Nimepata kazi ambayo inaniruhusu kuhamia USA nikitaka, lakini mshahara ni ule ule popote nitakapoamua kufanyia kazi

Mimi naona hamia US mkuu utajiongeza hata na mishe nyingine hata hivyo hilo jimbo la Texas maisha si expensive kihivyo, kulinganisha na majimbo kama New York au California kwanza TX ni kati ya majimbo ya US ambayo hayana kitu kinaitwa State Income Tax, na ni jimbo ambalo kwa sasa linapokea wahamiaji wengi toka majimbo mengine yenye maisha ya aghali
 
Sijui kuhusu nyinyi wenzangu ila binafsi sajawahi kutamani kuishi nje ya Nchi yangu kabisa. I mean, everyone is here. Wazazi, Kaka zangu, dada, Rafiki zangu, Ma ex, ma crush wangu kila cha maana na cha kipuuzi kwangu kipo hapa. Mnawezaje kwenda kuanza moja kwenye nchi za kigeni zenye tamaduni tofauti kabisa na mlizokulia huku mkiacha nyuma kila kilichowakuza... ?!
 

Jadda... samaleko 😎

-Kaveli-
 
Nawaza mtu mwenye elimu ya kulipwa mshahara wa 19,125,000
Anakosaje uwezo wa kuchanganua kipi ni kipi kwake mpaka aulize jf .... nawaza tu wakuu
JF ina watu wengi wenye exposure mbalimbali mkuu kuhusu masuala ya maisha, kuhamia na kuishi nchi za watu. So, nimeleta hapa just to get ideas hasa kutoka kwa watu ambao walishafanya movements za hivyo. Hakuna mjuzi wa kila kitu katika hii dunia mkuu, unaweza ukawa ni mbobezi katika field yako, lakini haimaanishi sasa hiyo inakupa uzoefu wa mambo ambayo huna uzoefu nayo.
 
Nawaza mtu mwenye elimu ya kulipwa mshahara wa 19,125,000
Anakosaje uwezo wa kuchanganua kipi ni kipi kwake mpaka aulize jf .... nawaza tu wakuu
Umewaza kama mimi. Mtu mwenye kulipwa huu mshahara bila shaka ni mtu mwenye upeo wa kuchambua mambo hasa maisha yake na familia yake. Mimi nimeona kwa angle nyingine. Je, anajiandalia mazingira ya kuombwa connection ili apige watu? Kwanza mashirika mengi huwa wanalipa mishahara kulingana na hali ya maisha ya nchi husika.
 
Asante kwa mawazo yako mkuu.
 
Mm naona baki hapa mkuu hiyo pesa kwa USA ni ndogo,maisha ya kule jumulisha na bills utajampa upepo na kwambia, kwa huku hiyo hela ni nyingi sana. Kwa huku uta jimwambafai sana tu.
 
Kufikia hapa sasa nashauri uzi huu ufungwe na maoni yasiendelee.
 
Ni shirika gani CHAI (Clinton Health Access Initiative) au lipi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…