ana miaka 16 je ulimwambia aache tabia ya kuomba hela wanaume japo ningekuwa mimi ningemtafuna sina wema uo
 
Nyie ndiyo mnaoharibu watoto na kuwaendekeza unampaje hiyo hela yote wakati amekuomba 500 ya nauli kama mtu mzima kwanini ukumuombea kwa konda au dereva kumpa lifiti au kamlipia nauli moja kwa moja ukaondoka zako......
 
Siajona tatizo kwa binti huyo kukuomba 500/=. Amekuja kwako akiamini u sawa na baba yake hivyo utamsaidia kwa amani kabisa kuliko kuomba kwa vijana wasio waadirifu mitaani. Nilichojifunza ni kuwa huwa husaidii pasipo kupewa offer
 
Sidhani kama ana sababu yoyote ya kufanya hivyo!
 
Tatizo lipo mtoto wa kike kuomba ela tena kwa mtu asiemfahamu alafu ya kununua samaki ni malezi mabaya na mwisho wake hua mbaya endapo atakutana na mabaharia wa nchi kavu wenye kiu
Malezi ya zamani yalitufundisha sana kuliko sikuizi hata ukiwa na njaa huli kwa watu itakua kumuomba ela stranger tena kwake....sema ndo technologia hii
 
Katarudi tena hapo kwako siku nyingine kujifaragua nakuambia.

Mtoto wa kike kuombaomba hela kwa stranger tena kwa kumfuata kwake kumgongea

Wasioona tatizo nao ni tatizo.
 
Watoto wa kike.wa shule hapo ndipo hupata ujasiri wa kuomba pesa kwa wanaume kwa sababu wanajua pesa utatoa na hutaomba chochote toka kwao kwa sababu magereza bado zina nafasi.
 
Sasa tatizo nn hapo, mbn ubinadamu umewaisha siku hizi? unawaza nn sasa
Mtoto wa kike kupiga hodi kwa mtu asiyemuhusu tena me ati anaomba hela Bado wewe huoni tatizo hapo!! Mungu wangu wewe huoni jipya niishie hapo.
 
Usimchekee huyo miaka 30 inakunyemelea
 
ohoo!1 kumbe mnajuana vizuri kabisa.
hapana yaani nimemaanisha nafahamu tu kama ni kidato cha pili kutokana na uzoefu wangu wa kuishi hapa karibu na shule......nina marafiki ambao ni walimu pia hivyo siku wakideal na kidato cha pili huwa namuona huyo binti hivyo sina shaka katika hilo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…