Nimepeleka mahari unyamwezini

GANG MO

JF-Expert Member
Joined
Dec 6, 2016
Posts
2,092
Reaction score
2,210
Wadau heri ya Christmas. Last week nimejifungasha toka Iringa mpaka Tabora wilaya ya nzega kumuoa binti ambaye nimempenda sana.

Nilifurahia sana namna walivyotupokea na namna mchakato ulivyofanyika fasta bila complication nyingi. Kwanza mfumo wa upokeaji mahari wa hawa jamaa ulinishangaza. Watu hawakuwa wengi ni ndugu wachache na majiran kadhaa tu.

Nilipangiwa mahari milioni 2.5 lakini wale watu ni waelewa mno tulipo bagain wakatuelewa na kufika 1.5m. ulipofika muda wa kutoa pesa tukatakiwa kuiweka kwenye hii sahani yenye majani mawiliπŸ˜€. nimesahau wanaitaje. Hakika moyo wangu unafuraha sana.

Pongezi kwenu wanyamwezi. Nishakuwa ndugu yenu

 
Kuna kabila waleta posa hukaribishwa na nyanya chungu. Wanaamini zina baraka ya uzazi yaani mwanaume utatoa mbegu kama zilivyo kwenye nyanya chungu na mwanamke utazaa watoto kama mmea wa nyanya chungu.
 
Kuna kabila waleta posa hukaribishwa na nyanya chungu. Wanaamini zina baraka ya uzazi yaani mwanaume utatoa mbegu kama zilivyo kwenye nyanya chungu na mwanamke utazaa watoto kama mmea wa nyanya chungu.
Kabila gani hilo mdau?[emoji16]
 
Tabora Hoooyeeeeee....

Wanyamwezi hoooyeeeee.....

Jiandae kulishwa mapishi ya asali....
[emoji23][emoji23][emoji23] nijiandae pia kula mapalage
 
Yaani mahali umepunguziwa sikuhiyohiyo ukalipa au ni chai unadanganya?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…