Nimepata kazi ambayo inaniruhusu kuhamia USA nikitaka, lakini mshahara ni ule ule popote nitakapoamua kufanyia kazi

Nimepata kazi ambayo inaniruhusu kuhamia USA nikitaka, lakini mshahara ni ule ule popote nitakapoamua kufanyia kazi

Sasa mkuu ukibaki bongo baada ya miezi kadha wakavunja mkataba utafanya nini? Bora uende usa hata mkataba ukiisha ukiisha bado utapata kazi tuu kwasababu elimu unayo and am sure hata wife akifika atapata kazi tuu mtasaidiana bills mbali mbali, mkuu yani unajiuliza mara mbili issue kama hiyo? Mamillion ya waafrica wanapambana kwenda usa kila mwaka wewe umepata fursa unachezea? Nakuhakikishia ukiamua kubaki bongo ipo siku utajilaumu maisha yako yote, nenda na ukomae upate permanent resident. Twende mkuu mimi niwe mfanyakazi wako wa ndani.
 
Sio scammers mkuu, hawa ni watu very legitimate, nimejiridhisha na hilo asilimia 100. Ondoa hofu.
Kama umejirizisha, ushauri wangu mimi na kwa uzoefu wangu, hiyo pesa kwa US unapiga life poa kabisa. Majority wanachoingiza ni kuanzia US$2,500 hadi US$4500 kwa mwezi, hivyo kulazimika kuwa na multiple Jobs ili kuongeza vipato na kumudu bills, of which na wewe itabidi utafute mishe za ziada.

Ukiongozana na shemeji, yeye pia unamfanyia mchakato apate vibali, anakuwa anapiga mishe kadhaa, ma wewe unatafuta kazi za ziada. Mnaweza kujikuta kwa mwezi mmetengeneza si chini ya US$13,000, ambacho ni kipato cha kima cha kati ya cha juu na cha kati, hadi hapo mnazidi kuwa well off financially. Hapo mnakuwa mpo vyema mno.
Hiyo ni fursa, sikushauri eti uje kuishi huku vikindu.
 
Sasa mkuu ukibaki bongo baada ya miezi kadha wakavunja mkataba utafanya nini? Bora uende usa hata mkataba ukiisha ukiisha bado utapata kazi tuu kwasababu elimu unayo and am sure hata wife akifika atapata kazi tuu mtasaidiana bills mbali mbali, mkuu yani unajiuliza mara mbili issue kama hiyo? Mamillion ya waafrica wanapambana kwenda usa kila mwaka wewe umepata fursa unachezea? Nakuhakikishia ukiamua kubaki bongo ipo siku utajilaumu maisha yako yote, nenda na ukomae upate permanent resident. Twende mkuu mimi niwe mfanyakazi wako wa ndani.
Asante kwa ushauri mkuu. Ila mkataba wanatoa wa mwaka mwaka, popote pale utakapoamua kufanyia kazi.
 
Kama umejirizisha, ushauri wangu mimi na kwa uzoefu wangu, hiyo pesa kwa US unapiga life poa kabisa. Majority wanachoingiza ni kuanzia US$2,500 hadi US$4500 kwa mwezi, hivyo kulazimika kuwa na multiple Jobs ili kuongeza vipato na kumudu bills, of which na wewe itabidi utafute mishe za ziada.

Ukiongozana na shemeji, yeye pia unamfanyia mchakato apate vibali, anakuwa anapiga mishe kadhaa, mnazidi kuwa well off financial. Hapo mnakuwa mpo vyema mno.
Hiyo ni fursa, sikushauri eti uje kuishi huku vikindu.
Asante sana mkuu kwa ushauri mzuri.
 
Habari wakuu,

Nahitaji ushauri kidogo hapa. Nimepata kazi ambayo inaniruhusu kufanyia kazi popote pale, na hata kuhamia yalipo makao makuu ya shirika kama nikitaka (Houston, Texas, USA), lakini pia nikitaka naweza kubaki hapa hata Tanzania nikaendelea kufanya kazi remotely, nikawa naenda USA mara mbili tu kwa mwaka. Nikiamua kuhamia USA, maana yake wako tayari kuni sponsor VISA ya H-1B.

