Nimepiga marufuku watoto wangu kwenda kanisani

Baada ya kuona ujinga mambo ya makanisani nimeona nipige marufuku watoto wangu kuwa brain washed na mambo ya kanisa na aina zote za imani badala yake nawafùndisha life manners mwenyewe.Kama wataamua kwenda kwenye imani yoyote wafanye baada ya kutoka kwenye himaya yangu.
Mke wangu kwa vile tulikutana ukubwani mi nimeachana nae aendelee kuwa nyumbu wa huu ujinga wa kuwa na matumaini ya kwenda mbinguni.
SERA YANGU:Mbingu yangu ni hii good life niliyo nayo kwa sasa nikifikwa na majanga basi itakuwa jahannam yangu.
KAMA UNAUNGANA NA MIMI GONGA LIKE TUJUANE
Umechelewa sana kujua me nishaamua kuachana na haya mambo kitambo!!
 
Naungana na mtoa mada, Samaki mkunje angali mbichi.....

kwa nchi zilizoendelea mtoto kusema hana Dini ni kitu cha kawaida sana ila kwa hizi nchi za kishenzi za Dunia ya Tatu ndo watu wanashangaa, acha mabadiliko yaanze huu upuuzi hata mimi kwa mwanangu ni marufuku.
Wajapan kwa mfano wengi hawaamini kwenye hizi dini 2 lakini ni mojawapo ya nchi zenye ustaarabu mkubwa. Watoto wanalelewa kwenye misingi ya nidhamu. Huku kwetu watu wanajifanya wamebobea kwenye dini lakini kuna ushenzi wa kila aina. Hajulikani kiongozi wala muumini . Shida sana. Kujua dini hakuzuii mtu kutenda maovu period.
 
watu hamuelewi mtaji wa kijamii vizuri

ni kama kuwa mwanaume halafu hufuatilii mpira vijiweni utakuwa unatoa macho tu

ndo dini sasa inakupa tiketi ya kuwa karibu na watu, haswa kwa watoto wadogo
Kuna watu ambao dini haijawahi kuwapa connection ,ikiwemo mimi. Naendaga kumtukuza Mungu tu basi. Connection zangu ziletokana na shule, vyuo na most of them kazini. Tena kazini ndio kuna connection kuliko kwingine kote.
 
Baada ya kuona ujinga mambo ya makanisani nimeona nipige marufuku watoto wangu kuwa brain washed na mambo ya kanisa na aina zote za imani badala yake nawafùndisha life manners mwenyewe.Kama wataamua kwenda kwenye imani yoyote wafanye baada ya kutoka kwenye himaya yangu.
Mke wangu kwa vile tulikutana ukubwani mi nimeachana nae aendelee kuwa nyumbu wa huu ujinga wa kuwa na matumaini ya kwenda mbinguni.
SERA YANGU:Mbingu yangu ni hii good life niliyo nayo kwa sasa nikifikwa na majanga basi itakuwa jahannam yangu.
KAMA UNAUNGANA NA MIMI GONGA LIKE TUJUANE
Utajutia uamuzi huo hadi unashuka kaburini, waulize waliokaa Ulaya watakuambia kukosa kanisa kumewafanya jamii ya aina gani
 
Ulaya gani hiyo inauzia watu kuabudu. Mbona unaweza kuabudu vizuri tu ukiwa kule.
Huyo anachanganya mambo wala haelewi alichosndika.

Mfano mimi nilikwenda Ujerumani kuna makanisa mengi tu lakini vijana hawaoni umuhimu wa kanisa wala Mungu na wana sababu zao.

Chamoto zao zote zinamalizwa na wataalam wao, kuanzia afya, elimu, miundombinu nakadharika.

Sasa hawa issue ya kanisa ni ngumu kidogo kwao maana wamezaliwa na kukuwa na kuamini binadamu anaweza kufanya yote.

