PreGE2025 Nimepewa wito nigombee Ubunge lakini nimeambiwa hamnahamna niandae 30M kwa kampeni. Nifanyeje?

PreGE2025 Nimepewa wito nigombee Ubunge lakini nimeambiwa hamnahamna niandae 30M kwa kampeni. Nifanyeje?

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Ijumaa Kareem!

Nchi IPO pazuri. Uchaguzi! Uchambuzi!
Kuingia mjengoni nikagonge Meza. Jioni nipokee mkwanja.
Sasa kuna mtu asiyejulikana au tumuite aliyesahaulika ingawaje heshima yake ingalimo. Juzi tulikuwa tunateta naye.

Kanambia huu ni mwaka muhimu Kwangu kama ningependa uwe hivyo. Anasema mfumo upo kwenye orbit yake. Yeye na wenzake wanazungukamo humo.
Akaongeza, kama ninataka aniunge kwenye orbit yao hiyo ambapo mihimili ya utawala inazungukepo hapo.

Lakini niandae hamnahamna 30M.
Anasema itakubwa Boom! Bam! Unaweka 30M unapata zaidi ya hiyo zaidi ya mara Mia. Dadeki!

Nikamwambia vipi kuhusu No reforms No election. Yule MTU asiyejulikana na aliyesahaulika lakini heshima yake ingalimo alinikazia macho yake yaliyobeba siri za kale ambazo zilibeba maamuzi ya watanzania waliowengi.

Nisiende mbele nikawaacha nyuma! Mimi niwaachie hapa.
Mkiamua kuendelea ni hiyari yenu. Mkiamua kubaki shauri yenu.

Nawatakia maandalizi Mema ya Sabato.

Taikon Master
Dsm
Bi Angela KAIRUKI anagawa pesa kama hana akili vizuri huko kibamba. Juzi alitoa 70000 kwa kila mjumbe
M 30? Hiyo labda serikali ya mtaa kidooigo
 
Bi Angela KAIRUKI anagawa pesa kama hana akili vizuri huko kibamba. Juzi alitoa 70000 kwa kila mjumbe
M 30? Hiyo labda serikali ya mtaa kidooigo
Mama ameamua kuzigawa, watu wanakula 50k za kutosha
 
  • Thanks
Reactions: apk
Mama ameamua kuzigawa, watu wanakula 50k za kutosha
Hakuna uchaguzi ambao pesa iatembea huko ccm kama huu. Ni kama vile nchi na chama kinajiendesha chenyewe
Ndege ipo off pilot yani
 
Mtibeli nakuheshimu sana lakini M30 sio hela ya kukuweka kwenye jimbo.Tafuta mishe nyingine.
Wamesema udiwani labda ndio itatosha.
Lakini pia ingekuwa wananchi wanachagua hata kama huna hela ya kampeni na wanakukubali mbona wanakuchagua tu sema sasa nchi yetu ndio imeshapinda uhuni mwingi NRNE.
 
Hakuna uchaguzi ambao pesa iatembea huko ccm kama huu. Ni kama vile nchi na chama kinajiendesha chenyewe
Ndege ipo off pilot yani
Kwa hiyo tuseme bila 100m+ huwezi kulipata jimbo mkuu! Kweli kwa sasa mwenye nacho anaongezewa.
 
Kwa hiyo tuseme bila 100m+ huwezi kulipata jimbo mkuu! Kweli kwa sasa mwenye nacho anaongezewa.
Yaani 100 ni ndogo sana. Mkuu hapo abda huko kijijini na tena mbunge mwenyewe awe ana kubalika sana
 
Haya mambo ndiyo yanayolipotosha taifa letu, that mean UBUNGE NI BIASHARA KAMA ZINGINE NDIYO MAANA UNAWEKEZA MTAJI?, Kuna andiko nimeliweka hapo kitambo, UBUNGE Isiwe biashara, mtu aende na sera zake, na ushawishi na rekodi zake za utendaji kazi ulioonekana kitambo!, pesa pesa pesa za nini?, kwa jinsi nijuavyo, mafao mengi ya wabunge hutumika kwa rushwa na ndiyo sababu ya hata wabunge wabovu kabisa kuendelea kuwepo bungeni.
Je hapo kunatofauti gani na pale unapo watetea wala kwa urefu wakamba.
 
Mipango nimeambia haitoshi.
Angalia hata humu wadau wanasema hilohilo. Na wanasema hata hiyo 30M ni kama nachekesha
hivyo ni vitisho vya kisaikojia katika siasa gentleman,

niliwahi kutoa simulizi ya attempt yangu ya kwanza kuwania ubunge. Nilikua na laki5 tu cash mkononi, hiyo hiyo ndio nauli yangu kutoka dar hadi jimboni, hiyo hiyo ndio ya kulipia gharama ya fomu. Hapo ni mchakato wa uteuzi tu ndani ya chama. Mengine ni simulizi ya kusisimua mno.

Bado baada ya kulipia fomu ya uteuzi kwenye chama nikaambiwa ninawajibika pia kuchangia zaidi ya 3.m gharama ya usafiri wa pamoja kwa wagombea kwenye kampeni ya kata kwa kata pale jimboni ambapo kuna kata zaidi ya 20.
Ilikua experience ngumu na ya kushangaza sana kwangu,

Licha ya changamoto hizo za kifedha nilitoboa na nikathibitisha
kweli Mungu yupo na anaweza kumtoa maskini mavumbini na kumketisha meza moja na wafalme.

Usikatishwe tamaa na porojo za kisayansi katika siasa. Wawekezaji kutoka ng'ambo huja Africa na ideas na mipango mikakati ya uwekezaji wao tu, pesa za uwekezaji huzipata humu humu Africa 🐒
 
Back
Top Bottom