The tricky part ni kwamba mshahara ni ule ule, vyovyote vile nitakavyoamua. Jiji ambalo makao makuu ya jamaa yapo ni Houston, jimbo la Texas. Mimi nina familia ya mke na watoto wawili, ofa yao ya mshahara ni USD 7,500 kwa mwezi. Wamenipa muda wa wiki mbili nifanye maamuzi kisha niwaatarifu ili waandae mkataba wangu kulingana na maamuzi nitakayokuwa nimeyafanya.

Kufanya kazi na kuishi USA kiujumla limekuwa ni jambo ambalo nimelitamani sana kwa muda mrefu kusema ukweli, shida ni hapo kwenye maslahi naona kuhamia USA with the same income ambayo naweza pia ipata kwa kubaki hapa bongo ni kama nitakuwa nimerudi nyuma sana, kwa sababu USD 7,500 kwa maisha ya Marekani sio pesa nyingi kihivyo, kulinganisha na bongo ambako unaishi ki-don kweli kweli kwa hiyo pesa.

Najua humu JF kuna wazoefu wa kuishi USA, na pia kuna watu wana exposure za kutosha kiujumla, nikaona sio mbaya nikaja hapa kuomba ushauri.
Kama ni kweli basi baki bongo,
Tandale (mfano tu + joke) unaweza kupata chumba hata Cha 30,000/- maisha yakasonga but "Mamtoni" hiyo sahau. Hata mlo mmoja wa siku unalipa kidogo ki bongo bongo zaidi kuliko huko

Yaani kama mshahara ni constant basi mostly likely uta save zaidi ukiwa Tanzania kuliko ukiishi USA sababu ya living cost za kule kua juu zadi kuliko za hapa bongo.

Ila kama wewe kipaumbele chako sio saving wala anything relating to money bas kakae tu "Mamtoni/Majuu" ufurahie mema ya dunia.

Ila kama huko kuna uwezekano wa kupiga mishe zaidi ya moja bas bora huko. Sifahamu kwenye working hours kama zinalingana between Dar na USA Kwa hiyo kazi yako.

Ila hii yote inategemea pia kama issue yako ni ya kweli ama sound.
 
View attachment 2881703
Naomba uangalie hilo jedwari. Na nikushauri tena. Ungekua mwanafunzi ningesema hela hyo inakutosha. Ila kwasbabu una familia huku. Pambana bongo kwanza then baadae utaenda huko. Maana utahitaji walau 68,000$ ili uishi maisha favourable.
Umetaja Houston. Patakufaa ila kusanya kwanza hela. Au kama una mpunga nenda. Or else utaenda kuishi kama unajitafuta na inaweza kukucost zaidi. Angalia jedwali kwa maswali zaidi nitag.
Wabongo acheni uoga watu wanaenda america hawana hata hiyo Dola 7000 Kwa mwezi na wanatusua life kama Kawa sembuse huyo monthly salary ya Dola 7000.

Roma makatoliki Yuko Marekani anabeba box na Wala hataki kurudi bongo na ameshamaliza nyumba yake Iko bagamoyo.

Kweli wabongo nuksi!

Mleta mada Nenda Kwa Biden huku Africa unaishi mwaka 2024 umeme unakatwa mara mwigulu anakufokea uende Burundi tabu tupu.mara nchi Haina sukari si ni aibu hii. Halafu wewe unapata muda wa kutoka nje ya nchi unajiuliza mara mbili mbili mjinga wewe ( samahani ni hasira )

Unapenda ishi sehemu muda WOWOTE mtoto anagongwa na bodaboda au sio
 
Tumemshauri kwasababu ana chance ya kupiga kazi bongo. Ndio maana tumempa draft ndugu.
Watu wanaenda kule na nauli na makbrasha tu na milioni mbili na wanaishi. Sembuse 14 molly.
 
Hongera sana mkuu. Binafsi sina uzoefu wowote na mbele na sina cha kushauri. Ila ikikupendeza unaweza pia kuja kushare nasisi jinsi ya kupata fursa kama hizo. Hatua uliyopiga wewe wengine tupo nyuma ya hapo hivyo tunatamani fursa kama hiyo.
Mi nikutakie heri tu.
 
Kwa takwimu za US Bureau of Labour and Statistics average annual salary Kwa US ni Dola 50,000 Hadi 70,000 sawa sawa na kama Dola 27-30 Kwa saa.

