Nimepata milioni 50, nifanyie biashara gani niwe milionea?

Nimepata milioni 50, nifanyie biashara gani niwe milionea?

Ushauri wangu kwako ndugu ni kwamba mimi naona kilimo cha viazi mviringo kinalipa na ni kizuri sana kwa kuwa kinachukua maxmum ya miez 4 lakini kawaida ni miez 3 kuvuna, na kiazi kina mahitaji makubwa sana sokoni na kwa mtumiaji wa mwisho pia...Kwa milion 50 unaweza kupata zaid ya milion 800 ikiwa unafanya kilimo kama kinavyotakiwa...Utaanza na kukod shamba la hekali 40 ambayo itakugharimu sh 60,000 kwa kila heka...Mbegu mpya ya kiazi ambacho hakina mabonde ni sh 100,000 kwa hekal moja ...Utanunua mashine za kumwagilia ambazo kwa makadilio itakughalimu sh milion 3 maximum ....Utanunua mbolea ambayo kila heka utanunua mbolea ambayo itakugharimu sh mil 6 kwa hekali 40 zote ...Utaweka vijana wa kulima ambao utaelewana nao kwa mazungumzo ya kawaida ambayo inaweza kukugharimu sh 400,000 maximum kwa hekali zote 40 ..ukipiga hesabu kwa ujumla utakuwa umetumia sh milion16 tu katika hiyo 50 uliyonayo..Na kiazi kwa hii mbegu mpya unatoa gunia 80-100 kwenye hekali moja...Kiazi kama hiki kisichokuwa na mabonde kina mahitaji makubwa sana sokoni na kikishuka bei kinauzwa 80,000 kwa gunia dar es salaam...Ndugu ukipiga kwa mahesabu ya haraka haraka unaweza kuvuna gunia 3,200 katika shamba la hekali 40 kwa msingi wa shiling milion 16 tu kati ya milion 50 ulizo nazo ...Na kama utauza kipind cha bei ya chini ya sh 80,000 kwa gunia utakuwa umejipatia tsh 256,000,000 ...ukitoa gharama za usafirishaji kutoka shamba hadi masoko ya dar es salaam itapungua hapo kidogo lakini haita affect hiyo figure ..May be 240,000,000... Huo ndo ushauri wangu ndugu na nina uhakika kabisa kama ukitumia kias chote cha sh mil 50 bas utapata faida zaid ya hiyo ambayo inaweza kufikia hadi milion 800...
Mkuu hiyo mbegu mpya ya kiazi ndo ipoje??
 
Kwa sasa sio kipingi kizuri kuwekeza Tanzania coz uchumi umeyumba. Hiyo biashara yako inaweza isikulipe kwa sasa... Bora tu hiyo hela uendelee kuitunza tunza mpaka hapo 'utakapokuwa mkubwa'...
 
  • Thanks
Reactions: MC7
Unataka PM yako ijae mkuu? katika huo umri kama na kama kweli unaishi ufaransa exposure yako isingekufanya ulete hili bandiko kama kweli ume BAHATIKA kupata huo mpunga?...
We ndio umeongea pumba kabisa umri na exposure inasaidia nini kuwa wazo la kufanya na pesa mtu alizopata...? Hapa kusema kweli sijakuelewa we unadhani kuwa Ufaransa na hiyo "exposure" ndio kujua kila kitu..? Kama huna cha kunyangia ukaa kimya kuacha wengine wamsaidie dogo unaona haitoshi..? Hebu watu wenye akili zao wampe mawazo dogo.
 
