Nimependwa na mke wa mtu lakini watu wananionea wivu

Nimependwa na mke wa mtu lakini watu wananionea wivu

Habari yako,

Sorry leo nipo hapa katika jukwaa hili naomba ushauri kuhusiana na hili ninalolileta kwako muda huu.

Naitwa Mr George Francis kwa jina maarufu. Kuna dada mmoja anaitwa Latipha niliwahi kusoma nae sekondari. Kipindi hicho tulikuwa na mahusiano lakini tulivyomaliza shule, mahusiano hayo yalipotelea hewani. Yeye alienda Dar es Salaam kwa mama yake, mimi nilibaki hapahapa Singida.

Latipha alizaliwa hapa Sigida lakini mama yake sio mzaliwa wa hapa. Ni mzaliwa wa Tanga lakini alikuja Singida kwasababu ya ndoa. Baba yake ndio Mnyaturu wa hapa. Baada ya kuachana, mama yake aliamua kwenda kujitafutia maisha yake huko Dar es Salaam.

Tangu hapo hatukuwahi kuonana tena kwa zaidi ya miaka kama nane hivi. Mimi sikuwaza kama kuna siku tutakuja kuonana, hata yeye hakuwahi kuwaza. Alikuwa ameamua kuondoka jumla kwasababu aliona ni heri akaishi na mama huko kutakuwa na raha kuliko kubaki na baba yake ambae alikuwa mlevi hana malezi mazuri kwa watoto, yupo bize na mambo yake.

Miaka kadhaa iliyopita, alipata mwanaume hukohuko Dar. Mwanaume huyo ni mwalimu wa shule ya msingi.

Mwaka wa jana mwanzoni mumewe alihamishiwa hapa Singida kikazi ndipo tulipokuja kuonana na Latipha kwa mala nyingine.

Nilijua amekuja tu kumsalimia baba yake kumbe ndio wamehamia jumla. Mimi nilikuwa sijui lakini aliniambia kuwa ameolewa na ana watoto wawili lakini bado ananipenda na miaka yote hiyo alikuwa ananifikiria sana lakini alijua tu labda nilishaoa, hivyo na yeye aliamua kuolewa.

Alivyoniambia kuwa ameolewa, mimi niliamua kumpotezea na kuendelea na maisha yangu. Lakini baada ya miezi michache alinitafuta mwenyewe akaniambia mumewe amebadirika hamuhudumii vizuri kama mwanzo. Siku hizi hamuachii pesa ya matumizi inayotoshereza kwa mahitaji.

Niliamua kumsaidia na kumpa pesa kila alipohitaji msaada wangu. Hata pesa za kubadilisha mavazi ili apendeze nilikuwa nampatia.

Siku moja, aliniambia amemisi penzi langu la zamani hivyo anaomba tukumbushie kidogo. Kusema ukweli sikumkatalia, nilifanya alivyotaka. Tangu hapo tukafufua ule upendo wetu wa zamani.

Nimejikuta nampenda sana Latipha kuliko mwanamke yoyote hapa duniani. Raha anazinipa sijawahi kuzipata popote maishani. Hatakama kwasasa ni mke wa mtu lakini nampenda sana, na yeye pia ananipenda sana. In short, mimi na Latipha tunapendana sana. Hivyo sijali hata kama ameolewa lakini mimi nipo tayari kusimama katika nafasi yangu kama mchepuko wake ninayempenda kwa dhati.

Lakini kuna watu wananionea wivu na kuanza kunitisha eti wanasema mume wake akijua itakuwa msala.

Sasa najiuliza iwe msala kivipi wakati mwanamke kanipenda mwenyewe?
Kwani kuna ubaya gani mimi kupendana na yeye?
Si ni haki yangu, kumpenda mtu yoyote?
Eti jamani? au wewe ndugu msomaji kwa upande wako hili unalionaje?
Naomba ushauri wako tafadhali."
-----------------------
It's me
Mr. George Francis
KWA SIMULIZI NZURI KAMA HII NA STORY KIBAO ZA KUSISIMUA JIUNGE NA GROUP LANGU LA SIMULIZI

JIUNGE HAPA [emoji116][emoji116]
..Kumbe ni Simulizi TU!
 
Uzuri ameshasema ni hadithi ya kutunga. Amefikisha ujumbe kwa wale wote wanaopatwa upofu wa mapenzi kwa kupenda wake za watu wanafurahia pasipo kuona hatari iliyo mbele yao. Hongera kwa utunzi wako.
 
vase.jpg
 
Kuna dogo kazini kwetu kakutwa na msala wa kungonoka na mke wa mtu, aisee kesi imekuwa kubwa mpaka tumeshindwa kuelewa Kama shida ni hiyo tu ya kula huyo mdada au Kuna mengine. Kwanza kapigwa ndani bila dhamana kwa muda wa siku kadhaa, katoa faini Kama 10M, kahamishwa kituo Cha kazi kwa gharama zake mwenyewe na mengine mengi.
 
Sawa mkuu, Muhimu kujifunza vyema misingi ya uandishi ili kuvutia watu kupata shauku ya kusoma na kujua litakalofuata mbele katika simulizi zako.
 
Ni haki yako kumpenda yeyote....sasa sijui kama mke wa mtu ni yeyote....katafute kwenye sheria yeyote ni nani???Endelea tu na unachokifanya, utapata tu unachokitafuta...Usiache tu kutembea na ile Baby Vaseline...... Watu wakikuoa, uje pia hapa JF kutupa mrejesho wa hii story......Mimi ni MMpem
Unaongea ongea tu kama umelishwa dawa za kulevyfun

..Kumbe ni Simulizi TU!
😀😀😀 Kumbe ulijua ni kweli !!! Simulizi tu ndugu yangu
 
Nashukuru kwa ushauri wako ndugu yangu
 
Hizo story zako ndio unaandika hivi?
Janja la Kinyaturu[emoji38][emoji38][emoji38][emoji38]

NB "si kanipenda mwenyewe...............
Hahahah,, simulizi zipo nyingi tu kwenye group zipo nyingine katika vipande vipande sehemu ya kwanza na kuendelea
 
Kuna dogo kazini kwetu kakutwa na msala wa kungonoka na mke wa mtu, aisee kesi imekuwa kubwa mpaka tumeshindwa kuelewa Kama shida ni hiyo tu ya kula huyo mdada au Kuna mengine. Kwanza kapigwa ndani bila dhamana kwa muda wa siku kadhaa, katoa faini Kama 10M, kahamishwa kituo Cha kazi kwa gharama zake mwenyewe na mengine mengi.
Duh!! Kweli kakutwa na kitu kizito kichwani, mpe pole yake kamanda
 
Uzuri ameshasema ni hadithi ya kutunga. Amefikisha ujumbe kwa wale wote wanaopatwa upofu wa mapenzi kwa kupenda wake za watu wanafurahia pasipo kuona hatari iliyo mbele yao. Hongera kwa utunzi wako.
Hii ni story tu laini katika jamii zetu wapo watu wenye tabia kama hii. Wanadhani kuwa wanaweza kutembea na wake za watu na wasifanywe chochote. Hatakama mtu alikuwa mpenzi wako kabla hajaolewa akishaolewa tu achana nae tafuta mwingine. MKE WA MTU SUMU TUACHE KUISHI KIMAZOEA
 
Back
Top Bottom