Habarini!
Kuna jambo limenitokea, linanipa maswali na mshangao kiasi.
Ninakaa jirani na shule, jirani sana tu. Ni mtu mzima mimi.......35 yrs. Kwa sasa shule nyingi zipo ktk makambi kwa vidato vya 2 na 4, hii ni mojawapo pia.
Jioni ya leo, nikiwa sina hili wala lile nimepumzika tu nasikia hodi ikigongwa. Nilipomruhusu aingie bs alikuwa n mwanafunzi flan wa kidato cha pili.......aliamkia na kisha akaniomba tshs 500/=. Nilipigwa na bumbuazi kupita maelezo lkn nikajifanya sina nilichokishangaa. Nikamuuliza unataka kununua nn akajibu anataka kununua samaki alie ugali (akilini nilitegemea nisikie peni au daftari). Nikampa tshs. 2000/=. Aliipokea haraka, akashukuru kisha huyo haraka akaondoka.
Bandugu, tangu muda huo nimetafakari mara kutafakari ujadiri wa huyo binti bado sijapata majibu mpaka nimemua nifanye sharing nanyi kisa hiki.....