Kuanzia juzi, kuja mpaka jana, nilikuwa ninaonana na watu ambao macho yao ni kama yamevujia damu kwa ndani. Nilikuwa ninawatizama kwa kustaajabu sana, naishia kusema,"Mambo yao tuwaachie wao".
Usiku wa jana, mida ya saa 2 usiku, nalishangaa kuhisi macho yakiwasha sana, hivyo kuyapekecha vya kutosha. Ilipotimu usiku wa manane, nalihisi ni kama vile macho yamepatwa na vipele uchungu kwa ndani, maake sio kwa maumivu yale, nilihisi nimebebeshwa bichwa la Giant Man. Mida hii ya saa 12 nimeona wacha nivunje sheria ya uanaume, nikaamua kwenda kujitizama kwenye kioo. Alooo! Inatisha sana! Nimekutana na mucus za kutosha kuyazunguka macho yangu, hada hasa hili la kushoto. Baada ya kunawa kwa uhakika zaidi, nimebaki na RedMi kwenye macho, yaani kama nimetoka kilingeni kujifukiza kwa dk. Mshana Jr
Nimepoteza muonekano na pia napitia hali ngumu sana. Msaada!