Nimepigiwa simu na kutukanwa kisa kutoa maoni

Biashara sio Mapenzi eti mtavumiliana mapungufu yenu.

Lazima uambiwe mapungufu yako,kama hujirekebishi wateja wanahama.
 
Shida ni ileile naona comments nyingi wanasapoti ujinga. Mfanyabiashara lazima ukubali kupokea maoni na umjibu mteja kwa ustaarabu.

Shida ni kwamba mtu akiona tayari ana vimilioni kadhaa anajiona kama ameshamaliza kila kitu, yaani maoni ya mteja anachukulia kama usumbufu. Truste me. huyu mtu hawezi kufika mbali kamwe, yaani ataendelea kucheza levo yake kwa sababu hatokuwa na wateja endelevu.

Unamdharau mteja aliyeagiza mzigo wa laki 5 leo, kumbe baada ya muda angeagiza mizigo hata ya mamilioni na ungenufaika.

Facebook
wanahudumia mamilioni ya wateja wao ambao ni matajiri, lakini ukiwa na shida serious hata kama una biashara ya mtaji wa milioni 1 tu wanaweza kukupigia na ukaongea nao kwa muda wa dakika 30. Na wapo very very very polite. Yaani wanakubembeleza hata ukipanic hawakujibu maneno ya hovyo wanakujibu maneno laini kabisa.

Sasa ngozi nyeusi hii sijui tunakwama wapi, na hili naliona hata kwenye maduka, yaani kuna wakati unafika dukani unataka huduma, unakuta mtu anakudharau kwa jinsi tu ulivyo (yaani unaona kabisa anakudharau kwa maneno au ishara ya uso/facial expression).

Tubadilike , huduma nzuri kwa mteja ni kitu muhimu sana katika ukuaji wa biashara yako.
 
Mkuu yaani nilicho comment ilikua kama natoa maoni kuwa office zao zipo morocco ambapo ni kushoto sio kama ingekua kkoo kwa maana ya kurahisisha huduma na hii ni kwa faida yake yeye maana hata yule mtu wake wa delivery hana polite language. Lakini kanipigia na kunifoka tena anajiita mkurugenzi hahaha yaani mkurugenzi unanyanyua simu kupiga na kutukana mteja wako

Basi angeajiri mtu wa kudeal na customer wake yeye ashughulikie mambo mengine mazito AU AKASOME NAMNA YA KUDEAL NA WATU
 
Customer care ni muhimu, we fikiria kampuni kama PayPal na kimpuni kubwa sana na worth millions of dollars, lakini hata uwe na tatizo la $3 watakusikiliza hata uwasumbue siku tatu mpaka uelewe au kama tatizo walisort.
Watanzania customer service hatuna. Mtu hajali kumpoteza mteja kisa tu anaingiza ela tayari
 
Alitakiwa kuchukulia very positive, na hata kama ni kitu labda ambacho haki make sense kibiashara, angeweza tu kujibu asante sana mteja wetu kwa maoni yako, tutayafanyia kazi kwa kadri ya mahitaji na mipango ya kampuni.
 
Bwana wee kuna mfanyakazi wao mmoja yule anaijua kazi angalau angemuweka yule adeal na wateja yeye kama navyojiita mkurugenzi akae pembeni sio kila jambo mkurugenzi ujibu utajibu mangapi
 
Maoni umeyatoaje? Usikute uliandika kwa jazba na matusi pia au kama ni simu tornation uliyotumia haikua rafiki
 
Customer retention Ni msamiati kibongo bongo.
 
Mshitaki,ila unaushahidi???
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…