Habari zenu. Naombeni ushauri kwa ufupi.
Nimejifungua mwaka huu ila nimepata presha baada ya kujifungua nikavimba na kuumwa kifua sasa.
Hospitali moja wakasema nimepata tatizo la moyo wakanipa rufaa kwenda hospital kubwa lakini wanasema moyo upo salama japo mapigo ya moyo yanapiga sana na haraka, pia baadhi ya vipimo ECG ilisema Ischemia na Possible Heart Enlargement na echo EF 53-58 nna regurgitation ya valve Ila wanasema zipo sawa hazina shida.
Nipo kwenye dawa za presha so nawaza sana kwanini hospital nyingine waseme nina tatizo nyingine waseme sina?
Habari!
Kwanza nikupe pole kwa kuumwa na hongera kwa kupata mtoto.
Pili naomba uwe na utulivu kwenye wakati huu uliopo.
Kwenye kutoa huduma, wahudumu wa afya huweza kutoa mawazo yao kulingana na dalili pamoja na ukaguzi wanaoufanya kwenye mwili.
Kuna matatizo ambayo dalili zake huingiliana sana na ukizingatia na matumio kabla ya dalili.
Uthibitisho au kanusho la mawazo huweza kuja baada ya vipimo. Vipimo pia huweza kutofautiana kuweza kung'amua tatizo kulingana na mazingira tofauti:
1: Aina ya kipimo vs toleo lake.
2: Mpimaji husika
Kwa kadi ya tatizo linaloelezwa ni kweli dalili zake zinaweza kuleta mawazo mengi kwa mtoa huduma ya afya. Hii inatokana na mambo mengi yaliyokuwa yanakuzunguka.
Mfano:
1: Ujauzito
2: Valve prolapse
3: Presha
4: Mabadiliko ya ujazo wa damu
5: Mabadiliko ya vichocheo
6: Mabadiliko ya moyo kulingana na hali ya ujauzito
Mfano:
Kuwa mjamzito/ujazo wa damu kuongezeka/presha/ huweza kufanya hali ya valve peolape kuwa si njema/tatizo huzidi lakini hayo yote huweza kusababiaha moyo kutanuka/Dilated cardiomyopathy.
Hapo utapata dalili za :
1: kizunguzungu
2: kuchoka
3: moyo kwenda mbio
4: kifua kubana
5: maumivu ya kifua
Kupata presha baada ya kujifungua ni suala ambalo huweza kumtokea mama yeyote. Halijalishi tatizo lako la hapo kabla.
Valve prolapse pia huweza kuleta maumivu ya kifua kwani kunakuwa na ahida ya moyo kupata chakula na okaijeni ya kutosha.
Ili kuzingatia yote hapo juu ni ukweli kwamba uzingatifu mkubwa ni muhimu ili kujua mtihani kwa watoa huduma kwani kila kimoja hapo juu kina mchango wake kwenye hali unayojisikia.
Baada ya kujifungua Mabadiliko husika yaliyotokea wakati wa ujauzito nayo huondoka na kuufanya mwili kuyumba tena.
Bado kuna uwezekano mkubwa uwezo unaoonyeshwa na moyo kurejea vyema kama hayo hapo yote yakifanyiwa kazi vyema kulingana na uwezo unaouonyesha.
Kuna vitu utahitaji kuzingatia wakati wa tiba yako:
1: matumizi sahihi ya dawa zako
2: kuondoa wasiwasi
3: kupunguza matumizi ya chumvi
4: kutokutumia vinywaji kama kahawa, coca, pepsi
5: kutokukaa na njaa
6: kunywa maji ya kutosha
7: kutokufanya mazoezi/kazi za nguvu
8: hakikisha kiasi chako cha damu ni kizuri
NB: Cardiologist opinion/mawazo ni muhimu ili kuweka haya yote sawa.