Nimepata milioni 50, nifanyie biashara gani niwe milionea?

Nimepata milioni 50, nifanyie biashara gani niwe milionea?

Mkuu naona ni typing Error hiyo na nadhani alimaanisha Biashara. Au unasemaje mkuu Nikuletee Anti-biotics nikuondoe kabisa? maana Plasmodium wepesi sana Kufa ila wabishi kinoma.
unamaanisha ana MALARIA iliyopanda kwa ubongo?
 
Kuna biashara fulani hv haiko open sana but ndani ya siku 35..hiyo pesa itakuwa X2 yan 100m nitafute kwa muda wako mkuu

Sent from my GT-I9500 using JamiiForums mobile app
 
Ushauri wangu kwako ndugu ni kwamba mimi naona kilimo cha viazi mviringo kinalipa na ni kizuri sana kwa kuwa kinachukua maxmum ya miez 4 lakini kawaida ni miez 3 kuvuna, na kiazi kina mahitaji makubwa sana sokoni na kwa mtumiaji wa mwisho pia...Kwa milion 50 unaweza kupata zaid ya milion 800 ikiwa unafanya kilimo kama kinavyotakiwa...Utaanza na kukod shamba la hekali 40 ambayo itakugharimu sh 60,000 kwa kila heka...Mbegu mpya ya kiazi ambacho hakina mabonde ni sh 100,000 kwa hekal moja ...Utanunua mashine za kumwagilia ambazo kwa makadilio itakughalimu sh milion 3 maximum ....Utanunua mbolea ambayo kila heka utanunua mbolea ambayo itakugharimu sh mil 6 kwa hekali 40 zote ...Utaweka vijana wa kulima ambao utaelewana nao kwa mazungumzo ya kawaida ambayo inaweza kukugharimu sh 400,000 maximum kwa hekali zote 40 ..ukipiga hesabu kwa ujumla utakuwa umetumia sh milion16 tu katika hiyo 50 uliyonayo..Na kiazi kwa hii mbegu mpya unatoa gunia 80-100 kwenye hekali moja...Kiazi kama hiki kisichokuwa na mabonde kina mahitaji makubwa sana sokoni na kikishuka bei kinauzwa 80,000 kwa gunia dar es salaam...Ndugu ukipiga kwa mahesabu ya haraka haraka unaweza kuvuna gunia 3,200 katika shamba la hekali 40 kwa msingi wa shiling milion 16 tu kati ya milion 50 ulizo nazo ...Na kama utauza kipind cha bei ya chini ya sh 80,000 kwa gunia utakuwa umejipatia tsh 256,000,000 ...ukitoa gharama za usafirishaji kutoka shamba hadi masoko ya dar es salaam itapungua hapo kidogo lakini haita affect hiyo figure ..May be 240,000,000... Huo ndo ushauri wangu ndugu na nina uhakika kabisa kama ukitumia kias chote cha sh mil 50 bas utapata faida zaid ya hiyo ambayo inaweza kufikia hadi milion 800...
Mzee unapatikana mkoa gan.tukutane pm tafadhali

Sent from my HUAWEI P7-L10 using JamiiForums mobile app
 
Heshima zenu wakuu.

Mimi ni kijana mwenye umri wa miaka 25, ni Mtanzania nnae ishi nchini ufaransa.

Nimebahatika kupata shillingi mil 50 za kitanzania na nahitaji kuwekeza nchini Tanzania.

Je ni fursa zipi nnazo weza kuzipata Tanzania kuweza ili kuimaximize hii pesa ili niweze kuwa Millionaire ndani ya miaka 10 kutoka sasa.?

Asanteni.
''You are already a Millionaire" Angalizo ukitaka kufanya biashara yoyote ile kitu cha kwanza lazima ujue vizuri hiyo biashara unayotaka kuifanya cha pili lazima uwe na andiko la Biashara "Business plan'' cha tatu ni jinsi utakavyo enenda kwenye biashara yako ''PECS (Personal entrepreneur characteristics) hizi ni tabia za mfanya biashara maarufu aliye fanikiwa ziko km 25 zinaweza kuongezeka kutokana na mabadiloko ya hii dunia
 
Mkuu inategemea upo katika mazingira yapi. Kama unataka kuwekeza Tanzania , utahitaji kupata muda uweze kuangalia biashara tofauti tofauti.

Wewe ingia kama muekezaji katika biashara zilizopo.. Maeneo yatakuwa ni tofauti tofauti .

Mfano, unaweza kuwekeza katika biashara ya logistic- lakini kama local courier --- ukutane wakuonyeshe business plan au ulewe toka kwao kama wanataka kupanua operation zao. Angalia zaidi wanaohitaji financing, halafu uingie nao mkataba fulani kuhusu malipo, endapo mnakubaliana unaweza kununua Suzuki carry za kusafirishia mzigo zaidi, au pikipiki ambazo zinaweza kutumika katika kusambaza mizigo ya wateja walio nao.

Eneo jingine ni biashara ya bima ...... hasa kwa watu ambao wana shida ya mtaji lakini wanahitaji kupanuka.

Maeneo hayo nimeyaongelea kutokana na uwezo wa kusimamia biashara ukiwa mbali na unaweza pata msimamizi wa wabia wako. Nafikiri unaweza kuchunguza maeneo hayo, kwa vile naamini hutaki kurudi Bongo kwa sasa .

Ukisharidhika unaweza kuweka vigezo vyako, halafu utawatafuta watu hao na mkafanya mazungumzo.

Ni hayo tu kwa sasa.
 
hizo pesa kwa haraka peleka police. uwaambie wakurudishe kwa riba.
 
wewe nakuona kama mtu mzalendo, njoo uwekeze nchini mkuu, kuna fursa nyingi, njoo, uwekeze kwenye lendingi mkuu, milioni 50, zinatosha au km huna experience nayo njoo ofisini kwetu tunaingia contract nzuri kutokana na fedha yako kila mwezi tunakulipa 10% ya mtaji wako, dheni after 24 month unarudishiwa fedha yako km ilivyo wakati huo ndani ya kipindi chote kila mwezi ulikuwa unakula 10% sisi tunafnya biashara ya lending mkuu kwa muda wa miaka7 sasa
mzee ofisi yenu iko wapi niwaletee zangu
 
Heshima zenu wakuu.

Mimi ni kijana mwenye umri wa miaka 25, ni Mtanzania nnae ishi nchini ufaransa.

Nimebahatika kupata shillingi mil 50 za kitanzania na nahitaji kuwekeza nchini Tanzania.

Je ni fursa zipi nnazo weza kuzipata Tanzania kuweza ili kuimaximize hii pesa ili niweze kuwa Millionaire ndani ya miaka 10 kutoka sasa.?

Asanteni.
Mil 50 umepataje? Biashara kwa maeneo gani? Sector gani? Wewe intrest yako ni nini? Hobby yako je? Wewe unahisi biashara ipi itakufanha uwe milionaire?

Sent from my Iphone 7 using JamiiForums mobile app
 
Heshima zenu wakuu.

Mimi ni kijana mwenye umri wa miaka 25, ni Mtanzania nnae ishi nchini ufaransa.

Nimebahatika kupata shillingi mil 50 za kitanzania na nahitaji kuwekeza nchini Tanzania.

Je ni fursa zipi nnazo weza kuzipata Tanzania kuweza ili kuimaximize hii pesa ili niweze kuwa Millionaire ndani ya miaka 10 kutoka sasa.?

Asanteni.
Tayari wewe ni milionea...koz unamiliki zaidi ya milioni.

Sent from my SM-A310F using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom