Nimepata milioni 50, nifanyie biashara gani niwe milionea?

Kaka kuna biashara ya mazao inalipa sana, hii biashara huwa inaanzia mwenzi wa tatu, kwa mtaji kama wako ndan ya mwaka mmoja unapata faida milion 50, pia kuna fulsa nyingine.
 
Kaka kuna biashara ya mazao inalipa sana, hii biashara huwa inaanzia mwenzi wa tatu, kwa mtaji kama wako ndan ya mwaka mmoja unapata faida milion 50, pia kuna fulsa nyingine.
maelezi zaidi mdau
 
Njia ulio tumia kuipata hiyo million 50, ukiwa na miaka 25, ongeza ubunifu thru njia hiyo hiyo utapata nyingine nyungi.

Hongera mm nipo hapa ni above 30 hata pikpik sina.
Watu wengi naona mnamshauri aendelee kutumia njia aliyotumia kupata hiyo Pesa ili iongezeke je Kama aliiba akaibe tena...!?
 
It will take time and experience doing that. It's not an easy thing.
Nnaelewa hilo na kwa sasa nnajitahidi kusoma soma kidogo nipate walau uelewa... Ila kama kuna shortcut ya kupata ufahamu zaidi wa hiyo kitu ningefurahi zaidi
 
Biashara za magari usifanye. Angalia kilimo na ufugaji, lkn fuatilia masoko kwanza
 
Kila biashara ina changamoto zake usiziweke zote kwenye biashara utafirisika sababu hauna uzoefu
 
Kwa hali iliyopo Tanzania kwa sasa sidhani kama mil.50 itafua dafu kukupa umilionea katika nchi inayoelekea kutangazwa mufilis yaani kufilisika kabisa kutokana na hali ya kiuchumi kudorora...mabenki mengi sasa hivi yanatangaza hasara...zaidi zaidi kwa chochote utakachoplan kukifanya bongo kitafail kwani wapo wajasiliamali wengi tu ambao tayar walikuwa kwenye system nzur ya kiuwekezaji na walikuwa wanapata faida zao vizur tu tena wenye mitaji mikubwa kuliko hata huo wa 50M lakini Leo wote wanalia hali mbaya
My take mkuu.....

Bila shaka unaonekana upo timamu sana kiutafutaji kupata dola 25 elf yaani hizo MIL50 tena ughaibuni pesa ambayo kuna wazungu wengi tu wana ndoto nayo na hawaipati....sasa....umeshapata exposure ya kutosha kwa kuishi ughaibuni tafuta ama buni biashara itakayokupa nafasi ya kusafirisha bidhaa kutoka Bongo zinazohitajika katika masoko ya ulaya na hususan ufaransa and vice versa....zipo bidhaa nyingi ambazo waweza kuanzia kwa mtaji ulionao na bado ukapata faida yako ukasave....kuna asali,dhahabu nk. bila shaka kwa hapo ufaransa lazima kuna bidhaa nyingi tu zinahitajika kutoka masoko ya Africa mathalani Tanzania etc,kwa hapo pesa yako na faida vitaenda pamoja na kwa uhakika zaidi....tofauti na hapo mkuu sikushauri hata kidogo kurudi kuwekeza bongo milioni 50 kwa jinsi hali ya uchumi tunavyoishuhudia inavyozidi kudidimia.....Labda uje uwekeze ununue kiwanja sehem nzur kwa pesa yote hiyo then ukae kusubir miaka kumi ili ukiuze kwa mili200-300....tofauti na hapo utakuja kuzamisha pesa yote uanze na moja,biashara imekuwa ngum bongo yahitaji umakini & uzoefu kwa pamoja kumaintain mtaji....ni hayo tuuu
 
Nnaelewa hilo na kwa sasa nnajitahidi kusoma soma kidogo nipate walau uelewa... Ila kama kuna shortcut ya kupata ufahamu zaidi wa hiyo kitu ningefurahi zaidi

Mambo ya pesa hayana shortcut ndugu. Soma sana na uanze mazoezi na demo account.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…