Nimepewa onyo na wafanyabiashara wenzangu nisipopandisha bei watakatisha uhai wangu

Nimepewa onyo na wafanyabiashara wenzangu nisipopandisha bei watakatisha uhai wangu

Heri ya Pasaka!

Eneo nilipo kuna wafanyabishara 5 wanauza nyama ya nguruwe kilo 1 wanauza elfu 12, ilo eneo mimi ni mgeni nina miezi 4 tu Ila punde baada ya kufungua banda langu nilikuwa nauza bei sawa na wenzangu sh 12k lakini nilikuwa siuzi kabisa naweza kukaa mpaka siku 4 siuzi kabisa ikafikia hatua nyama ikawa tasteless napata hasara nyama natupa.

Baadae nikapiga hesabu nikasema ngoja nishushe bei niuze KG 1 kwa elfu 8, nikabandika tangazo kuwa nyama ni elfu 8 tu Mambo yakawa c haba nikaanza kupata wateja wakutosha tu kwa wiki nikawa nachinja mpaka nguruwe 3.

Juzi kijana wangu niliyemuajiri wakamfata wakamwambia dogo unatuharibia biashara tafadhali tunaomba uuze bei ile ile ya mwanzo 12k,dogo akasema mimi sio boss ngoja niwape namba za boss; walivyopata namba zangu wakanipandia hewani wakaanza kuniambia nishushe bei nawaharibia biashara na hiyo ndio biashara inayoendesha maisha yao na familia yao.

Leo asubuhi wamenifata nyumbani sijajua ni nani aliyewaelekeza wakanipiga mkwara mzito lazima roho yangu iende kuzimu.

Nipeni ushauri wananzengo, nifanyaje?Tusijekufika pabaya maana wanaoneka hawatanii.
Katika pita pita zangu kwenye maandiko matakatifu nilikutana na maneno Haya "Watu wale wajitakasao, na kujisafisha katika bustani, nyuma yake aliye katikati; wakila nyama ya nguruwe, na machukizo, na panya; watakoma pamoja, asema Bwana".
Isaya 66:17
Kama wewe ni Mcha Mungu, Nyama ya nguruwe Sio chakula, Tafuta biashara nyingine.
 
Nyie wote hiyo biashara ni haramu naxwengi wenu ni wskristo ila ulafi unawasumbua someni kitabu chenu biblia takatifu ioiyoandikwa kwa roho mtakatifu kama inavyodaiwa soma WALAWI 11:7 MPAKA 8. NAJISI KWENU MSIILE WALA MSIGUSE MIZOGA YAO 😂ATI MNACHINJA TOKA LINI NGURUE ANACHINJWA HUPIGWA RISASI YA KICHWA AU NYUNDO YA KICHWA.
 
Watakuua wachaga hao [emoji1787][emoji1787]roho zao ziko kwenye hela kama mchungaji kimaro [emoji1787][emoji1787]katoea taarifa kituo Cha polisi au hamisha goli la biashara ,tafuta sehemu jiran kiasi na hapo afu uuze kwa bei hiyohiyo ya elfu 8 wateja wako watakufata
Nakataa mkuu wachaga hatupo hivyo , ingekua apo ni wachaga wangewaambia wateja jamaa anauza vibudu ,ndio maana kapunguza bei , then wateja wajiongeze wenyewe.
 
Ondoa tangazo wapunguzie bila tangazo. Ila elf 4 umepunguza Sana .
Au ingia nao mkataba wauzie wao KWA elf 8 KWA jumla Ili wabaki na soko.
Umeshindwa hama kaanzishe chimbo pengine mdudu anauzika popote
 
Ondoa tangazo wapunguzie bila tangazo. Ila elf 4 umepunguza Sana .
Au ingia nao mkataba wauzie wao KWA elf 8 KWA jumla Ili wabaki na soko.
Umeshindwa hama kaanzishe chimbo pengine mdudu anauzika popote
 
Wakipiga simu fanya recording ya mazumgumzo yao tena wa provoke kidogo ili kuwachota. Wakikufuata buchani record fasta na chukua video wqanachosema. Mpe dogo wa dukani smart phone kwa muda ili awafanyie recording. Hapohapo nenda ka report polisi ukianzia ofisi ya serikali ya mtaa ya eneo ulipo. Watakamatwa na watafunguliwa kesi ya jinai kulingana na matishio waliyofanya kwako. File likifika kwa DPP unamtafuta mwendesha mastaka wako mnakaa mnasuka kesi ya jinai yenye vifungu kadhaa vya makosa ya jinai (penal code) zenye miaka kadhaa ya kufungwq. Hakikisha unao ushahidi imara. Nakuambia watafungwa si chini ya miaka 7 na kuendelea.
 
Babu uza bei hiyo hiyo elfu 8 wananchi wenye kipato kidogo tupate sehemu ya kupoza roho,mbeya,iringa, Kilimanjaro,ruvuma bei zao kitonga tu Ila dar wanajifanya wanauza bei kubwa mbezi kuna sehemu elfu 15
Mkipatikana watu 10 kama nyie maisha yatakuwa kitonga sana just image kabla pasaka nyama ya ng'ombe ilikuwa elfu 7 jana bei ikapaa wakawa wanauza elfu 9/10
Mbezi kitimoto ni ghari Sana,Dar sehemu nyingine elfu kumi na mbili lakini Mbezi sehemu nyingi ni 14
 
Hata mimi ningekufata, hawa watu humu wanakuvimbisha kichwa ila ukweli ni kuwa unaharibu biashara za watu na watakufanya kitu mbaya ukizidi kuwa kichwa ngumu.
Pandisha bei hadi 11500 au 11000 utaeleweka.
Mbona Simu Kariakoo kwingine laki nne kwingine tatu na nusu lakini simu hiyohiyo Moja lakini hawana hizi mambo
 
Tatizo wewe bado uko kwenye 'theory' za supply vs demand; uhalisia sio hivyo, ndio maana kuna taasisi au umoja unao 'regulate' bei; tofauti na hivyo mtoa mada akichukua ushauri wako anaweza kujikuta yuko mbinguni, kama alivyoonywa.​
Umeongea kitu ambacho kanjanja wengi hawajui
But wanaingia tu kwenye biashara kuharibu projects za watu wengine hususani ukute ile biashara ndio inampa pato la kwanza.
 
