danhoport
JF-Expert Member
- May 20, 2020
- 1,984
- 4,502
Wazima humu?
Mimi huwa na utaratibu wa kutoka na mwanangu asubuhi kumpeleka shule kila siku na huwa natoka nae kuanzia saa moja huwa tunapanda bajaji au bodaboda, sasa leo tukiwa tunatembea kuona kama tutakutana na bajaji ili tupande ndo akapita jamaa na Rumion nyekundu akaniambia panda nikusogeze mpaka stand na sisi tukapanda.
Wakati tumeshuka mwanangu akaniuliza "baba mbona hujamlipa nauli"? Ikabidi nimuongopee tu nikamwambia nimempa ila wewe hukuona.
Niseme tu ukweli japo jamaa kanisaidia ila roho imeniuma sana, manake mwanangu anajua baba yake ndo mtu mwenye nguvu kuliko baba za watu wote, mwanangu anajua baba yake ndo mtu mwenye hela kuliko baba za watu wote.
Roho imeniuma sio kwa wivu wa chuki kwanini sina gari bali ni kwa wivu wa maendeleo, itabidi nipambane na mimi ili nimpeleke mwanangu shule na usafiri.