Nimepata kazi ambayo inaniruhusu kuhamia USA nikitaka, lakini mshahara ni ule ule popote nitakapoamua kufanyia kazi

Hiyo USD 7500 ni NET; Yaani baada ya makato ya kodi, bima ya afya, pension; ninachobaki mkononi ndio hiyo amount mkuu, sio GROSS.
Chance ndoto
 
Ni kweli kabisa mkuu, yaani kichwa kinawaka moto balaa. Asante sana kwa ushauri mzuri, uko sahihi sana.
 
Watu kama hao unawafunga mdomo unatupia ka visa hako ulichosema.

Hiyo ana stress ajala, umeme hakuna, joto na mafuriko kwa pamoja. Akili jaiwezi kuwa sawa
Wala sijishughulishi nao mkuu, acha kila mtu aamini anachotaka kuamini tu. Huwezi ridhisha mtu wa nyuma ya keyboard, hata hamfahamiani, sijui anatype akiwa wapi, tabia zake, na kadhalika.
 
Acha uzwazwa kijana na ulimbukenii wa kijingaa.... hizo dola 7500 ni mil 15 kibongoo komaa hapa uishii kama upo peponiii..
 
Akazae watoto huko huko na kufanya hayo yote.
Mkuu watoto wa kuzalia USA na wakakulia USA ni tofauti kabisa na watoto wanaozaliwa Tanzania na kupelekwa USA kwa kila kitu akili mpka matendo.
Mtoto alie maliza la saba Tanzania ukimpeleka shule za USA anaweza wakimbiza kwa masomo vibaya sana.
 
Bado marekani usiende ww.
Kuna vitu vingi sana bado hujavielewa kwenye mshahara wa marekani. Kwa maelezo yako. Usiende. Kama kuna kazi fanya hapa hapa.
Asante sana kwa ushauri wako. Ni kweli, kuna vitu vingi sijui bado kuhusiana na maisha ya Marekani, ikiwepo hayo masuala ya makato ya mishahara, gharama za maisha, na kadhalika; nina taarifa limited kuhusiana na mambo mengi ya huko, ndio maana pia nikaleta hapa maana najua JF ni jungu kuu, kuna watu wana exposure za kutosha juu ya maisha ya huko. Kwa hiyo, nitafurahi zaidi pia kama uki share hapa zaidi kuhusu masuala ya maisha ya huko. Chance ndoto
 
Acha uzwazwa kijana na ulimbukenii wa kijingaa.... hizo dola 7500 ni mil 15 kibongoo komaa hapa uishii kama upo peponiii..
Ni zaidi ya milioni 19 to be precise. Nakushauri pia utumie lugha ya staha katika ushauri wako mkuu. Asante pia kwa ushauri, nimelichukua.
 

Naomba uangalie hilo jedwari. Na nikushauri tena. Ungekua mwanafunzi ningesema hela hyo inakutosha. Ila kwasbabu una familia huku. Pambana bongo kwanza then baadae utaenda huko. Maana utahitaji walau 68,000$ ili uishi maisha favourable.
Umetaja Houston. Patakufaa ila kusanya kwanza hela. Au kama una mpunga nenda. Or else utaenda kuishi kama unajitafuta na inaweza kukucost zaidi. Angalia jedwali kwa maswali zaidi nitag.
 
Shukrani sana mkuu. Nimeangalia na gharama za nyumba, seems kwa Houston na Texas in general is relativelly cheaper compared na states zingine. Chance ndoto
 
Kula sana huwa siyo vizuri. Unatakiwa kula sababu mwili unauhitaji, siyo unakula kwasababu tu chakula kipo na unakula had kiishe. Just kula responsibly.
 
Usd 7500 sio pesa ndogo hata USA, maana hapo una kazi ya karibia dola 40 kwa saa which is very nice hata marekani, kapige kazi mzazi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…