Katika hii dunia, kuna vitu inabidi uende wa step, hasa vitu vinavyohusu kugusa maslai ya watu; tofauti na hivyo, unaweza ukatangulia na ukawaacha wenzako wanaendelea na maisha
Watanzania kama hawa ndio wanafanya taifa lionekane halina watu wanaotosha kusimamia Miradi mikubwa ya uchumi kwa kuhisi eti kuna kitu kinaitwa biashara huria.
In a real sense hakuna kitu kinaitwa Biashara huria ya wewe kuuza kwa discount ya asilimia 33.3333
Halafu watu wanatoa haki kwa Mtu anaedistort price sokoni?
Mtu hakatazwi kufanya Price-discount hasa kwa short time like mwezi au miezi miwili, kwa ajili ya kushoot mauzo then baada ya hapo ana-level price ili asiumize wengine.
Mkuu Equation x unahangaika bure kubishana na wahitimu ambao hawajawahi kufanyia kazi taaluma zao field
Maana unaweza kuta wachumi ndio wanaoongoza kuajiriwa huku wakiwa wanakosoa uchumi wa nchi ambapo wao wenyewe hawazalishi chochote zaidi ya kusubiri mshahara mwisho wa mwezi.
 
Katika hii dunia kila kundi huwa lina umoja wao, na huo umoja ndio unaowafanya waongee lugha moja; inapotokea mmoja atoke nje ya umoja na kufanya maamuzi yatakayoathiri umoja wa kundi husika, anakuwa amejitengenezea uadui.
Na hii inaweza kuathiri ata uhai wake.​
 
Napenda sana umoja katika kufanya biashara shida baadhi ya watu katika biashara huleta unafiki na roho za ubinafsi kama mtoa mada. Wakubwa ( Mashirika na makampuni makubwa ) yalishajua namna ya kumantain soko ni kuwa na Regulatory bodies in association na serikali za mataifa husika but, wasaka tonge sisi hudhan tukivunja bei ndio mafanikio, hakuna balance sokoni.
So baadae Industry inakufa kibudu tunabaki kusema biashara fulani kwa sasa hailipi wakati tuliua channel wenyewe na kuifanya iwe ya hivyo mleta mada anadhani kuvunja bei ni vizuri je akija mtu mgeni akaweka hapo jiran yake nae akauza kilo kwa 6k yeye tena ataungana na wale wanaotaka kumuua ili wamuue huyu wa 6k thats the circle
If you think you can break it what makes you think others can't?
 
Umeongea kitu ambacho kanjanja wengi hawajui
But wanaingia tu kwenye biashara kuharibu projects za watu wengine hususani ukute ile biashara ndio inampa pato la kwanza.
Projects za watu sio tu kuuza nguruwe, hata mazao ya kilimo ni project za watu na ndio zinazowapa pato la Kwanza, mnavyotetea bei kubwa kwenye nguruwe mngeongeza nguvu hizi kwa wakulima kama alivyoanza bashe, hakika tz ingetoa mabilionea buku wakulima!!
 
Ukiwatetea wakulima unamaanisha wapandishe bei ya mazao ifike wapi mkuu?
 
UNATAKA KUWAONDOA KWENYE GAME HAHA..... ILA HILO UNGEANZA NA GAP DOGO WAKISHUSHA UNAWASHUSHA TENA MPAKA WAOMBE POO KISTAAARABU WASINGEKUTISHA MAANA NAO WANGEKUA WAMESHUSHA PIA
 
Napenda sana umoja katika kufanya biashara shida baadhi ya watu katika biashara huleta unafiki na roho za ubinafsi kama mtoa mada. Wakubwa ( Mashirika na makampuni makubwa ) yalishajua namna ya kumantain soko ni kuwa na Regulatory bodies in association na serikali za mataifa husika but, wasaka tonge sisi hudhan tukivunja bei ndio mafanikio, hakuna balance sokoni.
So baadae Industry inakufa kibudu tunabaki kusema biashara fulani kwa sasa hailipi wakati tuliua channel wenyewe na kuifanya iwe ya hivyo mleta mada anadhani kuvunja bei ni vizuri je akija mtu mgeni akaweka hapo jiran yake nae akauza kilo kwa 6k yeye tena ataungana na wale wanaotaka kumuua ili wamuue huyu wa 6k thats the circle
If you think you can break it what makes you think others can't?
Naungana na wewe mfano sisi tunauza soda tunapata faida sh 600/kwa kreti, na wakati huo unanunua kampuni ya pepsi inakuchagulia brand wanayoitaka wao sio wewe unayoitaka, faida yote unajikuta inabaki kwenye brand isiyotoka

Wafanyabiashara katika eneo husika tulikubaliana tupandishe bei lakin mmoja aligoma akawa anauza bei elekezi ya kampuni
Sisi pia tukaamua kushusha bei

Inaumiza faida ni ndogo tunaishia kuinufaisha kampuni, sidhani kama kuna mfanya biashara aliyetajirika kwa kuuza soda za chupa bila kuabuse bei, risk ni kubwa chupa zinavunjika.
 
Back
Top Bottom