Ujerumani kuna Waturuki wengi sana hawa ni waislamu ndio angalau kama wanatangaza kitu kipya kupromote Islam na wapo vijana kweli wanaingia uislamu waone kuna jipya gani, wazungu wanapenda sana kujifunza kitu kipya, lakini Ukristo hauna jipya kwa ulaya.
 
Yeye anadhani duniani kote ni wajinga, watu tunaenda makanisani kwa sababu za kijamii, hayo mengine unayoubiliwa kwa sasa hayana nafasi kwa maisha ya leo haina tofauti sana na kuendekeza waganga, majini nk
Huhitaji Degree kuelewa nilichokiongea.
 
Utajutia uamuzi huo hadi unashuka kaburini, waulize waliokaa Ulaya watakuambia kukosa kanisa kumewafanya jamii ya aina gani
Kwa hiyo wewe unaeishi huko Mbagala rangi tatu unakula maisha na Yesu wako kuliko watu wa Ulaya sio?
 
Huyo anachanganya mambo wala haelewi alichosndika.

Mfano mimi nilikwenda Ujerumani kuna makanisa mengi tu lakini vijana hawaoni umuhimu wa kanisa wala Mungu na wana sababu zao.

Chamoto zao zote zinamalizwa na wataalam wao, kuanzia afya, elimu, miundombinu nakadharika.

Sasa hawa issue ya kanisa ni ngumu kidogo kwao maana wamezaliwa na kukuwa na kuamini binadamu anaweza kufanya yote.

Ujerumani kuna Waturuki wengi sana hawa ni waislamu ndio angalau kama wanatangaza kitu kipya kupromote Islam na wapo vijana kweli wanaingia uislamu waone kuna jipya gani, wazungu wanapenda sana kujifunza kitu kipya, lakini Ukristo hauna jipya kwa ulaya.
Kifupi makanisa yameonesha ni old version ya mtindo wa kuishi
 
Kuna watu ambao dini haijawahi kuwapa connection ,ikiwemo mimi. Naendaga kumtukuza Mungu tu basi. Connection zangu ziletokana na shule, vyuo na most of them kazini. Tena kazini ndio kuna connection kuliko kwingine kote.
Ujinga wa dini ni kukulia Muda na fedha tu kwa sababu tangu uanze kwenda wewe ndie mpelekaji wa hela ,matoleo, sadaka na vitu vingine kibao ila wao hawana cha kukupa zaidi ya neno So called la Mungu
 
Nina 50 yrs kanisani nimekanya mara ya mwisho miaka 30 iliyopita na sina taabu yoyote sijawahi pata kesi hata ya kusingiziwa, sinywi pombe sivuti sigara nipo na familia wao wanasali mie sisali maisha yanaendelea, sababu za kuto kusali ni binti aliyekuwa rafiki yangu (urafiki wa kawaida) alipata ujauzito halafu akasema ni wangu kwakuwa tulikuwa wanafunzi mie advance yeye o'level hii kesi ilinisimamisha masomo na kipindi hicho 1994 vipimo vya vinasaba hapa kwetu sijui, ikumbukwe sikuwahi kula huu mzigo nilisimamishwa masomo sasa binti akajifungua kopi ya mchungaji wa kanisa tulipokuwa tukisali na ilibainika baadae kuwa kumbe mchungaji ambaye pia alikuwa family friend wa familia ya binti aliepewa mimba kumbe ile ishu ilipangwa ili kuondoa fedheha kwa mchungaji na iliposemwa kuwa nimempa mimba haikuwa ajabu kwani nilikuwa karibu nae sana.

