KING MIDAS
JF-Expert Member
- Dec 1, 2010
- 8,589
- 16,936
Jana tarehe 17/12/2024 nilipanda miti minne mtaa wa Mwenge Kijijini.
Nimepanda jumla ya miti minne, mmoja mbele ya ilipokuwa shule ya Mwenge Open Academy (MOA), na mingine mitatu nimepanda mbele ya Kebby's Hotel.
NI utamaduni wangu wa kupanda miti kandokando ya barabara ili kuwafanya waendao kwa miguu wapate hewa safi chini ya kivuli watembeapo kwa miguu.
Maeneo mengine niliyopanda miti ni pamoja na Boko, Bahari Beach, Mikocheni, Ununio na Oyster Bay.
Kila ninapopanda miti siiachi hivihivo, huiwekea mbolea na kumwagilia mpaka pale inaposhika kabisa na kuweza kujitegemea yenyewe.
Karibuni wana JF tufunge mwaka kwa kupanda miti kwenye maeneo yanayotuzunguka.
Mimi pia ni mwanachama wa TREE OF LIFE FOUNDATION