Nimeota nipo nje ya mwili wangu, ndoto hii inamaana gani?

Nimeota nipo nje ya mwili wangu, ndoto hii inamaana gani?

Hivi Majuzi niliona nimeamka kutoka usingizini lakini cha kushangaza nilijiona bado nipo kitandani nimelala.

nilijaribu kujiamsha lakini sikuamka, basi nikapotezea. Nikaamua nitoke nje niende dukani nikanunue Azam Energy lakini cha kushangaza kila nikipiga hatua siendi popote.
Nikachanganikiwa! nikajaribu kujiamsha lakini wapi.

akili ikanijia labda Mimi ni nafsi inatakiwa nilale juu ya mwili ili niingie ndani ndio ntaamka.

Basi nikafanya hivyo lakini cha kushangaza!, sikuwa nafsi nilikuwa na Mwili kama ule uliolala kitandani.

Nikatumia sana nguvu kuingia ndani lakini ilishindikana basi nikaamua kulala pengeni ya ule mwili mwingine kwasababu nilikuwa siwezi kwenda popote.

Nimetafakari sana hii ndoto bila majibu.
Ina maanisha kwamba ulikuwa nje ya mwili wako
 
Sema tu Kweli,

Umetoka kuangalia muvi za kinigeria ukaamua kuigeuza kuwa Uzi!!

Kama uko serious Kweli umetoa ,hiyo ni hatari.
Nimeota kweli lakini sijachukulia serious kiivyo, kwa sababu kipindi nipo chuo nilikuwa nafanya Astral projection lakini sikufanikiwa.
Lakini hapa majuzi nimejikuta naota nipo nje ya mwili.

Naamini ni Astral Projection.
 
Nimeota kweli lakini sijachukulia serious kiivyo, kwa sababu kipindi nipo chuo nilikuwa nafanya Astral projection lakini sikufanikiwa.
Lakini hapa majuzi nimejikuta naota nipo nje ya mwili.

Naamini ni Astral Projection.
Kama una amini kwanini umeleta uzi? Au unapenda kusikia tu watu wakireply utakufa soon, utakufa kabla ya Xmas?
 
Mda si mrefu, ila kifo chako hakitakuwa cha kawaida, inaonekana utachukuliwa msukule na ndugu watazika tu kitu chenye mfano wa mwili wako. Ongeza maombi, pia unaweza ni PM kwa ajili ya maombi zaidi na sadaka. Amen
Unataka kunigombanisha na ndugu zangu. Siamini kwenye Miracles
 
Back
Top Bottom