Nimepewa Taarifa na washikaji zangu kijiweni kwamba kuna watu wananitafuta

Hivi mkuu akija askari mmoja wale ambao huwa wanavunja tofali kwa ngumi unaweza kabiliana nae?

Imagine wapo 6 na wana silaha either uzi au smg.

Utachomoka hapo?
Kukabiliana nao ni kipengere mkuu ila kwenye issue za kutafutana ni weupe mno ndio maana wanatumia mbinu za manually sana sijajua ni techonolojia ndio ndogo au lack of skilled labour 😁
 
Ukamtwe kwa kosa gani? Unahisi ni kina nani?
 
Wale Wafanyabiashara waliuawa kutokana na sababu za kiuhalifu tu walizonazo Polisi wengi zaidi waliopo hapa nchini.

Aidha, ogopa sana Polisi kujua kwamba una pesa, watakufuata ili wakupore pesa ulizonazo na Kisha wakuue ili kupoteza kabisa ushahidi. Nakumbuka mojawapo ya kisa kimoja cha kweli kilichotokea miaka zaidi ya kumi iliyopita ktk mkoa fulani ambao nisingependa kuutaja jina, wafanyabiashara wawili wa mifugo walikodi gari ili liwapeleke kwenye mnada wa mifugo (ng'ombe) ktk mji fulani. Wakiwa safarini njiani walikutana na gari la Polisi wa doria za barabarani, na Kisha gari la wafanyabiashara hao likasimamishwa, walikuwapo Askari Polisi wawili tu ambao baadaye ilijulikana kuwa walitumwa na Rpc ili kuwafuatilia wafanyabiashara hao na kuwakamata kwa sababu Polisi walishatonywa kuwa wafanyabiashara hao wamebeba fedha nyingi za kwenda kununulia ng'ombe. Wale wafayabiashara walikamatwa na Kisha kwenda kuhifadhiwa sehemu fulani kwenye nyumba binafsi ya mmoja wa maaskari, hawakupelelwa katika Kituo cha Polisi. Baadaye usiku "mkubwa" aiyewatuma kazi alikuja kwenye hiyo nyumba na kuchukua 'mzigo wake' na kisha kuamuru wafanyabiashara hao wote na dereva wamalizwe na gari yao kwenda kutelekezwa ktk mji wa mbali karibu 80km kwenye wilaya ya jirani, na ilifanyika hivyo usiku huo huo na baadaye ilikuja kujulikana kuwa wale wafanyabiashara walikuwa na fedha Tshs. 60milioni cash. Maiti za wale wafanyabiashara pamoja na dereva wao waliyemkodi walienda kuzitupa mbali kwenye mashamba ya wakulima. Wakati matukio yote haya yakiendelea kulikuwa na Askari Polisi mmoja ambaye hakuwa zamu siku hiyo ambaye alikuwa akiishi kwenye mtaa mmoja wenye nyumba walikohifadhiwa wafanyabiashara wa mifugo waliotekwa. Askari huyo baada ya kuona gari la Polisi wa doria lenye namba za kawaida za kiraia lilikuwa linapita mara kwa mara mtaani hapo siku hiyo aliamua kulifuatilia gari hilo na mchongo huo wote kisirisiri bila ya hao Askari wenzake kujua.
Miezi michache baaaye minong'ono ya taarifa hii ilivuja na ilianza kusambaa mitaani, wale Askari waliopiga dili walifuatilia ili kujua nani hasa chanzo cha taarifa za kubumbuluka kwa dili lao la Siri kubwa, wakagundua kuwa chanzo Cha kuvuja kwa taarifa hiyo ni Askari mwenzao . Ndani ya muda mfupi kabisa yule Askari aliyevujisha taarifa hizo alimalizwa/aliuawa, alikutwa 'amekufa' nyumbani kwake, na muda mfupi siku chache baadaye yule Rpc alihamishwa kutoka mkoa ule(inavyoonekana huenda makao makuu ya Polisi walipata taarifa za dili lile). Polisi ni hatari, kaa nao mbali kama umebeba pesa taslimu.
 
HAKIKISHA MTU MWENYE RASTA AU KIJANA YOYOTE ALIYEONGOZANA NA BINTI HAWAKUKARIBII, USIKUBALI KUINGIA KWENYE GARI AINA YA NOAH KWA MAELEZO KUWA UNAELEKEA KITUO CHA POLISI.
 
Haya mambo bwana unaweza kuona kama sio shida kwakua hajakukuta wewe au Ndugu yako ama rafiki yako wa karibu.
Tanzania yetu haikuwa hivi miaka yote. Tuwe wa moja maana tukishirikiana kwa Umoja wetu tunaweza kuokoa nchi yetu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…