Nimepata kazi ambayo inaniruhusu kuhamia USA nikitaka, lakini mshahara ni ule ule popote nitakapoamua kufanyia kazi

Habari wakuu.
Nahitaji ushauri kidogo hapa. Nimepata kazi ambayo inaniruhusu kufanyia kazi popote pale, na hata kuhamia yalipo makao makuu ya shirika kama nikitaka (Houston, Texas, USA), lakini pia nikitaka naweza kubaki hapa hata Tanzania nikaendelea kufanya kazi remotely, nikawa naenda USA mara mbili tu kwa mwaka. Nikiamua kuhamia USA, maana yake wako tayari kuni sponsor VISA ya H-1B.

The tricky part ni kwamba mshahara ni ule ule, vyovyote vile nitakavyoamua. Jiji ambalo makao makuu ya jamaa yapo ni Houston, jimbo la Texas. Mimi nina familia ya mke na watoto wawili, ofa yao ya mshahara ni USD 7,500 kwa mwezi. Wamenipa muda wa wiki mbili nifanye maamuzi kisha niwaatarifu ili waandae mkataba wangu kulingana na maamuzi nitakayokuwa nimeyafanya.

Kufanya kazi na kuishi USA kiujumla limekuwa ni jambo ambalo nimelitamani sana kwa muda mrefu kusema ukweli, shida ni hapo kwenye maslahi naona kuhamia USA with the same income ambayo naweza pia ipata kwa kubaki hapa bongo ni kama nitakuwa nimerudi nyuma sana, kwa sababu USD 7,500 kwa maisha ya Marekani sio pesa nyingi kihivyo, kulinganisha na bongo ambako unaishi ki-don kweli kweli kwa hiyo pesa.

Najua humu JF kuna wazoefu wa kuishi USA, na pia kuna watu wana exposure za kutosha kiujumla, nikaona sio mbaya nikaja hapa kuomba ushauri.
Nakushauri uende ili familia nzima mpate fursa za huko.

Sent from my moto g 5G (2022) using JamiiForums mobile app
 
Hakuna shirika lenye kujielewa wakatoa same salary scale kwa mtu anakaa bongo na mwingine Texas us ukizingatia tofauti kubwa ya gharama za maisha
Sawa, ni mawazo yako pia.
Ila hawa wao ni kwamba they dont require you kuwa USA ili kuifanya kazi,so you do not have to relocate. Nadhani ndio maana iko hivyo.
 
Aisee [emoji119][emoji119]

Parefu mno kwa maisha ya kibongo,

Natamani nikushauri ubaki Bongo ule mema ya nchi,
Ila no way Go to USA kwasababu ya future ya Generation yako na kupave a way ya fursa zaidi,
Ili ufanikiwi sometimes inabidi ufanye maamuzi ambayo wengine watahisi umechanganyikiwa,
 
Kuna mshenzi mmoja tuko chuoni alitulaghai bana akasema atatuajiri Barric gold mine North Mara...yani tuliwehuka..huo mshahara aliotutajia ni interms of dollars tukataka tuache na chuo...mhh badae tunajiuliza mshahara wote huu ni sisi au? Na barua yenye nembo ya barick zikatumwa kwny simu zetu sijui yule alikua IT mpk leo nawaza..ila akasema kuna kiasi tutatakiwa tutoe...ndo akili ikaja kuuliza uliza tukaambiwa mtaliwa hela na nyie wenyewe mtaliwa..tuka escape from sorbibo
 
Habari wakuu.
Nahitaji ushauri kidogo hapa. Nimepata kazi ambayo inaniruhusu kufanyia kazi popote pale, na hata kuhamia yalipo makao makuu ya shirika kama nikitaka (Houston, Texas, USA), lakini pia nikitaka naweza kubaki hapa hata Tanzania nikaendelea kufanya kazi remotely, nikawa naenda USA mara mbili tu kwa mwaka. Nikiamua kuhamia USA, maana yake wako tayari kuni sponsor VISA ya H-1B.

The tricky part ni kwamba mshahara ni ule ule, vyovyote vile nitakavyoamua. Jiji ambalo makao makuu ya jamaa yapo ni Houston, jimbo la Texas. Mimi nina familia ya mke na watoto wawili, ofa yao ya mshahara ni USD 7,500 kwa mwezi. Wamenipa muda wa wiki mbili nifanye maamuzi kisha niwaatarifu ili waandae mkataba wangu kulingana na maamuzi nitakayokuwa nimeyafanya.

Kufanya kazi na kuishi USA kiujumla limekuwa ni jambo ambalo nimelitamani sana kwa muda mrefu kusema ukweli, shida ni hapo kwenye maslahi naona kuhamia USA with the same income ambayo naweza pia ipata kwa kubaki hapa bongo ni kama nitakuwa nimerudi nyuma sana, kwa sababu USD 7,500 kwa maisha ya Marekani sio pesa nyingi kihivyo, kulinganisha na bongo ambako unaishi ki-don kweli kweli kwa hiyo pesa.

Najua humu JF kuna wazoefu wa kuishi USA, na pia kuna watu wana exposure za kutosha kiujumla, nikaona sio mbaya nikaja hapa kuomba ushauri.
Naona umetaka ushauri na mwisho umeishia kujijibu mwenyewe, anyway gharama za maisha USA ni kubwa kuliko bongo, unless unataka kuishi maisha ya marekani regardless ya hayo hapo juu. Lakini kama unataka kufanya savings na maendeleo maana kipato ni kilekile basi Tanzania panabakia kuwa chaguo sahihi.

Kila la kher
 
Back
Top Bottom