Nimepata matatizo lakini hakuna Ndugu yangu aliyekuja wala kupiga Simu ya pole

Nimepata matatizo lakini hakuna Ndugu yangu aliyekuja wala kupiga Simu ya pole

Katika maisha ya sasa nilivyojifunza watu wenye uchungu na watakaokuwa sambamba na wewe kwenye shida na raha ni wazazi wako,watoto wako na mkeo hao wengine tunaowaita ndugu usiwategemee hata kidogo watakuwa karibu na wewe pale wanapo hitaji kitu fulani kama wanachotaka wanaona huna hutawaona hata simu zao hutaziona na hata ukiwapigia hawapatikani,walinifungia vioo wakati nimeacha mishe zangu na kwenda chuo miaka wengine wakani block kabisa,sitaki ujinga na mtu kila mtu aishi maisha yake.
 
Habari zenu? Kunakipindi nilileta uzi huu, Ndugu zangu nashindwa kuwaelewa

Baada ya kuvuta jiko niliishi na mke wangu, mwezi wa 11/2021 tulibahatika kupata mtoto na mke wangu, sikuwa na hiyana niliona japo ndugu zangu walinikosea kiasi fulani acha niwataarifu japo mke wangu alipata PPH (Postpartum Haemorrhage) nusura afe niliwataarifu pia kuhusu hayo matatizo lakini hawakujali na wala mke wangu hakupigiwa simu wala kuulizwa chochote.

Baadae nilisema isiwe kesi acha niendelee kutulia kimya nikaamua kutokuwatafuta tena, pia japo nilifiwa na baba niliandika kwenye uzi hiyo link juu, baada ya kutoka msibani hakukuwa na mtu aliyekuja kunipa pole hasa mama yangu mdogo wala wajomba zangu hakuna na wala eti waulizie kuhusu mtoto wangu anaendeleaje hakuna.

Baada ya kuona hivyo nilitulia tulii, juzi kati mamdogo wangu ananipigia na kunilazimisha nimpeleke mke wangu na mtoto wangu kwake, pia naambiwa mtoto wa mjomba anafunga ndoa mwaka huu hivyo nijiandae kirohoni nikajisemea hivi hawa wananichukuliaje?

Nimepata msiba hawajaja na baadhi yao hajanipigia simu kunipa pole, haya mke wangu alijifungua na akapata matatizo na niliwataarifu hakuna aliye toa pole na wala kujali.

Nawasilisha wakuu, hiyo ni sahihi?

Pia kuna mambo mengi tu sema siwezi andika Wakuu
Nanda kwenye kikao cha urusi baada ya kumaliza imba time useme ya Moyoni.. kukaa na kitu kifuani unaweza kuta nao walikuwa na shida zao pia
 
Back
Top Bottom