Nimepewa siri nashindwa kuitunza (roho inauma)

Nimepewa siri nashindwa kuitunza (roho inauma)

Tatizo siku mwana akijua na akajua kuwa ulikuwa unajua kitambo tena na wakati huo ndo ashaukwaa ule ugonjwa wetu kupitia kwa huyo mke wake. Ndo urafiki utaishia hapo....NA ATAKUONA WE NDO SNITCH MAISHA!!!
 
Ndugu yangu achana na mambo yasiyokuhusu. Ukimwambia jamaa yako wewe ndio utaonekana unavuruga ndoa yao na wala sio hao wapambe waliokupa story. Ukiona unakosa kifua basi wakwepe hao jamaa uachane nao kabisa kwenye Maisha yako au lah mkopeshe huyo jamaa hela akatengeneze gari yake ili usiwe na ukaribu nao.

Kama kujua kama mtoto sio wake ajue mwenyewe huko sio kwa kuambiwa na wewe. Halafu kumbuka "kitanda hakizai haramu" wazee wa zamani walisema
 
When two stimulus are repeatedly paired together stimulus one starts to acquire properties of stimulus two

To no truly I wondering water can be down but not all stimulus will finish because the sun will fabulous than the car although me travelled to Mars yesterday I will see you yesterday madam mahondaw and sir suzukiw
 
Nikodi mimi nikamteke huyo kijana atueleze kinagaubaga wala sio kazi ngumu!
Ndani ya siku masaa 24 namleta wewe nipe adress yake, picha yake namleta bila malipo akiwa analia sana
 
Halafu mtoto wa miezi 10 huwezi mfananisha bado na mtu mzima, sura za watoto wadogo huwa bado zabadilika badilika

Kabisa mkuu mi wangu ana miezi 11 na anafanana na padree wa huku kwetu mpaka kucheka 😂 sijajua baba watoto anawaza vipi ila sio sawa kwakweli mana mimi hata salamu ya karibu na padre sijawahi kusalimiana naee😁😁
 
mkuu unaweza kuta jamaa yako kifua hana ukimwambia unaweza ukasababisha janga au ukajiaibisha mwenyewe muda utafika tu ukweli utajulikana waachie mambo yao jamaa yako naye kayataka mwache apambane na hali yake
 
Mwokoe kijana mwenzio na maradhi kama kisukari, presha, matatizo ya moyo au Ukimwi.

Halafu kama mke anaendelea kuzini basi atakuwa anatafuta wa pili. Sasa kama akiwa nao watatu na jamaa akawa na mali mbili Tatu mke na mzazi mwenzie watawaza nini?

Okoa maisha. Ila uwe na uhakika sio ukurupuke.
 
Hiki ndicho kinachonipagawisha hata mimi najikuta naumia kuliko mhusika
Ili uweze kumsaidia huyo rafiki yako jaribu kwanza kuivaa nafsi yake. Fikiria ungekuwa ndio ww umetendewa hivo na unaendelea kusalitiwa.
 
We huna urafiki wa kweli vipo vitu unaweza ukamficha rafiki lakini sio kugegedewa mkewe hadi anazalishwa na mtoto
 
Hiki ndicho kinachonipagawisha hata mimi najikuta naumia kuliko mhusika
Fanya jambo umsaidie mwenzio mkuu. Maana huyo dem wake anaonekana ameridhika na huo uovu wake na anaonekana ataongeza na petii mwingine.
 
Naona kama ngoma itanigeukia mimi iwapo ishu haitakuwa kweli? Au kuna ile mwanaume anampenda sana mkewe wakaniona mimi kama mchonganishi.NITAJIONA KAMA NIMEKUWA SHANGINGI AU MMBEYA FULANI HIVI ALAFU MI MWANAUME KABISA WA MKOANI.
Aisee! Lazi unayo. Ushauri wangu ni kama ifuatavyo; kama jamaa ni rafiki yako kweli basi mshitue.

Sababu ya kukuambia hivyo ni kwamba hiyo Story sio siri tena, kwani inaonekana wengi hapo mitaani wanazijua ila yeye tu ndiyo hajui.

Pili huwezi kwema majukumu kwani tayari umesha ingiza kwenye hiyo issue, kilicho baki ni wewe kumweka rafiki yako sawa.

Zingatia kuwa mpaka wewe umeipata na kuingizwa kwenye hiyo kesi, ni kwa sababu inaonekana kuwa wengi wanatumia na kitendo hicho, ila wanaogopa kuchukua majukumu. Kitu kinacho wasumbua katika hili ni kama ulivyo sema kuwa jamaa ni mmpole sana na kwa hali hiyo wanahofia Reaktion yake itakuwaje kipindi atakapo pata hiyo taarifa.

Kwa tabia yake, kama ulivyo characterize, ana weza akachukua uamuzi wa kuondoa maisha yake. Kwa hali hiyo ndiyo maana wamekutupia game wewe uimalize. Usipofanya sasa hivi iko siku atatokea jasiri atamwambia ukweli na hapo huwezi jua, inawezakana wakakusukumia wewe kwa kumwambia kuwa rafiki yako anajua hiyo issue lakini hakuna kukueleza. Na hapo utakuwa umesha makosa rafiki yako na kuvunja uhusiano pengine.

Huna choice bali ni kufunga goli tu. Huyo mke wake, kama ambavyo nimedokeza hapo awali, inaelekea ana maadui wengi mitaani kwake. Watu wana donge naye kubwa. Na wewe usipocuheza huo mpira itakula kwako. Kuwa na ujasiri na mweleze rafiki yako.

