Nimepiga marufuku utamaduni wa mgeni kushukuru kwa chakula kila baada ya kula

Nafikili awashukuru chakula ila kazi ya kupika chakula hicho kizuri.
 
Mkuu wazo lako zuri na nimeipenda lakin dhana ya kushukuru ni jema na chanzo chake ni kama agizo la Mungu anaposema "Shukuran Kwa kila jamboa" mm spingani na wazo lako ni zuri na pengne una Nia njema!!!
 
Je watoto wakishukuru kwa chakula walichokula inakuaje na hapo , manake wengine tulilelewa kushukuru baada ya kula kumshukuru Mungu na wazazi kwa kutulisha
Shukrani ni kwa Mungu, kwa wazazi utiifu wako kwao ni shukrani tosha.

Kushukuru kwa maneno kama "Asante kwa chakula" ni mbaya kati ya mtu na mtu haijalishi ni mtoto kwa mzazi, mgeni ama hata mfanyakazi wa ndani. Hatari yake kubwa ni kumnyongesha anaetoa shukrani na kumtia kiburi anayepewa hiyo shukrani.

Mimi kwangu pia ni marufuku hii kitu. Infact mwenye nyumba unapopokea wageni ni wewe unapaswa uwashukuru kwa ujio wao na kuwaonyesha umefurahi kuwa nao pamoja (sio immediately baada ya kula, bali pale wanapoaga wakati wa kuondoka). Hii ina opposite effect ya ile nilielezea hapo juu, mgeni anakuwa huru zaidi na furaha kuona amefurahiwa ujio wake na mwenyeji anaikandamiza nafsi yake dhidi ya kiburi kwa ukarimu alioufanya.
 
Haya ni makosa kaka, hupaswi kupokea shukrani kwa jambo la wajibu wako. Kulisha familia yako ni katika wajibu wa juu zaidi kwako. Mtoto kutoa shukrani kwa kupewa kitu ni jambo la sawa kabisa lakini sio kupewa chakula na mzazi wake. Halkadhalika tambua kuwa mgeni ni barka kwako na ni moja katika sababu za rizki yako, so hupaswi kusubiria shukrani kwa kutenda wajibu wako ama kupokea sababu ya kuzidishiwa rizki yako. Kuna mstari mwembamba sana wa kubakia humble ama kuangukia kwenye kibri baada ya kutenda wema.

Mashallah unaonekana ni Muislamu na unajitahidi kuishi hivo, Allah akuzidishie. Binafsi msimamo wangu ni huo na ninaamini kuwa hii ndo mila ya Mtume wetu (SAW)
 
wewe ni wa ajabu sana, kwani ukipata deal huwa humshukuru Mungu huko huko hata kimoyomoyo? Mwanangu akimaliza kula lazima naishukuru baba yake kwa kumtafutia chakula, anamshukuru mama yake kwa kupika na sisi tunamshukuru kwa kula, maana kuna mazingira unaweza tafuta chakula mtoto akawa anamsumbua kula na hili wazazi wengi huwa linawavunja moyo katika kutafuta, utasikia "hata nikimpikia nini hali" kwa hiyo mtoto akila anakupa moyo wa kumtafutia vingine.

Kushukuru inamaanisha unyenyekevu wa kupokea kile alichopewa, Mungu anapenda moyo wa shukurani, na ni utaratibu ambao Mungu anaupenda na anatuasa kufanyiana sisi kwa sisi, Moyo usioshukuru umejaa kiburi na majivuno
 
Mkuu waza vizuri, unamshukuru Mungu sawa, lakini Mungu hashushi chakula, bali huachilia nguvu ya utafutaji, basi mshukuru na aliyetumia nguvu katika kutafuta, lakini sio kutafuta tu na moyo wa kutoa, kuna Watu ni wachoyo anatafuta kwa ajili yake, sasa ukipata mtu anatafuta kwa ajili ya wengine unapaswa kumshukuru, kuna nyumba ukiingia utakunywa maji tu na kuondoka, lakini nyumba zingine ukiingia unatamani ukae hapo kwa ajili ya ule ukarimu, lazima ushukuru, sio hiari ni lazima kwa sababu umetendewa wema, Iweni na Moyo wa shukrani
 
Nadhani wewe umepitiliza kamanda. Kupokea shukrani kwa wema uliotenda sio kosa issue hapa ni kupokea shukrani kwa kumlisha uliye na wajibu nae kufanya hivo.

Akija mtu kwako akakuambia nina njaa naomba nisaidie chakula, huyu ukimpa na akikushukuru ni sawa kupokea shukrani yake kwakuwa haikuwa wajibu wako kumlisha, so inabakia kuwa ni wema kama wema wowote ambao ungeweza kumtendea stranger yeyote. Ila raia wako nyumbani ni wajibu wako kuwalisha so hupaswi kutegemea shukrani ya maneno kutoka kwao bali wanabakia kuwa na wajibu wa kukutii na kukuheshemu kwa nafasi yako.
 
Mungu aliyekuumba ni wajibu wake kukupa mahitaji yako au ni hiari?
 
Ni makosa kulingana na msimamo wako na malezi yako sisi tulivyolelewa hata leo hii nikikukopesha wewe pesa kesho ukinirejeshea nitakupa shukran hata kama ni haki yangu kwasababu haipunguzi chochote kwangu zaid ya kuzidisha upendo baina yetu
 
Huwa nikiwa ugenini huwa napata tabu kushukuru kwanza kuna muda hadi huwa nasahau maana sisi nyumban hatukuwa na utaratibu huo

Pia huwa hadi nakosea,unakuta chakula ni cha mchana lakin nasema asante kwa chai
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…