Nimepiga marufuku utamaduni wa mgeni kushukuru kwa chakula kila baada ya kula

Kushukuru ni Jambo jema, Kwanini tunamshukur Mungu kwa uhai wakati yeye ndo alituumba na alipaswa kutupa uhai. Lakin tunashukur kwa nafasi na upendeleo fulani. Kushukur humaanisha kuthamini.

Kisaikolojia mtu hujiskia vizuri anapothaminiwa hata kwa mchango kidg anaoutoa kwa watu au jamii.

Nikirud kwetu sisi, Jukumu la kushukur baada ya kula ni la kila mwanafamilia kumshukur aliendaa chakula maana inatumia muda mrefu kuandaa chakula kuliko kula.

Wakati fulani nilikua nimkiishi na mdogo wangu na nilikua nikimshukur kwa kuandaa chakula hata kama chakula nimeleta mimi. Lakin kupika ni kazi na kujitolea.

Watoto wanapaswa kumshukur Mungu kwa Riziki ya Chakula na wazazi pia kwa kuleta chakula nyumbani.

Mke anampa pole mume kwa kutafuta chakula na mahitaji, ni kuonesha kujali. Pia mume humshukuru mke kwa kupika chakula. Hii hufanya watu waone wanathaminiwa.


Utaratibu wa kushukuru ni utaratibu wa kiungwana. Mshukuru hata muhudumu hotelini au mgahawani anpoondoa vyombo vyako baada ya kula.

Narudia tena, Shukrani ni ustraabu wa kiungwana. Asieweza kuwashukuru watu hawezi Kumshukuru Mungu.
 
Kula ni ibada sheikh!
 
Umuhimu wa chakula sio sawa na tv, wala kitanda.

Kwa mimi kushukuru naona sahihi ila mtu asiponishukuru sio kesi pia, sioni tatizo kwa yeye kutokunishukuru. Ila mimi kushukuru naona ni sahihi.
 

kushukuru ni moyo. usiupangie moyo
 
Watoto na wengine wote hawashukuru. Kwanini mgeni ashukuru mara zote??
sasa nina umri wa miaka 43, tangia nizaliwe ndio mara yangu ya kwanza kusikia kuna WATOTO NA WENGINE WOTE HAWASHUKURU. Ama kweli kua uyaone. Duuuuuh
 
je vipi watoto wako wakienda kwa ndugu zao wengine, hawapaswi kushukuru?, na utajisikiaje ukienda ugenini halafu ukalazwq njaa??
 
Kwani shukrani inahusiana na ugeni? And by the way, kwa hio kwamba wewe huwezi kushikuru kwa chakula? Mtu ukimpa blanket wakat wa barid atashukuru alihitaji wakati huo, chakula wakati wa njaa atashukuru wakati huo, maji wakati wa kiu atashukuru wakati huo. Ukimstiri kwa nguo atashukuru wakati wa kumpa sio kila akivaa, ukimpa malazi atashukuru once or twice alipokuja ukampokea na atakapoondoka labda.


Thanks giving / Shukrani ni muhimu kila mtu akafundishwa kulitumia mara kwa kwa mara.
 
Mleta Uzi nimekuelewa vya kutosha
Ni kweli, ni utamaduni wetu kushukuru kwa Kila kitu, lakini sio Kila mtu anapendwa kushukuriwa

Mm hata nikienda kununua kitu dukani, ni lazima nimwambie ASANTE kwa sababu ndivyo tumefunzwa hvyo.

Ila mm Huwa sipendi mtu anishikuru, Tena kama nikifanya kitu ambacho ni nilipaswa kufanya (my duty).
Huwa nawakatalia sana
Au, niliona hatuelewani, basi jibu langu Huwa ni count nothing nikimaanisha asijali
 

Attachments

  • Screenshot_20241024-093809.jpg
    137.5 KB · Views: 2
  • Screenshot_20241024-093738.jpg
    26.3 KB · Views: 1
Kitu pekee kinachoweza kumfanya mtu akaendelea kuishi ni chakula. Mtu hawezi kufa kwa kukosa pa kulala,hawezi kufa kwa kukosa kuangalia Tv. Hivyo kushukuru kwa chakula ni sahihi,ksbb ndicho pekee kinaweza kumfanya mtu kufa akikosa.

Pili familia zingine zimelelewa hata watoto wakimaliza kula wanashukuru. Pia hata awe wa kwanza kukushukuru kuleta au kusababisha wale hapo nyumbani.
Uhangaikaji wa mtu mpaka familia ikala ikashiba ni kitu kikubwa sana. Japo wengi hata wewe unaweza kukiona cha kawaida,wengi wanakiona cha kawaida kilichozoeleka hivi. Lakini piga picha wapo wanazikimbia familia zao. Wapo wanaotelekeza watoto ksbb tu ya ugumu wa maisha. Kwa nini wasishukuru kwa kuwafanya waendelee kuishi?

Labda tu ningekuelewa ungesema nimejarmdiriana nao utaratibu wa kushukuru ubadirike,au tusishukuru ksbb unazotaka wewe.

Mwisho umesema umepiga marufuku kushukuru. Pamoja na kwamba kitendo hicho unaweza kuona ni kuwasaidia hivi,lakini pia ni marufuku ni kitendo cha kidicteta, kitendo cha kibinafsi. Unakuta wengine kati ya wageni wako wanajisikia huru sana moyoni wakishukuru. Lakini wewe na ubinafsi wako umewaondolea ile hali ya Uhuru wa nafsi moyoni kwao. Kuwe makini unapotunga sheria kuondoka uasili,kuna muda unaondoa Uhuru wa mwingine
 
Kushukuru ni utaratibu wa kistaarabu tu wala haina shida kutumika popote.

Maneno:
Asante.
Samahani.
Karibu.
Tafadhali.
nk

Yatumike bila kukoma.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…