Nimepata Milioni 2 Biashara ya Chips naona ngumu, nawaza kuwekeza kwenye hisa

Nimepata Milioni 2 Biashara ya Chips naona ngumu, nawaza kuwekeza kwenye hisa

Utt kwa mwezi kwenye hiyo hela anapata 20k kwa mwezi kama faida,bado ni hasara!! Hiyo hela akinipa hata mimi kwa biashara zangu kw mwezi Nina uwezo wa kumpa 50k kama Faida huku namlindia mtaji wake

Badala akupe wewe kwanini usimwambie hizo biashara zako ili afanye mwenyewe apate faida nzuri zaidi na uwe umemkwamua mwanajukwaa?​
 
Sijui kijijini kwenu ni wapi lakini mimi ningefanya hivi;
1. Ningenunua mbuzi wadogo niwe na fuga kwa kumuajiri mtu najua kijijini hii sio ghali, kwa miaka miwili uwezekano wa kua na mbuzi wengi zaidi ni mkubwa.
2. Ningenunua pikipiki naitumia kwendea chuo na muda usio wa masomo nabeba abiria.
3. Stationery kwajili ya printing&copy karibu na chuo
 
Sasa si upumbavu huo miaka 3 ni 780,000 income ya interest katika miezi 36 yaani kuweka 2m ili upate 21k kwa mwezi ni uzwazwa. Nikumbia Uza chupi tuu
Mkuu jamaa yupo sahihi mbona
Screenshot_20260819_095559_Chrome.jpg
 
Hamjambo?

Kwenye harakati zangu za hapa na pale nimepata Milioni 2 ambayo sikuitegemea kama nitapata

Mimi ni mwanafunzi wa chuo na sijawahi kufanya biashara kabisa. Nimeshauriwa kuanzisha biashara ya chips hapa mtaani lakini naogopa sana kuanza biashara maana sijawahi kufanya na sijui hata nianzie wapi

Kuiweka benki hiyo hela, kama mnavyojua maisha ya kibongo, kidogo tu utasikia shangazi kaumwa anataka hela ya hospitali

Hivyo nimewaza kuipeleka huko kwenye hisa, zikatumike na CRDB na NMB then by the time na-graduate ntauza hizo hisa nifanye mambo mengine

Mnanishaurije?
Biashara ya chips ni nzuri lakini inatakiwa upate mtu mwaminifu kwenye mauzo,husije kumaliza chuo unakuta banda linaenda kufa halafu uliyemwachia ana mabanda mawili mitaa tofauti
 
Mchawi ni ROI =Return on investment, yaani hiyo tshs 2m unayotaka kuwekeza itachukua muda gani kurudi. kwa kawaida micro business ROI yake haizidi miezi 6 na hiyo ni kwa sbb haigharimu sana ktk fixed costs na mwekezaji anatumia nguvu na maarifa nyingi za kwake yeye mwenyewe sometimes atahusisha family members. Hisa nyingi ROI yake ni zaidi ya miaka 3, labda ukutane na hot IPO kama ile ya twiga cement
 
Sijui kijijini kwenu ni wapi lakini mimi ningefanya hivi;
1. Ningenunua mbuzi wadogo niwe na fuga kwa kumuajiri mtu najua kijijini hii sio ghali, kwa miaka miwili uwezekano wa kua na mbuzi wengi zaidi ni mkubwa.
2. Ningenunua pikipiki naitumia kwendea chuo na muda usio wa masomo nabeba abiria.
3. Stationery kwajili ya printing&copy karibu na chuo
Ushauri umeshiba.
 
Yeah hizi ndio ideas ambazo zinamfaa kwa mwanachuo biashara zingine zitamvuruga tu
 
Ukiiweka UTT bond fund utapata interest ya karibia 13% kwa mwaka. Kwa miaka mitatu utavuna ~1,000,000/= + 2,000,000/= utapata jumla 3m.

Ukiiweka M wekeza, interest rate ndiyo hiyo hiyo.
kwa nn umemshauri aweke bond fund na sio liquid fund?
 
kwa nn umemshauri aweke bond fund na sio liquid fund?
Hii inatokana na wapi UTT wanawekeza pesa za bond fund na liquid fund.

Bond fund huenda pesa zake zinatumika kununua hati fungani za serikali za muda mrefu ambazo zina faida kubwa.

Liquid fund pesa zake huenda zinawekezwa kwenye hisa za benki au makampuni ambazo faida yake siyo kubwa na siyo fixed.
 
Thanks, japo naona wengi wanaichangamkia liquid fund
 
Back
Top Bottom