Wewe raia kutoka Africa unapewa hiyo offer unajiuliza mara 2 mbili
 
Wastani wa Mshahara kwa US ni $6,000,
Huo Mshahara ni Mzuri kabisaa, kama wao wenyeji inawatosha na wamarekani wanavyopenda bata, kwa wewe mtafutaji hio inakupush sanaa..

Sikatai kua gharama ni kubwa, insurance za kutosha, kodi n.k, ila kama wao wanachezea humu humo, means, wewe pia Inakuvusha, possibly ukawa unapata exta time kufanya vifurushi vingine vya kukuingizia kipato..

Kuna mshkaji alikua anafanya kazi ya 500k sehemu serikalini, akapata zali kama hilo, akaandika barua ya likizo ya miaka mi 3 bila malipo akasepa, Salary yake ilikua chini ya hapo, ila alikua anasave pakubwa, na nje ya hapo mtaani anapiga madili yanayompa zaidi ya Salary, Asaivi kabakiza miezi mkataba ukate, hana mpango na Futuhi.

US ukipata Uhalali wa kwenda tuu hilo linatosha kama ni mpambanaji.
 
Kama ni kweli basi baki bongo,
Tandale (mfano tu + joke) unaweza kupata chumba hata Cha 30,000/- maisha yakasonga but "Mamtoni" hiyo sahau. Hata mlo mmoja wa siku unalipa kidogo ki bongo bongo zaidi kuliko huko

Yaani kama mshahara ni constant basi mostly likely uta save zaidi ukiwa Tanzania kuliko ukiishi USA sababu ya living cost za kule kua juu zadi kuliko za hapa bongo.

Ila kama wewe kipaumbele chako sio saving wala anything relating to money bas kakae tu "Mamtoni/Majuu" ufurahie mema ya dunia.

Ila kama huko kuna uwezekano wa kupiga mishe zaidi ya moja bas bora huko. Sifahamu kwenye working hours kama zinalingana between Dar na USA Kwa hiyo kazi yako.

Ila hii yote inategemea pia kama issue yako ni ya kweli ama sound.
Asante sana kwa ushauri mzuri. Working hours ni the same bila kujali location (40 hrs per week).
 
Hongera sana mkuu. Binafsi sina uzoefu wowote na mbele na sina cha kushauri. Ila ikikupendeza unaweza pia kuja kushare nasisi jinsi ya kupata fursa kama hizo. Hatua uliyopiga wewe wengine tupo nyuma ya hapo hivyo tunatamani fursa kama hiyo.
Mi nikutakie heri tu.
Sawa mkuu, nitafanya hivyo ku share ili kuwafungua zaidi vijana. Japokua vijana wetu wengi wamejaa negativity, hata hapa jukwaani nadhani unaona. But nita share, anyways.
 
Hapa unatiwa moyo na kukatishwa tamaa kwa pamoja.Vyovyote vile wewe ndio mwenye uamuzi wa mwisho.
Yes, naona ushauri mbalimbali, napokea wote na kuuchakata kwenye halamshauri ya kichwa changu, mwisho wa siku nitafanya uamuzi.
 
Wastani wa Mshahara kwa US ni $6,000,
Huo Mshahara ni Mzuri kabisaa, kama wao wenyeji inawatosha na wamarekani wanavyopenda bata, kwa wewe mtafutaji hio inakupush sanaa..

Sikatai kua gharama ni kubwa, insurance za kutosha, kodi n.k, ila kama wao wanachezea humu humo, means, wewe pia Inakuvusha, possibly ukawa unapata exta time kufanya vifurushi vingine vya kukuingizia kipato..

Kuna mshkaji alikua anafanya kazi ya 500k sehemu serikalini, akapata zali kama hilo, akaandika barua ya likizo ya miaka mi 3 bila malipo akasepa, Salary yake ilikua chini ya hapo, ila alikua anasave pakubwa, na nje ya hapo mtaani anapiga madili yanayompa zaidi ya Salary, Asaivi kabakiza miezi mkataba ukate, hana mpango na Futuhi.

US ukipata Uhalali wa kwenda tuu hilo linatosha kama ni mpambanaji.
Nimekuelewa mkuu, n asante sana. Nitafanyia kazi ushauri.
 
Back
Top Bottom