Habari wakuu.
Nataka kuinspire wanaotamani kuanza hii challenge.
Mwanzo mgumu lakini ukishinda vishawishi huko mbeleni ni mteremko yaani unaserereka tu.
Niliwazaje kuacha Masterbution, Pornography, Sex?
1.MEDITATION.
Kuna siri kubwa ndani ya meditation, anza kujifunza jinsi ya kufanya meditation, tafuta YouTube, soma articles, sikiliza podcasts zenye kuhusu meditation. Itakusaidia sana kujitambua wewe ni nani na unapaswa kufanya nini.
2. SALA
Kwa imani yako, ukiwa una omba nafsi huwa inakusuta na kufanya uichukie dhambi. Kuna nguvu ndani ya maombi. Usiache kumuomba Mola wako.
3. FOOD
Jitahidi usile hovyo na vyakula vyenye mafuta mengi. Acha kutumia sukari, ni mbaya ikwemo soda, cakes, candies etc
Kula matunda kwa wingi, mbogamboga , viazi vitamu baadala ya chapati , inasidia sana hii.
4. OGA MAJI YA BARIDI ASUBUHI
Hii inaongeza sana mwili kuwa active na kuondoa uvivu unaoweza kukupelekea kufanya vitu vya ajabu kama kujichua.
5. MAZOEZI.
Binafsi kila nikiamka asubuhi napiga pushups 40, sit ups 30, squats 30 ndio nioge.
Mazoezi yanasaidia kuleta ukakamavu na kukufanya usifanye vitu vya uvivu kama kujichua.
6. SOMA VITABU
Upe ubongo wako mazoezi usiwe idle, hapa jenga tabia ya kusoma vitabu vyenye vitu unapenda kuvifahamu.
Hayo mambo juu yamenisaidia sana kwa kiasi kikubwa kufikia nilipo leo.
Nilikuwa naacha kujichua, porno au random sex najikuta baada ya muda narudi tena. Hii ilinikatisha sana tamaa.
Nikawa nafarijiwa na maneno ya watu eti kujichua huwezi kuacha na haina madhara. HUU NI UONGO.
Hakuna tabia usiyoweza kuiacha, Niamini mimi.
Its always seem impossible until is done.
Ahsanteni!