Nimepanda miti minne, mitatu mbele ya hotel ya Kebby's na mmoja ilipokuwa shule ya Mwenge Open Academy (MOA)

Nimepanda miti minne, mitatu mbele ya hotel ya Kebby's na mmoja ilipokuwa shule ya Mwenge Open Academy (MOA)

Jana tarehe 17/12/2024 nilipanda miti minne mtaa wa Mwenge Kijijini.

Nimepanda jumla ya miti minne, mmoja mbele ya ilipokuwa shule ya Mwenge Open Academy (MOA), na mingine mitatu nimepanda mbele ya Kebby's Hotel.

NI utamaduni wangu wa kupanda miti kandokando ya barabara ili kuwafanya waendao kwa miguu wapate hewa safi chini ya kivuli watembeapo kwa miguu.

Maeneo mengine niliyopanda miti ni pamoja na Boko, Bahari Beach, Mikocheni, Ununio na Oyster Bay.

Kila ninapopanda miti siiachi hivihivo, huiwekea mbolea na kumwagilia mpaka pale inaposhika kabisa na kuweza kujitegemea yenyewe.

Karibuni wana JF tufunge mwaka kwa kupanda miti kwenye maeneo yanayotuzunguka.

Mimi pia ni mwanachama wa TREE OF LIFE FOUNDATION View attachment 3179601

img20241217060238-jpg.3179597
👏👏👏
 
Umefanya safi.........sio lazima wengine wapende au hata hizo sheria pia zikupende ............sheria ni nini kwanza ? Mbona hazipambani na wasiojulikana wezi na mafisadi ya nchi? Mbona zinachezewa tu huko kwenye mahakama watu wanakamatwa na ushahidi na hawafanywi chochote?? Braza endelea kupanda miti .......ili nyani zao zije kula hayo matunda.........
 
Safi sana .... umenikumbusha enzi zangu wakati nikiwa active member wa roots &shoots tulipanda miti mingi sana

Ova
 
Umeshawahi kuona wapi MTU kashitakiwa kwa kwa kupanda miti?
Kuna masharti na taratibu zinazotakiwa kufuatwa kabla ya kupanda miti, hasa ikiwa ni katika maeneo ya umma au maeneo ya hifadhi. Hii ni ili kuepuka athari zinazoweza kutokea kama vile uharibifu wa mazingira au kuingiliwa kwa usalama wa mazingira asilia.

Kwa hiyo, kabla ya kupanda mti, inashauriwa kupata kibali kutoka kwa mamlaka zinazohusika, kama vile Serikali za Mitaa, Wizara ya Mazingira, au Taasisi ya Usimamizi wa Rasilimali za Asili.🐼
 
Serikali za mitaa hii ambayo wanasimamia uchafuzi wa mazingira na ukataji miti hovyo unaofanywa na matajiri pekee au zipi hizo?
 
Kuna masharti na taratibu zinazotakiwa kufuatwa kabla ya kupanda miti, hasa ikiwa ni katika maeneo ya umma au maeneo ya hifadhi. Hii ni ili kuepuka athari zinazoweza kutokea kama vile uharibifu wa mazingira au kuingiliwa kwa usalama wa mazingira asilia.

Kwa hiyo, kabla ya kupanda mti, inashauriwa kupata kibali kutoka kwa mamlaka zinazohusika, kama vile Serikali za Mitaa, Wizara ya Mazingira, au Taasisi ya Usimamizi wa Rasilimali za Asili.🐼
Waswahili mna roho za kutu sana, yaani hamtaki mtengenezewe mazingira mazuri, mtaibua vihoja vya ajabu ajabu.
 
Keep it up mkuu, hakika wewe ni mfano wakuigwa. Zibarikiwe kazi za mikono yako. Hongera sana.
 
Umenikumbusha enzi za Mali hai Club. Kuna mitaa nikipita naona ile misitu tulitengeneza najisikia faraja kuwa sijapita duniani bure bure.
 
Mkuu jambo jema sana hilo mwaka 2006 nilipanda miti3 kanisani sasa hivi miwili iliyopo ni kimbilio wana kwaya wanakaa hapo kufanya mazoezi na mambo mengine mengi. NItaanza tena kupanda
 
Umenikumbusha enzi za Mali hai Club. Kuna mitaa nikipita naona ile misitu tulitengeneza najisikia faraja kuwa sijapita duniani bure bure.
Watawapataje hawa mali club munama? nahitaji support yao.niko moshi
 
Miti hii niliipanda nnje ya uwanja wa jamuhuri Dodoma 2020 sijui Bado kama Bado hiko hai
 
We mtu wa faida sana kwenye jamii yetu, ukija mufindi nifute nikupe Miche ya parachichi mitano na debe mbili za parachichi
 
Back
Top Bottom