Nimepata ajira wife ameongeza matumizi ya pesa zaidi ya mara mbili

Laki 1 kwa wiki haitoshi? Twende pole pole, hiyo laki kwa wiki ni baada ya kuhakikisha kila kinachohitajika kipo au laki ndo kila kitu kipatikane hapo? Maji, unga, mchele, chumvi, mafuta ya kupikia, sukari, majani ya chai, mboga, mkaa, n.k?

Kaeni mjue gharama za vitu kwa mwezi, umeme, king'amuzi, matumizi yake binafsi, gesi, gunia la mkaa, nunua nyama, samaki, maharage, sukari, sabuni ya kufulia, kuoshea vyombo, kuogea, majani ya chai, unga wa ugali, nauli, n.k kisha mkabidhi fungu hilo, mkabidhi na sh 5,000 ya kila siku, baada ya hapi msijuane!

Akitaka pesa zaidi ya hapo, apeleke maombi Dawati la jinsia, utampea kule.
 
Miaka2 sio sasa. Umeskia bei ya mafuta ña vyakula ilivyopanda?

Halafu wewe unaweza kuwa mwanaume bahili hadi kwa mkeo kweli!?

Mama D issue siyo ubahili shida bado hatujajenga tunaishi kwenye nyumba ya kupanga.
 
Mistake kubwa itakuwa ulimwambia mkeo kipato chako

Code moja wapo ambayo hupaswi kushare na mkeo ni ukweli kuhusu kipato chako halisi.

Anaweza jua kazi yako ila kipato chako halisi mkadirie asijue exact figures
 

Asante sana kaka kwa usahauri
 

Nashukuru sana mkuu shida nafanyia kazi mbali na yeye kwa hiyo kidogo ni Changamoto
 
Sijajua unapoushi wewe lakini kama ni familia changa ya watu wawili mfano Morogoro : Mchicha fungu la haja Mia tano fungu mbili buku. Nyama nusu kilo 3500, vitunguu fungu la maana Mia tano, nyanya mia tano, mafuta lita elfu 4 lakini hununui kila siku, mchele kilo elfu moja Mia mbili mpaka Mia nne. Kiukweli elfu 10 ilitakiwa iwe inatosha kabisa. Ushauri wangu ni huu ukipata salary nunua vitu vya jumla vifuatavyo: mchele nenda mashine za kukoboa nunua 50kgs, unga nunua kufuko cha 25kgs, mafuta ya kupika lita tano, ngano ya Azam 5kgs, sukari, chumvi, nazi za pakiti, vitunguu, maharage, dagaa etc... Baada ya hapo mpe pesa kwa matumizi yake binafsi kulingana na kipato chako, na pia pesa ya matumizi madogo ya ndani kama nyama, nyanya etc... Mwisho kaa naye mkubaliane nini malengo yenu kwa huo mwaka na miaka mitano ijayo? Mfano kuanzia Mwaka huu tuanze kufanya serving kwa ajili ya kununua gari au kiwanja au kupata mtoto ili aone umuhimu wa serving na kubana matumizi. Asante.
 
Miaka2 sio sasa. Umeskia bei ya mafuta ña vyakula ilivyopanda?

Halafu wewe unaweza kuwa mwanaume bahili hadi kwa mkeo kweli!?
Sasa wakiendekeza kutumia laki moja ndani ya siku tatu wataweza kweli kujijenga au kuanzisha biashara? Je kazi ikiisha kama ni ya mkataba au matatizo yoyote?
 
Nafikiri na wanaume waanzishiwe mambo ya kitchen party maana kanuni na taratibu za kuishi na hawa viumbe hazipo tena.
 
Sasa wakiendekeza kutumia laki moja ndani ya siku tatu wataweza kweli kujijenga au kuanzisha biashara? Je kazi ikiisha kama ni ya mkataba au matatizo yoyote?

Wapi kasema mke anataka laki na wewe..... wacha kutia pilipili
Akae na mkewe waweke mipango sawa sio aje kulialia hapa jf
 
Kama mnanunua kila siku vitu vya kutumia Kama vyakula Hapo nyumbani kwako mkuu, nalo Hilo ni tatizo, jitahidini kununua vitu kwa jumla jumla ndo inakua afadhali kidogo na hata pia mtapata nafasi ya kufanya vitu vingine vya maana yan apo najua tu pesa mnatumia sana kwa sababu ya Kula tu,nunua kwa jumla mazagazaga inasave sana,hayo mengine yanapangika vzuri mkikaa chini mkayaongea na shemeji...
 
sasa mkuu umepata kazi na mshahara mnono unataka ukirudi nyumbani ukute ugali tembele kama zamani, aendelee kukufulia kwa sabuni za magadi kama zamani, aendelee kujipaka baby care na kusuka twende kilioni kama zamani?. matumizi ya pesa ndio hayo, na ukipandiswa cheo na matumizi yatapanda cheo vilevile, kuwa mpole mkuu mkeo hajakosea popote
 
Maisha ni uchaguzi, japo maisha yamepanda kiasi lakini usipijidhibiti utaishia matumizi ya kawaida tu, mkazie weka budget ya familia mkabidhi yeye na ziada, then wewe weka emergency tu, zingine peleka kwenye mambo ya msingi, mfano program za kiwanja kama huna,, kesho ni muhimu kuiangalia zaidi ya leo
 
Kila mbuzi hula kulingana na urefu wa kamba yake....kama anaujua hadi mshahara wako unategemea afanye nini? We mpe tu kama kujenga atajenga kwao
Sio kila mbuz atakula kwa urefu wa kamba yake wengine hula kwa huruma ya mchungaj wake, wanawake wanajsahau mapema sana kama mlkua kwenye msoto ukipata Chanel anabadlka mpka unajiulza huyu kawaje na kama ulkua na pesa zkapata naul au kaz ikaisha utamwona visa vyake kila kukicha na mabeg yake mgongon kama ngoni migration Leo kwa Dada ake kesho kwao hatulii tena hata ukiongea hakuelew wala kukuskia kikubwa Mungu atupganie tu watoto wa kiume sis
Spikn from Exprienc
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…