kilambimkwidu
JF-Expert Member
- Jul 21, 2017
- 6,097
- 7,199
Naomba nikosolewe au kupongezwa kwa utaratibu nilioelekeza nyumbani kwangu kwamba ni marufuku wife kupokea shukrani za mgeni anaeshukuru kwa chakula.
Hii imekua ikitokea hata kwa wageni ambao wanaishi muda mrefu, kwamba kila anapomaliza kula anamuangalia “mama mwenye nyumba” na kumshukuru kwa chakula.
Nimekataza hilo na kuelekeza shemeji yenu wakati wote kutoa elimu kwa upole kwa mgeni atakayeshukuru kuwa hatuna utaratibu huo na asiwe na hofu, ajisikie huru na kwakuwa ni mgeni wetu tunatamani ajione ni sehemu ya familia na anahaki na fursa sawa na wengine tuliopo.
Binafsi naona utamaduni huo ni unaguzi na unachochea madaraja na kufanya mgeni aendelee kujihisi ni mgeni wakati wote na chakula kwake aone kama hisani ambayo hakustahili kupata.
Nafikiri kwanini mgeni huyo asishukuru anapomaliza kuangalia televisheni kipindi anachokipenda, au ashukuru kila asubuhi kwa kupewa chumba cha kulala.
Baadhi ya familia hadi mtoto anashukuru kwa chakula kila anapomaliza kula. Hapana, hilo nimekataza.
(Picha haihusiani)