Nimeota nipo nje ya mwili wangu, ndoto hii inamaana gani?

Nimeota nipo nje ya mwili wangu, ndoto hii inamaana gani?

PLATO_

Senior Member
Joined
Jan 25, 2020
Posts
116
Reaction score
230
Hivi Majuzi niliona nimeamka kutoka usingizini lakini cha kushangaza nilijiona bado nipo kitandani nimelala.

nilijaribu kujiamsha lakini sikuamka, basi nikapotezea. Nikaamua nitoke nje niende dukani nikanunue Azam Energy lakini cha kushangaza kila nikipiga hatua siendi popote.

Nikachanganikiwa! nikajaribu kujiamsha lakini wapi.

Akili ikanijia labda Mimi ni nafsi inatakiwa nilale juu ya mwili ili niingie ndani ndio ntaamka.

Basi nikafanya hivyo lakini cha kushangaza!, sikuwa nafsi nilikuwa na Mwili kama ule uliolala kitandani.

Nikatumia sana nguvu kuingia ndani lakini ilishindikana basi nikaamua kulala pengeni ya ule mwili mwingine kwasababu nilikuwa siwezi kwenda popote.

Nimetafakari sana hii ndoto bila majibu.
 
Sema tu Kweli,

Umetoka kuangalia muvi za kinigeria ukaamua kuigeuza kuwa Uzi!!

Kama uko serious Kweli umetoa ,hiyo ni hatari.
 
Ungejaribu kupaa! Naskiaga roho zinapaaga!
Anyway ulisema ni ndoto hivyo ni ndoto mfano Mimi lishaotaga niko mtume na nabii issa tunapiga story live
 
Back
Top Bottom