Ndio mana mimi nitabakia niki kumbushia vijana wenzangu hembu tuache mishe za K tupige kazi kwanza. Mtoto wa 21 years na BRO wa 48 years alafu bro anataka mpangishia chumba bado hela ya matumizi ampe. Hivi kesho wewe msela huna misha bado za kueleweka umpende huyu mtoto kwa nia njema kabisa ya kutaka kuoa utawezana nae? Jibu ni No ata taka umtoe laki tano za matumizi kwa wiki kama bro na wewe huna kitu ina kuwa maumivu tayari.
Conclusion wanao haribu hawa kina dada ni MaBro. Bro ana ndoa ana mke ana watoto tena wanawez kuwa wakike bado kidem chetu mtaani ana kimiliki ana kipa hela kidem kina tudharau wakati uchumi wa kati umekaba hata ajira hamna. Sisi tuna endelea kudhalilika kila siku na wanawake wanasema no money no honey hela tuna toa wapi sisi, mfumo wa mapenzi ya kweli umeharibiwa na mabro na hela zenu mna taka kumiliki kila kitu na mabavu ya pesa zenu sisi wadogo tunaishi vipi? Ndio mana nawasihi wenzngu tuka pambane tu kwanza tutarudi baadae tukiwa kwenye maprado, teza, subenga na crown.