Habari wakuu,
Nahitaji ushauri kidogo hapa. Nimepata kazi ambayo inaniruhusu kufanyia kazi popote pale, na hata kuhamia yalipo makao makuu ya shirika kama nikitaka (Houston, Texas, USA), lakini pia nikitaka naweza kubaki hapa hata Tanzania nikaendelea kufanya kazi remotely, nikawa naenda USA mara mbili tu kwa mwaka. Nikiamua kuhamia USA, maana yake wako tayari kuni sponsor VISA ya H-1B.
The tricky part ni kwamba mshahara ni ule ule, vyovyote vile nitakavyoamua. Jiji ambalo makao makuu ya jamaa yapo ni Houston, jimbo la Texas. Mimi nina familia ya mke na watoto wawili, ofa yao ya mshahara ni USD 7,500 kwa mwezi. Wamenipa muda wa wiki mbili nifanye maamuzi kisha niwaatarifu ili waandae mkataba wangu kulingana na maamuzi nitakayokuwa nimeyafanya.
Kufanya kazi na kuishi USA kiujumla limekuwa ni jambo ambalo nimelitamani sana kwa muda mrefu kusema ukweli, shida ni hapo kwenye maslahi naona kuhamia USA with the same income ambayo naweza pia ipata kwa kubaki hapa bongo ni kama nitakuwa nimerudi nyuma sana, kwa sababu USD 7,500 kwa maisha ya Marekani sio pesa nyingi kihivyo, kulinganisha na bongo ambako unaishi ki-don kweli kweli kwa hiyo pesa.
Najua humu JF kuna wazoefu wa kuishi USA, na pia kuna watu wana exposure za kutosha kiujumla, nikaona sio mbaya nikaja hapa kuomba ushauri.