Katika ufunguzi wa maelezo yako tumia kauli za kumfanya yeye ajitafakari, kwa mfano; unaweza ukamwambia "amwangalie sana mke wake". Akikuuliza kwa nini? Mwambie kuna fununu kuwa mke wake anafanya mambo yanamwondelea heshina yake mtaani. Akiendelea kuuliza, mwambie "awa consult jirani zake kuhusu hiyo issue wata.msaidia."
 
Serikali haitakubari kwa sababu ya kuepuka watoto wa mtaani
Nina Campaign naianzisha soon kuhakikisha watoto wote kabla hawajaandikwa kwenye card za clinics hatimaye Birth Certificates wazazi wao( Baba + Mama) wawe wamefanyiwa DNA testing kuthibitisha kama ni watoto wao au laa
Na hii itabidi ifanyike kwa watoto wote wanaozaliwa hapa nchini
 
Hahahaha!!!

Hii kali
Kabisa mkuu mi wangu ana miezi 11 na anafanana na padree wa huku kwetu mpaka kucheka [emoji23] sijajua baba watoto anawaza vipi ila sio sawa kwakweli mana mimi hata salamu ya karibu na padre sijawahi kusalimiana naee[emoji16][emoji16]
 
NIP
Habari zenu wazee wa mmu,

Nina mfanyakazi mwenzangu ambae pia ni best yangu sana kwa kuwa hata mipango ya maisha huwa tunapeana mbinu mbili tatu ili tuweze kuzidi kunyanyuka kimaendeleo.

Mimi nimeoa na yeye ameoa sasa huyu jamaa yangu ni type fulani ya watu wapole kupita kiasi.

Hapa karibuni mke wake kamfukuza dada wa kazi na mtoto na wana mtoto wa miezi 10 hivi kama sikosei,mke wake nae ni muajiriwa sector nyingine tofauti na yetu, sasa huyu jamaa yangu huwa nampitia kumchukua na tunaenda kazini kwa sababu gari yake imepata ajali haiwezi tembea. Imekuwa kama ratiba ya kawaida mimi kumpitia pale nyumbani kwake kwa kuwa ni njiani kuelekea kazini

Sasa siku moja nimepack kwa nje namsubiria jamaa akatokea dada mmoja na kunisalimia nikiwa ndani ya gari akaniomba nimpe namba yangu kuna ishu sensitive anataka kuniambia. Mwanzo nilihisi labda anataka tuanzishe mahusiano nikataka kumpa namba ya uongo anyway kwa sababu mimi ni mwanaume nikasema ngoja nimpe ya ukweli.

Siku ya pili tangu nichukue ile namba nikapokea namba mpya kumbe ni ya yule mdada akaanza kuniomba msamaha kuwa hajapenda kunihusisha mambo ambayo hayanihusu,nikamuuliza mambo yapi?

Akaanza kuniambia rafiki yako unampitiaga kila siku kuna mchezo anachezewa, kuuliza upi akasema "Kaka nyie mkiondoka mke wake huwa anampeleka nyumba ya jirani mtoto kwa mmama fulani ambae huyo mama ana kijana yake ambae huku mtaani tunajua anatembea na mke wa rafiki yako na mtoto ni wa huyo jamaa so pale kwa yule mama kuna kila aina ya vikolo kolo vya kuchezea mtoto vimenunuliwa na yule kijana wa yule mtoto na yule mama

Kwa kujiongeza nikasema isije huyu dada alikuwa na mahusiano na jamaa yangu hivyo kaachwa sasa anataka kusambaratisha ndoa ya huyu rafiki yangu ikabidi nianze kuchunguza ndipo nikapata jina la yule kijana wa yule mama na kulisearch fb nikaziona picha zake na kuanza kuzifananisha na picha za yule mtoto wa rafiki yangu ki ukweli kama kuna ufanano fulani kati ya yule mtoto na yule kijana.

Sasa kila nikimpitia jamaa huwa namuangalia usoni natamani kumuambia ila sina kithibitisho ya yale niliyoambiwa na yule dada najikuta naumia mimi kwa sababu jamaa huwa ananieleza plan nzuri kuhusiana na familia yake haswa maendeleo ya kuwalinda watoto wasije fedheheka huko mbeleni.

Imefika muda nikimuona mke wa jamaa natamani nimpasukie ila ushahidi sina hebu wana mmu tushauriane. Je, hapa ni-mute au nitapike tu?
Nipe namba ya huyo jamaa nimwambie ukwel then wewe utakuwa umemsaidia maana ataepeka future cost za kumlea huyo mtoto
 
Ndugu yangu achana na mambo yasiyokuhusu. Ukimwambia jamaa yako wewe ndio utaonekana unavuruga ndoa yao na wala sio hao wapambe waliokupa story. Ukiona unakosa kifua basi wakwepe hao jamaa uachane nao kabisa kwenye Maisha yako au lah mkopeshe huyo jamaa hela akatengeneze gari yake ili usiwe na ukaribu nao.

Kama kujua kama mtoto sio wake ajue mwenyewe huko sio kwa kuambiwa na wewe. Halafu kumbuka "kitanda hakizai haramu" wazee wa zamani walisema
Ninyi ndio husababisha nchi kuyumba kwa kukaa na siri za watu waovu. Sababu mnayotoa eti hayakuhusu! Usalama wa nchi huanzia usalama wa mtu mmoja (human security), halafu usalama wa jamii inayokuzunguka (societal security) ambayo kwa ujumla wake hutengeneza usalama wa taifa (national security).

Tatizo la mwenzako ni lako maana linaweza kukuathiri wakati na majira usoyajua. Kinachopaswa kuzozaniwa sio kuambiwa bali ataambiwaje na kwa kutumia njia (modus operandus) ipi!

Bazazi!
 
Back
Top Bottom