Jamani mi natoa ya moyoni leo kwasababu naamini hapa JF ndo sehemu pekee nitaongea na kero yangu ikatatulika.
Huwa tunaambiwa mteja ni Mfalme, lakini huu ufalme mbona kama umegeukia Kwa watoa huduma?
Hili suala nilishaliona sana NHIF lakini kwasababu sikuwa na pa kuongelea basi likawa linauma.
Pale kuna wale watoa huduma unaowakuta dirishani ukienda wanahisi wao wanakusaidia, wanakupa msaada wakati ni jukumu lao.
Mimi binafsi ni Mwanachama wa NHIF nimejiunga na kifurushi cha TIMIZA.
Sasa nilienda kuchukua kadi pale NHIF plae katika ofisi zao zilizopo kweye jengo la PSSF, nimefika pale namkuta mbaba pale dirishani, picha linaanza naenda dirishani ananiangalia tu, nikamwambia nimekuwa kuchukua kadi.
Akauliza kwahiyo? Heee nikamwambia kwahiyo? Ndo akauliza hiyo kadi ni yako au nikamwambia ndio, akasema nani kalipia nikamwambia mume wangu, hee akasema mpaka aje yeye ndio tutatoa hiyo kadi.
I was like what!!!! Ila nikasema sawa kwa sababu kila sehemu ina sheria labda ndio sheria, nikamuuliza kaka hii Sheria imeanza lini maana mimi ndio nilikuja kufuata kadi ya mume wangu pamoja na watoto, sasa inakuwaje unasema siwezi kuchukua kadi yangu mpaka yeye?
Akasema "Sina muda wa kuongea sasa hivi, sogea pembeni nihudumia mtu mwingine 😟😟."
Aisee nilikasirika, nikabaki nimesimama akasema nakuitia mlinzi, heee nikamuuliza kaka una shida Gani?
Hee mara mlinzi akafika pale ohooo mara nikapelekwa kwenye ofisi hapo NHIF.
Nikaanza kuulizwa nikaeleza kila kitu ndio nikahudumiwa. Tena yule mtu wa ofisini alikuwa anaongea vizuri hadi akaomba msamaha.
Wana JF hii sio mara ya kwanza linatoke swala kama hili pale NHIF, kuna siku pia nilienda kusajili nikakuta mhudumu anamfokea mteja pale dirishani, I was like hivi hii ni namna gani ya kutoa huduma?
Jamani NHIF embu jitahidini kutoa huduma nzuri kwa wateja yaani tulipie vifurushi bei kubwa na bado tukija ofisini kwenu mtugombeze?
Wana JF Naomba nijue kama hili suala limenikuta mimi tu au na nyie mmekutana nalo