Nimepata au nimepatikana?

Nimepata au nimepatikana?

Wadau mwaka 2017 nilifunga ndoa na mpenzi wangu F niliyedumu naye kwenye mahusiano kwa miaka mitatu, Nadhani sikufanikiwa kumjua kwa undani kiivyo! Jambo linalonitatiza sana ni ishu ya pesa, mke wangu hawezi kutoa hata 100 kununua chumvi, mambo yote ya chakula, Ada,Kodi ya pango na matumizi yote nagaramia mimi, mke wangu pesa yake anaiweka kwenye investments tu, utasikia kanunua kiwanja, kapanua biashara yake, kaanza ujenzi n.k.

Kinachoniuma mimi pesa yangu yote inaenda kwenye matumizi ya familia na yakwako inaenda kwenye maendeleo ya familia. Sasa kwa marafiki niliowashirikisha situation yangu wengi wananiambia umepata mke mwenye akili ya maisha, wengine wananiambia Nimekwisha!.. Nawasilisha naomba mawazo yenu (Tuepuke matusi na kejeli)

Simple tu,
Embu mwambie Sasa badilishaneni matumizi, yake yawe yako. Na yako yawe yake, ila usijenge kwenye kiwanja chake, Anza na chako fresh.
 
Hivi yale majukumu pale Eden hukuyaelewa vizuri eeh, mliambiwa wanaume mtakula kwa jasho na sisi tutazaa kwa uchungu, so baba pambana ya hela yote timizia mahitaji ya familia yako, pesa ya mwanamke usiipigie hesabu sana maana mtaanza kupangiana hata zamu ya kuosha vyombo na deki sasa. Kama ulioa sababu ya pesa zake , badili mtazamo pambana.
 
Umesoma proverbs 31??kama unataka tutumie bible
 
Ndo maana Sioni ulazima wa kuoa napambana na maisha yangu mwenyewe
 
Kuna jamaa mmoja namfahamu

Yeye kadi ya benki ya mkewe anayo yeye na wote ni watumishi wa serikali

Yaani mshahara ukiingia tu dada wawatu anaona meseji tu ila mshahara hauoni hawezi chukua hadi akaombe kwa jamaa[emoji1787][emoji1787]

Daaah ndoa hizi
 
Hivi yale majukumu pale Eden hukuyaelewa vizuri eeh, mliambiwa wanaume mtakula kwa jasho na sisi tutazaa kwa uchungu, so baba pambana ya hela yote timizia mahitaji ya familia yako, pesa ya mwanamke usiipigie hesabu sana maana mtaanza kupangiana hata zamu ya kuosha vyombo na deki sasa. Kama ulioa sababu ya pesa zake , badili mtazamo pambana.
Mwanamke anayempenda mume wake lazima atamuonea huruma mume wake. Mwanamke mbinafsi anahatarisha ndoa ya familia. Na maisha haya ya watumishi halafu majukumu yote anamuachia mume wake it's unfair ndio maana huwa nijifikirie pamoja na elimu yangu hii ya MSc naogopa kuoa Mwanamke mwenye kazi
 
Kuna jamaa mmoja namfahamu

Yeye kadi ya benki ya mkewe anayo yeye na wote ni watumishi wa serikali

Yaani mshahara ukiingia tu dada wawatu anaona meseji tu ila mshahara hauoni hawezi chukua hadi akaombe kwa jamaa[emoji1787][emoji1787]

Daaah ndoa hizi
Kwanini wasiweke mshahara Kati wakaupangia matumizi Kwa pamoja. Na huu ni ukatili mwingine
 
U are too wrong broh siyo kwamba wanaume atupendi maendeleo ya mwanamke ila unaangalia hayo maendeleo Yana agenda gani ..

Utajisikiaje ukisikia mkeo kajenga kwao gorofa uku ata akiumwa awezitoa ata shing 100 yamatibabu yake kila kitu anategemea kwako .. ?

Ukimuacha mkeo afanye investment bila msaada wako ni hatari Sana kwa ndoa yenu

Leo atanunua kiwanja kesho atajenga keshokutwa atapata lishkaji atalipangisha kwenye iyo nyumba watoto atawapeleka boarding so what's next ?

