Hao bodaboda wasio kuwa na akili usitake kufanya generalization kuwa wote wapo hivyo mbona wapo madereva vichaa wa magari ,narudia tena na tena kukwambia mimi ni dereva wa vyombo vyote hivyo makosa yapo kwa watu wote,,mbona kuna madereva wengi wa magari wamesababisha vifo tena kwa uzembe!!!
Wewe ni dereva mjinga unaeongozwa kwa hisia hasi,sifa ya dereva ni kuwa mvumilivu na busara sasa Kama hauna uvumilivu utaishia pabaya.
Nina gari lakini mara nyingi natumia usafiri wa pikipiki kwa safari ndefu ina maana ikitokea kidogo nikafanya mistake inayoweza kukwepeka kwahiyo hukumu yangu nikanyagwe na gari sio?
Acheni mawazo hasi kila mwendesha pikipiki ni fukara
Ningekuwa dereva mjinga ninayeongozwa na hisia hasi, yule dereva wa jana wa boda boda ningemsukumia kwenye kingo za bara bara tena za zege.......mimi nipo na safari zangu, imagine mtu wa boda boda ananifuata hapa nyuma, kaacha mita moja tu aguse bampa la nyuma upande wa kushoto...
Nikaanza kuonyesha ishara ya indicator ya kushoto kuwa ninataka kutoka...bado kakomaa kama vile ananidai....
Nimefika ninapotaka kutoka barabara kubwa bado kakomaa, nikatumia hekima nikasimama, huku napigiwa honi nyuma yeye akaniovateki kushoto kwa mbwembwe kuwa kashinda ligi....kisha akaniangalia vibaya..akajaza moto akapotea....
Nisingesimama alikuwa anajaa kwenye aidha mlango wa kushoto wa abiria au mlango wa nyuma...
Sasa mtu kama huyu, sehemu tupo wawili tu, kwa nini nisimsogezee mtaroni ?....
Mwisho naomba nikuase jambo moja...
Punguza dharau...
Wewe kama kwenu maisha yalikuwa ya mserereko, basi heshimu watu wenye passo za pistoni 3....
Na kama umejaliwa kazi/biashsra inayolipa, heshima iwe kitu cha msingi...maisha hubadilika..
usiite magari ya watu viCrown, sijui vigari vya mkopo, vitakataka....hujui mtu amejinyima mambo mangapi akanunua hayo magari...
Nilikuwa nafanya kazi kwenye mazingira yenye snow na baridi NEGATIVE 20 °C kwenye nchi za watu....ndiyo nikaweza kutimiza baadhi ya ndoto zangu ikiwa ni pamoja na kununua hizo unazoita vigari vya mkopo...
Hao wenye hizo unazoita viCrown hujui walitoka jasho na damu kiasi gani...heshimu chombo cha mtu..