Baba mzazi wa binti alikula mlungula wa maana kuuficha upuuzi huu na kutokana na kusimamishwa masomo ikabidi baba anipeleke private nikamalizia huko sijajuaga huyo mchungaji na huyo binti waliishia wapi tangu siku hiyo nikimuona mchungaji yeyote ni bora Nikae na shetwani labda tutaelewana sijakanyaga kanisa lolote hadi leo na sitaki kusikia dude linaloitwa mchungaji upuuzi mtupu
 
Umepost shule niliyosoma mimi AZABOY na PUGU nikajua una akili kumbe bado we mtumwa wa hizo historia za uongo za kwenye biblia na misahafu unaambia Yesu alipaa mbinguni mara Mtume alienda na farasi mbinguni kuswali na wewe unaamini huku shule ulijifunza Gravitational force.
Mkuu kupost shule ndo akili?
 
Nina 50 yrs kanisani nimekanya mara ya mwisho miaka 30 iliyopita na sina taabu yoyote sijawahi pata kesi hata ya kusingiziwa, sinywi pombe sivuti sigara nipo na familia wao wanasali mie sisali maisha yanaendelea, sababu za kuto kusali ni binti aliyekuwa rafiki yangu (urafiki wa kawaida) alipata ujauzito halafu akasema ni wangu kwakuwa tulikuwa wanafunzi mie advance yeye o'level hii kesi ilinisimamisha masomo na kipindi hicho 1994 vipimo vya vinasaba hapa kwetu sijui, ikumbukwe sikuwahi kula huu mzigo nilisimamishwa masomo sasa binti akajifungua kopi ya mchungaji wa kanisa tulipokuwa tukisali na ilibainika baadae kuwa kumbe mchungaji ambaye pia alikuwa family friend wa familia ya binti aliepewa mimba kumbe ile ishu ilipangwa ili kuondoa fedheha kwa mchungaji na iliposemwa kuwa nimempa mimba haikuwa ajabu kwani nilikuwa karibu nae sana.

Baba mzazi wa binti alikula mlungula wa maana kuuficha upuuzi huu na kutokana na kusimamishwa masomo ikabidi baba anipeleke private nikamalizia huko sijajuaga huyo mchungaji na huyo binti waliishia wapi tangu siku hiyo nikimuona mchungaji yeyote ni bora Nikae na shetwani labda tutaelewana sijakanyaga kanisa lolote hadi leo na sitaki kusikia dude linaloitwa mchungaji upuuzi mtupu
Utetezi wa kijinga kabisa, hizo ni personal issues nothing to do with doctrine.
 
Peleka watoto kanisani. Watakapojitambua wataamua wenyewe.

Haya maisha unayotaka uwafunze, mwisho kila mwanao ataona anapaswa kuwa mwenyewe. Watakuona mzazi wao bladifakeni.
 
Kijana wangu akiwa mdogo nikampeleka kanisani,ule ukimya aliogopa sana.na kufikia kuimba nyimbo alipiga ukunga km ile anachinjwa.
Anyway ni Imani tu,
Kanisani nenda kwa roho yako mwenyewe inavyokutuma.
Kwa tuliowahi kupigwa spana za Duniani kanisa ndio kimbilio.
Si lazima utoe sadaka wala fungu la kumi.
Kwa manabii tonge sikanyagi
Niliwai kwenda enzi za Moses Kulola na Reinhard Bönke.
 
Imani pekee niliyo nayo ni Juu ya Familia yangu, Wazazi, Mke na Watoto pengine na ndugu wa karbu maana tangu nizaliwe Dini haijawah nisaidia chochote licha ya kwamba mimi nimeusaidia sana kwa kutenga muda na VIBUNDA vyangu ili isonge mbele.

Ni vyema mtu ajifunze dini kwanza aijue ili aikosoe vizuri kishaa aachane nayo kabisa, so waache wajifunze waujue ujinga wa huko huku nawe ukiwafundisha maisha mwisho wataamua wenyewe kuendelea kua wajinga au waelevu.

Kumbuka huna mbingu ya kumpeleka mtu ko tusilazimishane ili siku ya majuto tusilaumiane🤣
Ewaaa
 
Back
Top Bottom