Ninaushuuda wa live kabisa sehem niliokua nafanya kazi boss wangu siku moja alirudi nyumban kwake na washkaj alikuta mkewe kaweka party anasherekea ujio wa NDINGA mpya ambayo amenunua Tena gari Kali zaidi ata ya mmewe ..jamaa alijisikia vibaya Sana .. iyo ni dharau kubwa Sana ..

Zaman wazee wetu walikuw wanalima nakuvuna pamoja ila kwenye mauzo mwanaume ndo huongea kauli ya mwisho yanini kifanyike..

Sikuizi wakati mwanaume anaangaika kupambania familia kupeleka watoto shule kulipa bills mbali mbali kusaidia wakwe kutumaela kwa wazazi .. wakatiuo mwanamke Ela yake ana invest .. siku ukiishiwa mke anaanza dharau .. utamfanya nini wakati .. kashajenga kashafungua na biashara kashapata na connections ? ..

Wanaume amkeni mwanamke afanyagi vitu kijinga jinga tu hua ana agenda..
Mi binafsi njia nayoona ya kummiliki mwanamke ni kumfanya toothless! Binafsi hata kitu akinunua mke nitapenda nikifanye cha familia. Ile hali ya kumpa wadhifa kuwa ni chake per se sintohitaji iwe hivyo. Najua namna ya ku go about it very gently ili isilete mtafaruku. Mke akileta ubishi kwenye hilo najua kabisa sina mke.

Kama ni shamba nitaandika jina la mtoto. Kama ni kiwanja ntafanya the same. Provided sinto mdhulumu wala sina mpango huo ila nataka tu kumuondoa kwenye kile kiburi kuwa anamiliki vitu nje ya vya familia.
 
Kuna jamaa mmoja namfahamu

Yeye kadi ya benki ya mkewe anayo yeye na wote ni watumishi wa serikali

Yaani mshahara ukiingia tu dada wawatu anaona meseji tu ila mshahara hauoni hawezi chukua hadi akaombe kwa jamaa[emoji1787][emoji1787]

Daaah ndoa hizi
Ila cha ajabu jamaa ndio atadumu vizuri na mkewe kuliko hawa mapoyoyo ambao wana access na hela full time! Mwanamke anaweza fanya maamuzi ya ajabu kama atakosa monitoring and control ya mume.

Unampa nafasi intruder aanze kumtongoza mkeo na kupata anachotaka kupitia kipato chake.
 
Asilimia kubwa hapa mnamshambulia Jamaa, ila kiuhalisia ndoa ni kusaidiana...hakuna cha pesa ya mke wala ya mume as long as anafanya biashara au kazi ni wajibu wake kumpiga tafu mme wake kimaisha. Tena ukikuta mke mwema anaweka hela yote mezani ipangiwe matumizi.
 
Wadau mwaka 2017 nilifunga ndoa na mpenzi wangu F niliyedumu naye kwenye mahusiano kwa miaka mitatu, Nadhani sikufanikiwa kumjua kwa undani kiivyo! Jambo linalonitatiza sana ni ishu ya pesa, mke wangu hawezi kutoa hata 100 kununua chumvi, mambo yote ya chakula, Ada,Kodi ya pango na matumizi yote nagaramia mimi, mke wangu pesa yake anaiweka kwenye investments tu, utasikia kanunua kiwanja, kapanua biashara yake, kaanza ujenzi n.k.

Kinachoniuma mimi pesa yangu yote inaenda kwenye matumizi ya familia na yakwako inaenda kwenye maendeleo ya familia. Sasa kwa marafiki niliowashirikisha situation yangu wengi wananiambia umepata mke mwenye akili ya maisha, wengine wananiambia Nimekwisha!.. Nawasilisha naomba mawazo yenu (Tuepuke matusi na kejeli)

Swali langu ni moja tu.

Hivyo vitu anavyofanya mkeo, hua mnakaa mnakubaliana kwamba sasa tufanye hivi au ni yeye anaamua kufanya bila kukushirikisha?

Nijuavyo mimi, mke wa ndoa mnatakiwa mkae chini mpange kwamba sasa tunanunua kiwanja (hata kama pesa atatoa yeye), sasa tujenge, tununue gari n.k. Kama hamfanyi hivyo, ipo shida.
 
Back
Top Bottom