Mkuu ushauri wangu fungua office ndogo ya kukopa yani uwe unakopesha watu pesa nina mfano wa jirani yangu mmoja amefungua office kama hiyo yeye anakupa laki moja basi unarejesha laki moja na elfu 15 kwa mwezi mmoja na ukitaka kwa miezi miwili basi utarejesha laki 1 na 30. Yani mkopo wake hauvuki miezi miezi mi 3 kila kwenye laki moja basi kuna riba ya elfu 15 na watu wanakwenda wengi sana kwa sababu ni mkopo wa haraka japo unariba kubwa ukizingatia na kipindi hiki kigumu watu hali ya uchumi sio nzuri hivyo wanahaha sana kutafuta hela nadhani hii itakuwa ni biashara nzuri sana kwako na itakufanya uwe milionea mapema sana. Asante mkuu
 
We ndio umeongea pumba kabisa umri na exposure inasaidia nini kuwa wazo la kufanya na pesa mtu alizopata...? Hapa kusema kweli sijakuelewa we unadhani kuwa Ufaransa na hiyo "exposure" ndio kujua kila kitu..? Kama huna cha kunyangia ukaa kimya kuacha wengine wamsaidie dogo unaona haitoshi..? Hebu watu wenye akili zao wampe mawazo dogo.

The good thing umesema haujanielewa, una haki ya kukiita pumba au chochote nilichokipost.
 
Njoo chemba utashangaa. Pesa ninazo.kazi nzuri kubwa na cheo kikubwa na kampuni kubwa vinafanya kazi.
Hofu ya Mungu ndo mpango mzima.
Mkuu kwa majibu haya umenifanya nipate uchu wa kujiajiri
 
That was my advice. Take it or leave it.
Matajiri wengi wakubwa duniani wameanza na mtaji mdogo sana, Mdogo ambao labda hata Million haufiki. Wewe unasema 50 M ni ndogo??

Wewe utakuwa mbabaishaji tu..
 
  • Thanks
Reactions: MC7
kama mpaka unapata hizo 50M hukuwa na wazo la kuinvest, wewe sio mfanyabiashara tena!
achana na wazo la kuziinvest tafuta kibanda tu ununue au ujenge, ili akili yako yoote iendelee kutafuta 100M kwa kutumia njia uliyotumia kuzipata hizo 50M.
 
Kivipi mkuu kwenye hili suala.?
Wanaokushauri kununua gari sijui coaster au daladala wanataka kukuongezea pressure bure maana hujui uko barabarani kitatokea nini na hawa madereva wetu. Maana dereva hasiposababisha wengine wanaweza kumsababishia ajari na ukaishia kuwa na scrapers. Kilimo ndgu yangu yataka moyo maana unategemea Baraka za mwenyezi Mungu ili mvua inyeshe na wapi utapata mashamba. nayo ni pressure nyingine na pia hata ukilima je soko unalo? ili kuuza madalali wanajua kucheza na mkulima na kujua jinsi ya kumlalia na kuishia umepata hasara na mwaka huu tumeshuudia watu wamelima nyanya zimeishia kuozea shambani. Nyumba nayo biashara yake ni kizungumkuti maana utegemee hela za mpangaji kila mwezi kurudisha mtaji wako ni kizungu mkuti. Labda ujenge Guest nzuri kidogo italipa lakini gharama zake si 50m.
Kidogo labda aliyesema ufugaji wa samaki na kuku japo sina experience nao.
Biashara mpaka uwe na uhakika wa shindano la soko
 
Labda udoble huo mtaji. Biashara nyingi hapa Tz ni zaidi ya milioni hamsini na zinaonekana kawaida tu.
 
Kapande Miti ya Mbao baada ya hiyo miaka 10 utaanza kuvuna
 
Ukiwa na mil50 wewe sio milionea...Milionea maana yake unatakiwa uwe na pesa kuanzia bilion...
Nitakupa mfano mdogo..Mwenye milion 50 mana yake hana milion 100 ...ukiwa milionea unatakiwa uwe na kiasi cha pesa chochote kinacho tamkwa milion kadhaa..


Mnasikitisha sana. Billion ni Billionea.

Hivi hizo shule mlienda kusomea ujinga?
 
Back
Top Bottom