David Harvey
JF-Expert Member
- Jul 17, 2014
- 2,894
- 6,020
Heri ya Pasaka!
Eneo nilipo kuna wafanyabishara 5 wanauza nyama ya nguruwe kilo 1 wanauza elfu 12, ilo eneo mimi ni mgeni nina miezi 4 tu Ila punde baada ya kufungua banda langu nilikuwa nauza bei sawa na wenzangu sh 12k lakini nilikuwa siuzi kabisa naweza kukaa mpaka siku 4 siuzi kabisa ikafikia hatua nyama ikawa tasteless napata hasara nyama natupa.
Baadae nikapiga hesabu nikasema ngoja nishushe bei niuze KG 1 kwa elfu 8, nikabandika tangazo kuwa nyama ni elfu 8 tu Mambo yakawa c haba nikaanza kupata wateja wakutosha tu kwa wiki nikawa nachinja mpaka nguruwe 3.
Juzi kijana wangu niliyemuajiri wakamfata wakamwambia dogo unatuharibia biashara tafadhali tunaomba uuze bei ile ile ya mwanzo 12k,dogo akasema mimi sio boss ngoja niwape namba za boss; walivyopata namba zangu wakanipandia hewani wakaanza kuniambia nishushe bei nawaharibia biashara na hiyo ndio biashara inayoendesha maisha yao na familia yao.
Leo asubuhi wamenifata nyumbani sijajua ni nani aliyewaelekeza wakanipiga mkwara mzito lazima roho yangu iende kuzimu.
Nipeni ushauri wananzengo, nifanyaje?Tusijekufika pabaya maana wanaoneka hawatanii.