Nimepewa lift nikiwa na mtoto wangu, roho imeniuma sana

Nashangaa sana hii tabia ya kumuamini mtu usiemjua anapokupa lift au unaomba lift
Una mtoto halafu unapanda vya bure
Hapo niemeweka risk zaidi maana hata peke yako sio salama kabisa kupanda vya watu

Kama ni psychopath na anakuuwa
Wengine ndio fantasy zao hizo
Mtoto anaekuona shujaa kwa sasa na ukamdanganya
Hivi kama just kama lingetokea mwanao akaachiwa bado ungekua hero wake

Acheni tabia za kupanda vya bure wakati hela mnazo
Nime Kumbuka documentary za watu wenye mawenge, Wana kuchuna ngozi mzima mzima😆😂
 
Wazima humu?

Mimi huwa na utaratibu wa kutoka na mwanangu asubuhi kumpeleka shule kila siku na huwa natoka nae kuanzia saa moja huwa tunapanda bajaji au bodaboda, sasa leo tukiwa tunatembea kuona kama tutakutana na bajaji ili tupande ndo akapita jamaa na Rumion nyekundu akaniambia panda nikusogeze mpaka stand na sisi tukapanda.

Wakati tumeshuka mwanangu akaniuliza "baba mbona hujamlipa nauli"? Ikabidi nimuongopee tu nikamwambia nimempa ila wewe hukuona.

Niseme tu ukweli japo jamaa kanisaidia ila roho imeniuma sana, manake mwanangu anajua baba yake ndo mtu mwenye nguvu kuliko baba za watu wote, mwanangu anajua baba yake ndo mtu mwenye hela kuliko baba za watu wote.

Roho imeniuma sio kwa wivu wa chuki kwanini sina gari bali ni kwa wivu wa maendeleo, itabidi nipambane na mimi ili nimpeleke mwanangu shule na usafiri.
Ndio maana mnashauriwa msizae kabla ya kujipanga vizuri, soon atapata akili na kukuona unaendesha Tz 11, hapo ndio anaona mshua chenga tu.
 
Wazima humu?

Mimi huwa na utaratibu wa kutoka na mwanangu asubuhi kumpeleka shule kila siku na huwa natoka nae kuanzia saa moja huwa tunapanda bajaji au bodaboda, sasa leo tukiwa tunatembea kuona kama tutakutana na bajaji ili tupande ndo akapita jamaa na Rumion nyekundu akaniambia panda nikusogeze mpaka stand na sisi tukapanda.

Wakati tumeshuka mwanangu akaniuliza "baba mbona hujamlipa nauli"? Ikabidi nimuongopee tu nikamwambia nimempa ila wewe hukuona.

Niseme tu ukweli japo jamaa kanisaidia ila roho imeniuma sana, manake mwanangu anajua baba yake ndo mtu mwenye nguvu kuliko baba za watu wote, mwanangu anajua baba yake ndo mtu mwenye hela kuliko baba za watu wote.

Roho imeniuma sio kwa wivu wa chuki kwanini sina gari bali ni kwa wivu wa maendeleo, itabidi nipambane na mimi ili nimpeleke mwanangu shule na usafiri.
Tafta pesa mkuu. Nguvu ya pesa niliioma christmas coco beach alipokuja mjukuu wa bakhresa sidhani hata kama ana umri wa miaka 18 ila wahudumu wa pale walivyobabaika sijapata kuona. Na mwisho hakumunua hata soda ila full kupraise na kuworship
 
Back
Top Bottom