Nimepata agents wa kuniuanganisha na kazi nchini POLAND. Je ni nitapa au nitaliwa hela yangu tu Bure na kazi nisipate

Poland si nchi yenye kupenda sana wageni hasa wa kutoka huku, wameweka Hadi sheria ya kwamba mfano mkimbizi akitaka kuingia bila makaratasi au kufuata sheria ni ruhusa kuuliwa Kwa risasi huko mpakani, hivyo hata kama ww unaingia Kwa njia za halali kuwa makini.
 
kijana wangu kimbia haraka unaenda kutapeliwa. tena eti agent ofisi magomeni? kwa matapeli wakiokubuhu, na wapo wengi wamefungua tuoffice wanajifanya agent wa kazi za nnje kutapeli vijana, na tutawashulikia very soon kisheria
 
Hakuna Agent wa kazi hapo Magomeni alikuwepo Babu mtama mchungu mzee wa passport kanjanja na mihuri feki miaka hiyo ni vizuri umeanza kuuliza hakuna kazi hapo hata wakikupa documents za Ubalozini jua ni sehemu ya kupaka rangi ili wakuibie nao wanafanya kujaribu tu ikishindikana hakuna wa kumuuliza maana pesa mmepeana mkononi...
 
Hiyo Ukraine inakuhusu. Jiandae kisaikolojia kupitia mafunzo ya muda mfupi ya KIJESHI huko Poland then unaenda Mistari wa Mbele wa Vita huko Ukraine Kwa kivuli Cha wapiganaji wa kujitolea kuitetea Ukraine.
 
Mkuu wasikukatishe tamaa haya mambo yapo na nimeshuhudia kwa watu wangu wa karibu. Jambo la kuzingatia hakikisha uyo agent amesajiliwa na ana ofisi, kuna mmoja town namjua kanyooka balaa na watu wanasafiri nnchi za ulaya. All the best.
ili akufate inbox umtapeli wewe? acheni utapeli vijana[emoji34]
 
Huwa nashangaa sana kwanini hao Agents ambao ni trusted wana fichwa fichwa as if ni siri hembu wawekeni hapa tujue mtu akiwa na shida asianze kuhangaika
 
Mkuu wasikukatishe tamaa haya mambo yapo na nimeshuhudia kwa watu wangu wa karibu. Jambo la kuzingatia hakikisha uyo agent amesajiliwa na ana ofisi, kuna mmoja town namjua kanyooka balaa na watu wanasafiri nnchi za ulaya. All the best.
Wanauzi huyu ndo agent mwenyewe sasa wa Magomeni kaamua kujitokeza bila shurti πŸ˜€
Haya muulizeni maswali muhimu atawajibu πŸ˜…πŸ˜…
 
Mkuu kuwa makini hiyo ni ngumu sana
 
Nakushauli Norway, Denmark au inchi za Scandinavian. Wanamishahala mizuri ukiludi nyumbani unafanya jambo lako kubwa, mimi nipo kwenye michakato ya kwenda Denmark. Ila kuhusu utapeli au la sijajuaa inategemeaa na agent wako na kama mtu aliyekuconnect unamwamini basi ondoa shaka
 
Ahsante kwa ushauri mkuu..ntumie njia ipi kujua kama amesajiliwa?
 
Jaribu bahati km ni kupoteza ushapoteza ving tu uko nyuma so risk maisha ni risk na usiogope turisk
 
Mkuu wasikukatishe tamaa haya mambo yapo na nimeshuhudia kwa watu wangu wa karibu. Jambo la kuzingatia hakikisha uyo agent amesajiliwa na ana ofisi, kuna mmoja town namjua kanyooka balaa na watu wanasafiri nnchi za ulaya. All the best.
Hatupo hapa kumtisha mtu,Ata kalynda alikuwa na ofisi,kasajiliwa na baadhi ya watu walivuta mpinga ......ila tulipiga sana kelele juu ya hizo scheme za hela unafahamu yaliwakuta watu kadhaa.....

Sisi tupo hapa mguu ndani ,mguu nje hela aliyohangaikia kwa MDA mrefu asijeingizwa mkenge kiboya
 
Kabla ya yote unaongea ki Polish ?, Ni kazi gani unaunganishwa ambayo kuna demand huko Poland ?

Hizo pesa za kuwapa bora ongezea mtaji unless wanakulipia kila kitu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…