PreGE2025 Nimepewa wito nigombee Ubunge lakini nimeambiwa hamnahamna niandae 30M kwa kampeni. Nifanyeje?

PreGE2025 Nimepewa wito nigombee Ubunge lakini nimeambiwa hamnahamna niandae 30M kwa kampeni. Nifanyeje?

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Chukua jimbo hilo Mkuu Kijana shupavu na Imara.

Nadokezwa Kila upande hiyo pesa ni ndogo.
Sasa najiuliza Kwa kijana wa kawaida wa kitanzania anawezaje kuwa Mbunge, yaani haki ya kugombea nafasi za kisiasa inamhusu vipi mtu Maskini ikiwa uongozi kuupata ni gharama kubwa
 
Dhamira na ujumbe wa andiko lako ni lipi? sasa.

Wewe ukitaka kuwa Mbunge kama haki ya kikatiba unahizo pesa ambazo nimeambiwa ni hamna hamna?

Jibu baki nalo, na jibu hilohilo ndio dhamira na ujumbe wa andiko.

Asante Kwa ushiriki
 
Usipoteze muda wako - hakuna uchaguzi mwaka huu bila reforms.
 
. Yule MTU asiyejulikana na aliyesahaulika lakini heshima yake ingalimo alinikazia macho yake yaliyobeba siri za kale ambazo zilibeba maamuzi ya watanzania waliowengi.




Umenikumbusha riwaya moja matata ya KISIWA CHA MADAGASCAR kwa haya maneno yako🤣

😄😄
 
Haya mambo ndiyo yanayolipotosha taifa letu, that mean UBUNGE NI BIASHARA KAMA ZINGINE NDIYO MAANA UNAWEKEZA MTAJI?, Kuna andiko nimeliweka hapo kitambo, UBUNGE Isiwe biashara, mtu aende na sera zake, na ushawishi na rekodi zake za utendaji kazi ulioonekana kitambo!, pesa pesa pesa za nini?, kwa jinsi nijuavyo, mafao mengi ya wabunge hutumika kwa rushwa na ndiyo sababu ya hata wabunge wabovu kabisa kuendelea kuwepo bungeni.

Wewe umenipata vilivyo Kabisa
 
Unaweza ukamzidi Babu Tale tale kidogo sana Kwa mchango wa Taifa hili anyway nenda wakakupruni haki ka m30

Huyo Babu Tale kwenye Taifa hili mchango wake ni mkubwa sana Kwa kiwango Cha mbali kuliko wewe na ukoo wenu plus ukoo wa Mkeo.
Kwenye music industry Babu Tale mchango wake umeleta matokeo makubwa yaliyoathiri makumi na mamia ya familia za Watanzania.

Kuhusu ubunge wake, Sina habari.
 
Back
Top Bottom