Aisee! Lazi unayo. Ushauri wangu ni kama ifuatavyo; kama jamaa ni rafiki yako kweli basi mshitue.
Sababu ya kukuambia hivyo ni kwamba hiyo Story sio siri tena, kwani inaonekana wengi hapo mitaani wanazijua ila yeye tu ndiyo hajui.
Pili huwezi kwema majukumu kwani tayari umesha ingiza kwenye hiyo issue, kilicho baki ni wewe kumweka rafiki yako sawa.
Zingatia kuwa mpaka wewe umeipata na kuingizwa kwenye hiyo kesi, ni kwa sababu inaonekana kuwa wengi wanatumia na kitendo hicho, ila wanaogopa kuchukua majukumu. Kitu kinacho wasumbua katika hili ni kama ulivyo sema kuwa jamaa ni mmpole sana na kwa hali hiyo wanahofia Reaktion yake itakuwaje kipindi atakapo pata hiyo taarifa.
Kwa tabia yake, kama ulivyo characterize, ana weza akachukua uamuzi wa kuondoa maisha yake. Kwa hali hiyo ndiyo maana wamekutupia game wewe uimalize. Usipofanya sasa hivi iko siku atatokea jasiri atamwambia ukweli na hapo huwezi jua, inawezakana wakakusukumia wewe kwa kumwambia kuwa rafiki yako anajua hiyo issue lakini hakuna kukueleza. Na hapo utakuwa umesha makosa rafiki yako na kuvunja uhusiano pengine.
Huna choice bali ni kufunga goli tu. Huyo mke wake, kama ambavyo nimedokeza hapo awali, inaelekea ana maadui wengi mitaani kwake. Watu wana donge naye kubwa. Na wewe usipocuheza huo mpira itakula kwako. Kuwa na ujasiri na mweleze rafiki yako.
Katika ufunguzi wa maelezo yako tumia kauli za kumfanya yeye ajitafakari, kwa mfano; unaweza ukamwambia "amwangalie sana mke wake". Akikuuliza kwa nini? Mwambie kuna fununu kuwa mke wake anafanya mambo yanamwondelea heshina yake mtaani. Akiendelea kuuliza, mwambie "awa consult jirani zake kuhusu hiyo issue wata.msaidia."